Sura 3

1 Basi katika mwaka wa kumi na nane wa Yehoshefati mfalme wa Yuda, Yoramu mwana wa Ahabu alianza kutawala juu yata Israeli katika Samaria; alitawala miaka kumi na miwili. 2 Alifanya yaliyo maovo machoni pa BWANA , lakini si kama baba yake na mama yake; kwa kuwa aliiondoa ile nguzo ya mungu wa Baali ambayo baba yake aliitengeneza. 3 Hata hivyo alishikilia dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambaye alisababisha Israeli kufanya dhambi; wala hakuziacha mbali nao. 4 Basi Mesha mfalme wa Moabu alifuga kondoo. Alikuwa akimpatia mfalme wa Israeli kondoo 100, 000 na manyoya ya kondoo dume 100, 000. 5 Ila baada ya Ahabu kufa, yule mfalme wa Moabu aliasi dhidi ya mfalme wa Israeli. 6 Hivyo Mfalme Yoramu akaondoka Samaria katika muda huo kuwahamasisha Waisraeli wote kwa ajili ya vita. 7 Akatuma mjumbe kwa Yehoshafati mfalme wa Yuda, akisema, "Mfalme wa Moabu ameasi dhidi yangu. Je mtakwenda pamoja nami kupigana dhidi ya Moabu?" Yehoshafati akajibu, "Nitaenda. Mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, farasi wangu ni kama farasi wako." 8 Ndipo akasema, "Tutawashambulia kwa njia gani?" Yehoshafati akajibu, "Kwa njia ya jangwa la Edemu." 9 Hivyo huyo mfalme wa Israeli, Yuda, na Edomu wakazunguka kwa muda wa siku saba. Hapakuwa na maji kwa ajili ya jeshi lao, wala kwa farasi au wanyama. 10 Basi mfalme wa Israeli akasema, "Hii ni nini? Yahwe amewaita wafalme watatu ili kutekwa mikononi mwa Moabu?" 11 Lakini Yehoshafati akasema, "Je hakuna nabii wa BWANA, ambaye tunaweza kufanya shauri kuhusu BWANA kupitia yeye?" Mtumishi mmoja wa wafalme wa Israeli akajibu na kusema, "Elisha mwana wa Shafati yuko hapa, ambaye alikuwa akimimina maji kwenye mikono ya Eliya." 12 Yehoshafati akasema, "Neno la Yahwe liko pamoja naye." Hivyo mfalme wa Israeli, Yehoshafati, na mfalme wa Edomu wakashuka chini kwenda kwake. 13 Elisha akamwambia mfalme wa Israeli, "Nifanye nini kwa ajili yako? Nenda kwa manabii wa baba na mama yako." Ndipo mfalme wa Israeli akamwambia, "Hapana, kwa sababu BWANA amewaita hawa wafalme watatu pamoja ili kuruhusu jeshi la Moabu liwateke." 14 Elisha akajibu, "Kama BWANA wa majeshi aishivyo, ambaye nimesimama mbele zake, hakika kama nisingemheshimu uwepo wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, nisingevuta usikivu kwako, au hata kukutazama. 15 Lakini sasa niletee mpiga kinanda." Ndipo alipokuja mpiga kinanda alipocheza, mkono wa BWANA ukaja juu ya Elisha. 16 Akasema, "BWANA asema hivi, 'Fanya hili bonde la mto mkavu lijae mahandaki.' 17 Kwa kuwa BWANA asema hivi, 'Hutaona upepo, wala hamtaona mvua, bali hili bonde la mto litajaa maji, na mtakunywa, ninyi na mifugo yenu na wanyama wenu wote.' 18 Jambo hili ni jepesi machoni pa BWANA. Pia atawapa ushindi juu ya hao Wamoabu. 19 Mtaiteka kila ngome ya mji na kila mji mzuri, kukata kila mti mzuri, kusimamisha chemichemi zote za maji, na kuharibu kila sehemu nzuri ya nchi na miamba." 20 Hivyo asubuhi karibia na muda wa kutoa sadaka ya kuteketeza, yakaja maji kutoka uelekeo wa Edomu; nchi ikajaa maji. 21 Ndipo wakati Wamoabu wote waliposikia kwamba wafalme wamekuja kupigana dhidi yao, walikusanyika pamoja, wote waliotakiwa kubeba silaha, na wakasimama mpakani. 22 Walitembea asubuhi na mapema na jua likang'aa kwenye maji. Wakati Wamoabu walipoyaona yale maji yaliyowaelekea, yanaonekana mekundu kama damu. 23 Wakatamka kwa hasira, "Hii ni damu! Yamkini hao wafalme wameharibiwa, na wameuana wao kwa wao! Sasa basi, Moabu, ngoja tuende tukawateke nyara!" 24 Wakati walipokuja kwenye kambi ya Israeli, Waisraeli wakawashtukiza na kuwashambulia Wamoabi, ambao walikimbia mbele yao. Hilo jeshi la Israeli waliwakimbiza hao Wamoabu hadi kwao wakiwaua. 25 Waliiharibu miji, na kila aina ya amani ya nchi kila mtu alirusha jiwe mpaka ulipojaa. Walizuia kila chemichemi ya maji na kukata chini miti mizuri yote. Kir-haresethi tu ndiyo ilichwa na mawe yake. Lakini hao maaskari wakawashambulia na makombeo wakiwazunguka na kuishambulia. 26 Ndipo Mfalme Mesha wa Moabu alipoona kwamba ameshindwa, alichukua watu hodari wa upanga 700 pamoja naye kwenda kwa mfalme wa Edomu, lakini walishindwa. 27 Ndipo akamchukua mtoto wake wa kwanza, ambaye angetawala baada ya yeye, na akamuudhi kwa kumtoa kama sadaka ya kuteketezwa juu ya ukuta. Hivyo, kulikuwa na hasira kubwa dhidi ya Israeli, na hao Waisraeli, na Jeshi la Israeli likamuacha mfalme Mesha na kurudi kwenye nchi yao.