1
Maneno ya Aguri mwana wa Yake mausia: Mtu huyu alimwambia Ithieli, kwa Ithiel na Ukali:
2
Hakika nipo kama mnyama kuliko mwanadamu na sina ufahamu wa wanadamu.
3
Sijajifunza hekima, wala sina maarifa ya Mtakatifu.
4
Je ni nani amekwenda juu mbinguni na kurudi chini? Je ni nani aliyekusanya upepo kwenye mikono yake? Je ni nani aliyekusanya maji kwenye kanzu? Je ni nani aliyeziimarisha ncha za dunia yote? Jina lake ni nani, na jina la mtoto wake ni nani? Hakika unajua!
5
Kila neno la Mungu limejaribiwa, yeye ni ngao kwa wale wanaokimbilia kwake.
6
Usiyaongezee maneno haya, au atakukemea, na utathibitishwa kuwa mwongo.
7
Vitu viwili ninakuomba, usivikatalie kwangu kabla sijafa:
8
Majivuno na uongo viweke mbali nami. Usinipe umasikini wala utajiri, nipe tu chakula ninachohitaji.
9
Maana nikipata vingi zaidi, nitakukana wewe na kusema, " Yehova ni nani?" Au kama nitakuwa masikini, nitaiba na kukufuru jina la Mungu wangu.
10
Usimkashifu mtumwa mbele ya bwana wake, au atakulaani na utapata hatia.
11
Kizazi ambacho kinachomlaani baba yao na hakimbariki mama yao,
12
kizazi hicho ni safi katika macho yao wenyewe, lakini hawajaoshwa uchafu wao.
13
Hicho ni kizazi jinsi gani macho yao yana kiburi na kope zao zimeinuka juu! -
14
kuna kizazi ambacho meno yao ni upanga, na mifupa ya taya zao ni visu, ili waweze kumrarua masikini wamtoe duniani na mhitaji atoke miongoni mwa wanadamu.
15
Ruba ana mabinti wawili, " Toa na Toa" wanalia. Kuna vitu vitatu ambavyo havitosheki, vinne ambavyo havisemi, "Inatosha":
16
Kuzimu, tumbo tasa, nchi yenye kiu kwa maji, na moto usiosema, "Inatosha."
17
Jicho ambalo linamdhihaki baba na kudharau utii kwa mama, macho yake yatadonolewa na kunguru wa bondeni, na ataliwa na tai.
18
Kuna vitu vitatu ambavyo vinanishangaza, vinne ambavyo sivifahamu:
19
njia ya tai angani; njia ya nyoka juu ya mwamba; njia ya meli kwenye moyo wa bahari; na njia ya mtu pamoja mwanake kijana.
20
Hii ni njia ya mzinzi anakula na kufuta kinywa chake na kusema, "sijafanya ubaya wowote."
21
Chini ya vitu vitatu dunia hutetemeka na vinne haiwezi kuvivumilia:
22
mtumwa anapokuwa mfalme; mpumbavu anaposhiba vyakula;
23
mwanamke anayechukiwa anapoolewa; kijakazi anapochukua nafasi ya mkuu wake.
24
Vitu vinne duniani ni vidogo na bado vinabusara:
25
mchwa ni viumbe ambao sio imara, lakini huandaa chakula chao wakati wa hari,
26
Wibari siyo viumbe wenye nguvu, lakini hutengeneza makazi yake kwenye miamba.
27
Nzige hawana mfalme, lakini wote wanamwendo wa mpangilio.
28
Kama mjusi, unaweza kumkunja kwa mikono yako miwili, lakini wanapatikana katika majumba ya wafalme.
29
Kuna vitu vitatu ambavyo ni fahari katika mwendo na vinne ambavyo ni fahari katika namna ya kutembea:
30
simba, aliyeimara miongoni mwa wanyama wala hajiepushi na kitu chochote;
31
jogoo anayetembea kwa mikogo; mbuzi; na mfalme ambaye askari wapo kando yake.
32
Kama umekuwa mpumbavu, jitukuze mwenyewe, au kama umekuwa ukisimamia vibaya- weka mkono wako juu ya kinywa chako.
33
Kama kusuka maziwa hufanya siagi na pua ya mtu hutoa damu kama imepigwa, basi matendo yanayofanywa kwa hasira huzalisha mafarakano.