sura 6

1 Na akaondoka hapo na kwenda mjini kwao nazarethi, na wanafunzi wake wakamfuata. 2 Sabato ilipofika, alianza kufundisha katika Sinagogi. Watu wengi walimsikiliza na wakashangazwa. Wakasema, "Amepata wapi mafundisho haya?" "Ni hekima ya namnagani hii aliyo ipata?" "Huyu Yesu anatendaje miujiza hii kwa mikono yake?" 3 "Je huyu si yule mtoto wa seremala, mwana wa Mariamu na ndugu zake ambao ni Yakobo, Yose, Yuda na Simioni? Je dada zake si tunaishinao hapa hapa pamoja nasi?" Watu wa nazarethi hawakufurahishwa na mafundisho ya Yesu. 4 Yesu akawaambia, "Nabii hapati heshima, katika mji wake hata kwa ndugu zake wa nyumbani mwake." 5 Hivyo Yesu hakuweza kutenda miujiza hapo, nazarethi, ila aliwawekea mikono wagonjwa wachache akawaponya. 6 Alishangazwa sana kwa sababu ya kutokuamini kwao. Kisha alivitembelea vijiji vya jirani akifundisha. 7 Aliwaita wale wanafunzi kumi na wawili akaanza kuwatuma wawili wawili. Aliwapa mamlaka juu ya pepo wachafu, 8 na kuwaamuru wasichukue chochote wanapokwenda isipokuwa fimbo tu. Wasichukue chakula, wala mkoba, wala fedha kibindoni; 9 lakini wavae viatu, na siyo kanzu mbili. 10 Na akawaambia, "Nyumba yoyote mtakayoingia, kaeni hapo mpaka mtakapoondoka. 11 Na mji wowote usipowapokea wala kuwasikiliza, ondokeni kwao, kung'uteni mavumbi ya miguu yenu, iwe ushuhuda kwao." 12 Nao wakaenda wakiwaambia watu watubu na kuacha dhambi zao. 13 Wanafunzi walipo kwenda Waliyfukuza mapepo wengi, na waliwapaka mafuta wagonjwa na wakaponywa. 14 Mfalme Herode aliposikia kuhusu, habari za Yesu jinsi anavyo ponya na kufukuza mapepo, na kutambulika kwa watu. Baadhi ya watu walisema, "Itakuwa Yohana mbatizaji amefufuka na kwa sababu hiyo, hii nguvu ya miujiza inafanya kazi ndani yake." 15 Baadhi watu wakasema, "Huyu ni Eliya,"Ambaye Mungu aliahidi kwamba ataludi, wengine wakasema, "Huyu ni nabii, kama mmoja wa wale manabii wa zamani." 16 Lakini Herode aliposikia haya akasema, "Yohana, niliagiza askari wamkate kichwa amefufuka." 17 Maana Herode mwenyewe alituma askari Yohana akamatwe na alimfunga gerezani kwa sababu ya Herodia (mke wa kaka yake ambaye ni Filipo) kwa sababu Herode alikuwa amemuoa. 18 Kwa maana Yohana alimwambia Herode, "Si halali kumuoa mke wa kaka yako." 19 Lakini Herodia alianza kumchukia na alikuwa akitaka kumuuaYohana, lakini hakuweza, Hivyo alitafuta njia ya kumuua 20 maana Herode alimwogopa Yohana; alijua kwamba ni mwenye haki mtu mtakatifu, na alimwacha salama. Na alipoendelea kumsikiliza Yohana alihuzunika sana, lakini alifurahiya mazungumzo yake kuyasikiliza. 21 Hata ulipofika wakati mwafaka ikawa imekaribia siku ya kuzaliwa Herode akawaandalia moafisa wake sherehe, na makamanda, na viongozi wa Galilaya. 22 Ndipo binti yake Herodia akaingia na kucheza mbele yao, akamfurahisha mfalme Herode na wageni walioketi wakati wa chakula cha jioni. Ndipo mfalme akamwambia binti, "Niombe chochote unachotaka nami nitakupa." 23 Akamwekea kiapo na kusema, chochote utakachoniomba, nitakupa, hata nusu ya ufalme wangu ninao miliki." 24 Binti akatoka nje ya chumba cha sherehe akamuuliza mama yake, "Niombe nini?"Mama Akasema omba, "Kichwa cha Yohana Mbatizaji." 25 Kwa haraka sana akaingia kwa mfalme akaanza kusema, "Nataka unipatie juu ya sahani, kichwa cha Yohana Mbatizaji." 26 Mfalme alisikitishwa sana na ombi la binti, lakini kwa sababu ya kiapo chake na kwa ajili ya wageni, hakuweza kumkatalia ombi lake. 27 Hivyo, mfalme akatuma askari kati ya walinzi wake na kuwaagiza kwenda kumletea binti kichwa cha Yohana. Mlinzi alikwenda kumkata kichwa Yohana akiwa kifungoni. 28 Akakileta kichwa chake kwenye sahani na kumpatia binti, na binti akampa mama yake. 29 Na wanafunzi wa Yohana waliposikia hayo, walikwenda kuuchukua mwili wake wakaenda kuuzika kaburini. 30 Na mitume, walipo ludi kutoka kuhubiri walikusanyika pamoja mbele ya Yesu, wakamweleza yote waliyofanya na waliyoyafundisha. 31 Naye akawaambia, "Njooni ninyi wanafunzi wangu mahali pa faragha na tupumzike kwa muda." Watu wengi walikuwa wanakuja kwa mitume na kuondoka, hata hawakupata muda wa kula chakula. 32 Hivyo wakapanda mashua wakaenda mahali pa faragha pasipokuwa na watu. 33 Lakini watu waliwaona Yesu na wanafunzi wake wakiondoka na wengi wakawatambua, kwa pamoja walikimbia kwa kupitia njia ya miguu kutoka miji yote, nao wakafika pwani kabla yao. 34 Yesu na wanafunzi wake Walipofika pwani, aliona umati mkubwa na akawahurumia, kwa sababu walikuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. Na akaanza kuwafundisha mambo mengi. 35 Muda uliendelea sana ilikuwa ni jioni, wanafunzi wakamjia wakamwambia,"Hapa ni mahali hakuna makazi ya watu, na muda umeendelea sana. 36 Uwaage watu waende miji ya jirani na vijiji ili wakajinunulie chakula." 37 Lakini akawajibu akisema, "Wapeni ninyi chakula." Wakamwambia, "Tunaweza kwenda na kununua mikate yenye thamani ya dinari mia mbili na kuwapa wale?" 38 Akawauliza," Mna mikate mingapi? Nendeni mkaangalie." walipotazama wakamwambia, "Mikate mitano na samaki wawili." 39 Akawaamuru watu waketi katika makundi makundi, juu ya majani mabichi. 40 Wakawaketisha katika makundi; makundi ya mamia kwa hamsini. 41 Kisha akachukua mikate mitano na samaki wawili, na kutazama mbinguni, akamshukuru, Mungu, kisha akawapa wanafunzi, ili wawape makutano. Wakaiweka mbele ya umati. Na kisha aligawa samaki wawili na kuwapa watu wote. 42 Watu wote walikula hadi wakatosheka. 43 Walikusanya vipande vya mikate iliyobaki, Vikajaa vikapu kumi na viwili, na pia vipande vya samaki. 44 Na walikuwa wanaume elfu tano waliokula mikate na samaki. Lakini wanawake na watoto hawakuhesabiwa. 45 Kisha akawaambia wanafunzi wake, wapande kwenye mashua waende sehemu nyingine, hadi Bethsaida, wakati Yeye akiwaaga makutano. 46 Watu walipokwisha kuondoka, Yesu akaenda mlimani kuomba. 47 Ilipofika jioni, na mashua yao ilikuwa katikati ya bahari, naye Yesu alikuwa peke yake pwani. 48 Na aliwaona wakitaabika kupiga makasia kwa sababu upepo uliwazuia. Ilipokaribia asubuhi akawaendea, akitembea juu ya maji, na alitaka kuwapita. 49 Lakini walipomwona Yesu anatembea juu ya maji, wakaingiwa na wasiwasi wakidhani ni mzimu wakapiga kelele. 50 kwa sababu walimwona wakajawa na hofu. Mara Yesu akasema nao akawaambia, "Muwe na ujasiri! ni mimi! Msiwe na hofu." 51 Akaingia ndani ya mashua, na upepo ukaacha kuvuma, nao wakamshangaa sana. 52 Hivyo hawakuwa wameelewa maana ya ile mikate. Maana akili zao zilikuwa zimeshindwa kuelewa. 53 Nao walipovuka ng'ambo, walifika nchi ya Genesareti mashua ikatia nanga. 54 Walipotoka nje ya mashua, watu wakamtambua, Yesu na wanafunzi wake. 55 Wakakimbia kutangaza katika mkoa mzima na wakaanza kuwaleta watu wagonjwa kwa machela, kila waliposikia amekuja . 56 Popote alipoingia katika vijiji, au mjini, au katika nchi, watu waliwaweka wagonjwa mahali pa soko, na watu wakamwomba awaruhusu wagonjwa kugusa pindo la vazi lake. Na wote waliomgusa waliponywa.