1
Jina jema huchaguliwa dhidi ya utajiri mwingi na fadhila ni bora kuliko fedha na dhahabu.
2
Watu matajiri na masikini wanafanana katika hili Yehova ni muumba wao wote.
3
Mtu mwenye hekima huiona taabu na kujificha mwenyewe, bali mjinga huendelea mbele na huumia kwa ajili yake.
4
Thawabu ya unyenyekevu na kumcha Yehova ni utajiri, heshima na uzima.
5
Miiba na mitego hulala katika njia ya wakaidi; yeye anayelinda maisha yake atakuwa mbali navyo.
6
Mfundishe mtoto njia inayompasa na wakati akiwa mzee hatayaacha mafundisho hayo.
7
Watu matajiri huwatawala watu masikini na mwenye kukopa ni mtumwa wa yule anayekopesha.
8
Yule anayepanda udhalimu atavuna taabu na fimbo ya hasira yake itanyauka.
9
Mwenye jicho la ukarimu atabarikiwa, maana anashiriki mkate wake pamoja na masikini.
10
Mfukuze mbali mwenye dhihaka, na ugomvi utaondoka, mashindano na matukano yatakoma.
11
Anayependa moyo safi na mwenye maneno ya neema, atakuwa rafiki yake mfalme.
12
Macho ya Yehova huyaangalia maarifa, bali huyapindua maneno ya wadanganyifu.
13
Mtu mvivu husema, " Kuna simba mtaani! Nitauwawa sehemu za njia."
14
Kinywa cha malaya ni shimo lenye kina kirefu; hasira ya Yehova huchochewa dhidi ya yule anayetumbukia ndani yake.
15
Upumbavu umefungwa katika moyo wa mtoto, lakini marudi ya fimbo huutoa.
16
Anayewanyanyasa watu masikini ili kuongeza mali yake, au kuwapa matajiri, atakuwa masikini.
17
Tega sikio lako na usikilize maneno ya wenye busara na tumia moyo wako katika maarifa yangu,
18
maana itakuwa furaha kwako kama utayaweka ndani yako, kama yote yatakuwa katika midomo yako.
19
Basi tumaini lako liwe kwa Yehova, ninayafundisha kwako leo hata kwako.
20
Sijakuandikia wewe misemo thelathini ya mafundisho na maarifa,
21
kwa kukufundisha kweli katika maneno haya yenye uaminifu, ili uwe na majibu yenye kutegemewa kwa waliokutuma?
22
Usimwibie masikini kwa sababu ni masikini, au kumponda kwenye lango,
23
maana Yehova ataitetea kesi yao, na atawaibia uzima wale waliowaibia masikini.
24
Usifanye urafiki na mtu mwenye kutawaliwa na hasira na wala usiambatane pamoja na mwenye hasira kali,
25
au utajifunza njia zake na utakuwa chambo kwa nafsi yako.
26
Usiwe miongoni mwao wapigao mikono, mwenye kuahidi madeni.
27
Kama umekosa njia za kulipa, nini kitaweza kuzuia mtu kuchukua kitanda chako chini yako?
28
Usiondoe jiwe la mpaka la wahenga ambalo baba zako wameweka.
29
Je umemwona mtu aliyeuwawa kwenye kazi yake? Atasimama mbele ya wafalme; hatasimama mbele ya watu wa kawaida.