Sura 7

1 Mafarisayo na baadhi ya waandishi ambao walikuwa wametokea Yerusalemu walikusanyika wakimzunguka Yesu. 2 Na mafarisayo wandishi waliona baadhi ya wanafunzi wake walikula chakula kwa mikono najisi; ambayo haikuoshwa mpaka kwenye kiwiko. 3 (kwa sababu Mafarisayo na Wayahudi wote hawali mpaka wameosha mikono yao vizuri; wanashikilia utamaduni wa wazee kwa muda wete. 4 Mafarisayo wanaporudi kutoka mahali pa soko, hawali mpaka wameoga kwanza. Na kuna sheria zingine ambazo wanazifuata kabisa, ikiwa ni pamoja na kuosha vikombe, masufuria, vyombo vya shaba, na hata viti vinavyotumika wakati wa chakula.) 5 Mafarisayo na waandishi walimuuliza Yesu, " Kwa nini wanafunzi wako hawatii na kufata utamaduni wa wazee wetu, kwani wanakula chakula pasipo kunawa mikono?" 6 Lakini yeye aliwaambia, "Isaya alitabiri vizuri kuhusu ninyi mafarisayo na wandishi wanafiki, aliandika, 'Watu hawa wananiheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali na Mungu. 7 Wananifanyia ibaada zisizo na maana, wakifundisha sheria za wanadamu kama mapokeo yao.' 8 Mmeiacha sheria ya Mungu na kushikilia kwa haraka tamaduni za wazee wenu." 9 Yesu akasema akawambia, "Mmezikataa amri za Mungu kwa haraka ili kwamba mtunze tamaduni zenu! 10 Kwa kuwa Musa alisema, 'mheshimu baba yako na mama yako,' na 'Yeye amtukanaye baba yake au mama yake hakika atakufa.' 11 Lakini mnasema, 'kama mtu akisema kitu cha kumwahidi baba yake au mama, cha "Msaada wowote ambao mngepokea kutoka kwangu ni hazina ya Hekalu,"' (hiyo ni kusema kwamba, 'nimeutoa kwa Mungu') 12 hivyo haumruhusu mtoto kufanya jambo lolote kwa ajili ya baba au mama yake. 13 Mnazifanya amri za Mungu kuwa bure kwa kuleta tamaduni zenu. Mnafanyanya mengi ya jinsi hiyo yanayofanana." 14 Yesu aliwaita makutano tena na kuwaambia, "Mnisikilize mimi, ninyi nyote, na mpatekunielewa. 15 Hakuna chakula chochote kitokacho nje ya mtu ambacho chaweza kumchafua mtu kiingiapo ndani yake. Bali ni kile asemacho mtu ndicho kimchafuacho. 16 "Kama mtu yeyote ana uelewa na jambo hili, na aelewe." 17 Yesu alipowaacha makutano na kuingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kuhusu mfano huo. 18 Yesu akasema, "Na ninyi pia bado hamjaelewa? Hamuoni kwamba chakula chochote kimuingiacho mtu hakiwezi kumchafua, 19 kwa sababu hakiwezi kwenda kwenye moyo wake, lakini kinaingia katika tumbo lake na kisha kinapita kwenda chooni." Kwa maelezo haya Yesu alivifanya vyakula vyote kuwa safi. 20 Yesu alisema, "kile ambacho kinamtoka mtu ndani ndicho kimchafuacho. 21 Kwa kuwa hutoka ndani ya mtu, ndani ya moyo, hutoka mawazo maovu, zinaa, wizi, mauaji, 22 uasherati, tamaa mbaya, uovu, udanganyifu, kujamiiana, wivu, kashfa, majivuno, ujinga. 23 Maovu haya yote yanatoka ndani, ya moyo ndiyo yale yamchafuayo mtu." 24 Yesu aliamka kutoka pale alipokuwa ameketi na kuondoka kwenda katika mkoa wa Tiro na Sidoni. Aliingia ndani na hakutaka mtu yeyote ajue kuwa alikuwa hapo, lakini haikuwezekana kumficha. 25 Lakini ghafla mwanamke alikuja kwe Yesu, ambaye mtoto wake mdogo alikuwa na roho mchafu, alisikia habari zake, akaja, na kupiga magoti miguuni pake Yesu. 26 Mwanamke huyo alikuwa Myunani, wa kabila la Kifoeniki. Alimsihi yesu amfukuze pepo atoke kwa binti yake. 27 Yesu akamwambia mwanamke, "Waache watoto walishwe kwanza, chakula, kwa kuwa sio sawa kuuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa." 28 Lakini yule mwanamke akamjibu na kusema, "Ndiyo Bwana, hata mbwa chini ya meza hula mabaki ya chakula cha watoto." 29 Yesu akamwambia, "Kwa kuwa unaamini hivi, uko huru kwenda. Pepo ameshamtoka binti yako." 30 Mwanamke alirudi nyumbani kwake na akamkuta binti yake amelala kitandani, na pepo alikuwa amemtoka. 31 Yesu alitoka tena nje ya mkoa wa Tiro na kupitia Sidoni kuelekea Bahari ya Galilaya mpaka kanda ya Dikapolisi. 32 Na wakamletea mtu aliyekuwa kiziwi na alikuwa hawezi kuzungumza vizuri, walimsihi Yesu aweke mikono juu yake. 33 Yesu alimtoa mtu huyu nje ya kusanyiko kwa siri, na akaweka vidole vyake kwenye masikio yake, na baada ya kutema mate, aligusa ulimi wa yule mtu. 34 Yesu alitazama juu mbinguni, akahema na kumwambia, "Efata," hiyo ni kusema "funguka!" 35 Na muda ule ule masikio yakafunguka, na kilichokuwa kimezuia ulimi kiliharibiwa na akaweza kuongea vizuri. 36 Na aliwaamuru wasimwambie mtu yeyote. Lakini kadri alivyowaamuru, ndivyo walivyotangaza habari hizo kwa wingi. 37 Hakika walishangazwa, na kusema, "Amefanya kila kitu vizuri. Hata amewafanya viziwi kusikia na mabubu kuongea."