sura 5

1 Walikuja mpaka upande wa bahari, katika mkoa wa Gerasi 2 Na ghafla wakati Yesu alipokuwa akitoka nje ya mtumbwi, alikutana na mtu mwenye roho mchafu akija kwake kutoka makaburini. 3 Mtu huyu aliishi makaburini. Hakuna aliyeweza kumzuia. 4 Alikuwa amefungwa muda mwingi kwa pingu na minyororo. Aliikata minyororo na pingu zake alizivunja. Hakuna hata mmoja aliyekuwa na nguvu za kumshinda. 5 Usiku na mchana alikuwa makaburini na milimani, akipiga kelele na kulia na kujikata kwa mawe makali. kama mapepo yalivyo mtumikisha. 6 Alipomwona Yesu kwa mbali, alimkimbilia na kuinama mbele yake. 7 Akalia kwa sauti kuu, akasema "Wataka kutufanyia nini, Yesu, Mwana wa Mungu aliye Juu sana? Nakuomba sana kwa huruma zake Mungu mwenyewe, usinitese." 8 Yesu alimwambia , "Mtoke mtu huyu, ewe roho mchafu." 9 Naye alimwuliza, "Jina lako ni nani?" Naye alimjibu, "Jina langu ni Legion, kwa kuwa tuko wengi." 10 Alimwomba tena na tena usitupeleke nje ya mkoa. 11 Palikuwa na kundi kubwa la nguruwe likichungwa juu ya kilima, 12 Mapepo yaliomba , yakisema, "Turuhusu tuingie, ndani ya nguruwe." 13 Hivyo aliwaruhusu; roho wachafu walimtoka yule mtu na kuingia ndani ya nguruwe, nao nguruwe walitelemka chini ya kilima mpaka baharini, yapata nguruwe elfu mbili walizama baharini. 14 Na wale waliokuwa wakichunga nguruwe walikimbia kwenda kutoa taarifa ya kilichotokea katika mji na. Ndipo watu wengi walitoka kwenda kuona kilichotokea. 15 Walikuja kwa Yesu na walimwona mtu aliyekuwa akipagawa na mapepo, amekaa chini, amevikwa, na nguo akiwa na akili zake timamu, nao waliogopa. 16 Wale waliokuwa wameshudia kilichotokea kwa mtu aliyekuwa akipagawa na mapepo waliwaambia jinsi alivyo ponywa na pia kuhusu nguruwe. 17 Nao walianza kumfukuza Yesu aondoke katika mkoa wao. 18 Na alipokuwa akiingia ndani ya mtumbwi, mtu aliyekuwa akipagawa na mapepo aliomba kwamba aende pamoja naye. 19 Lakini hakumruhusu, lakini alimwambia, "Nenda nyumbani kwako na kwa watu wako, na uwaambie alichokufanyia Bwana, na huruma aliyokupa." 20 Hivyo alienda na alianza kutangaza mambo makuu ambayo Yesu amefanya kwake maeneo yote ya Dekapoli, na kila mmoja alistaajabu. 21 Na wakati Yesu alipovuka tena upande mwingine, ndani ya mtumbwi, umati mkubwa ulikusanyika kumzunguka, alipokuwa kando ya bahari. 22 Na mmoja wa kiongozi wa sinagogi, aliyeitwa Yairo, alikuja, na alipomwona, alianguka miguuni pake. 23 Akamsihi zaidi na zaidi, akisema, " Binti yangu mdogo anakaribia kufa. Ninakusihi, njoo na uweke mikono yako juu yake ili aweze kupata afya na kuishi." 24 Hivyo alikwenda pamoja naye, na umati wa wanafunzi ulimfuata nao walimzonga karibu wakimzunguka. 25 Wakiwa njiani wakienda kwa Yeiro. Kulikuwa na mwanamke ambaye damu yake ilikuwa inamtoka kwa miaka kumi na miwili. 26 Aliteseka vya kutosha chini ya matabibu wengi na alitumia kila kitu alichokuwa nacho. Hata hivyo hakupata msaada kwa chochote, lakini siku baada ya siku hali yake ilizidi kuwa mbaya. 27 Alisikia habari za Yesu. Hivyo alikuja nyuma ya Yesu wakati alipokuwa akitembea ndani ya umati, naye aliligusa vazi lake. 28 Kwa kuwa alisema, "Kama nikiyagusa mavazi yake tu, nitakuwa mzima." 29 Alipomgusa, kutokwa damu kulikoma, na alijisikia katika mwili wake kwamba ameponywa kutoka kwenye mateso yake. 30 Na ghafla Yesu aligundua ndani yake mwenyewe kwamba nguvu zimemtoka. Na aligeuka huku na huku katikati ya umati wa watu akauliza, "Ni nani aliyeligusa vazi langu?" 31 Wanafunzi wake walimwambia, "Unaona umati huu wanakufuta, wamekuzunguka nawe wasema, 'Ni nani aliyenigusa?'" 32 Lakini Yesu alitazama huku na huku akimtafuta aliye mgusa. 33 Mwanamke, akijua kilichotokea kwake, aliogopa na kutetemeka. Alikuja na alianguka chini mbele yake na kumwambia ukweli wote. Ni miminiliye kugusa. 34 Yesu Alisema, "Binti, imani yako imekufanya uwe mzima. Enenda kwa amani na uponywe ugonjwa wako." 35 Yesu alipokuwa akizungumza, baadhi ya watu walikuja kutoka kwa kiongozi wa Sinagogi, wakamwambia Yeiro wakisema, "Binti yako amekufa. Kwa nini kuendelea kumsumbua mwalimu?" 36 Lakini Yesu aliposikia ambacho walikisema, alimwambia kiongozi wa Sinagogi, "Usiogope. Amini tu." 37 Hakumruhusu yeyote kuongozana naye, isipokuwa Petro, Yakobo, na Yohana, ndugu yake Yakobo. 38 Walikuja nyumbani kwa kiongozi wa Sinagogi naye aliona vurugu, za kulia kwingi na kuomboleza. 39 Alipoingia nyumbani, aliwaambia, "Kwa nini mnahuzunika na kwa nini mnalia? Mtoto hajafa bali amelala." 40 Walimcheka, lakini yeye, aliwatoa wote nje, alimchukua baba wa mtoto na mama na wanafunzi wake pamoja naye, na aliingia ndani alimokuwa mtoto. 41 Aliuchukua mkono wa mtoto na alimwambia, "Talitha koum," ambayo ni kusema, "Binti mdogo, nakuambia, amka." 42 Ghafla mtoto aliamka na kutembea (kwa kuwa alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili). Na ghafla walishikwa na mshangao mkubwa. 43 Aliwaamuru kwa nguvu kwamba hakuna yeyote anapaswa kujua kuhusu hili. Na aliwaambia wampatie yule binti chakula.