Sura 23

1 Hivyo mfalme akawatuma wajumbe waliokuwa wamemzunguka wazee wote wa Yuda na wa Yerusalemu. 2 Kisha mfalme akapanda hadi kwenye nyumba ya BWANA, na watu wote wa Yuda na wenyeji wote wa Yerusalemu pamoja naye, na makuhani, manabii, na watu wote, kuanzia mdogo hadi mkubwa. Kisha akasoma masikioni kwao maneno yote ya kitabu cha agano ambalo lililokuwa limepatikana kwenye nyumba ya BWANA. 3 Mfalme akasimama karibu na nguzo na kufanya agano mbele ya Yahwe, kutembea pamoja na Yahwe na kukumbuka maagizo yake, kanuni zake, na sheria zake, kwa moyo wake wote na kwa roho yake yote, kuthibitisha maneno ya hili agano ambalo lililokuwa limeandikwa kwenye hiki kitabu. Hivyo watu wote wakakubaliana kusimama kwenye agano 4 Mfalme akamwamuru Hilkia yule kuhani mkuu, makuhani chini yake, na walinzi wa lango watoe kwenye hekalu vyombo vilivyokuwa vimetengenezwa kwa ajili ya Baali na Ashera, na kwa ajili ya nyota zote za mbinguni. Akavichoma moto Yerusalimu kwenye mashamba ya bonde la Kidroni na kubeba majivu yake kwenda Betheli. 5 5 Akawaondoa makuhani waliokuwa wanaabudu miungu ambao wafalme wa Yuda waliwachagua ili kwa ajili ya kufukiza ubani katika mahali pa juu kwenye miji ya Yuda na sehemu zinazoizunguka Yerusalemu wale waliokuwa wanachoma ubani kwa Baali, kwa jua na kwa mwezi, kwa sayari, na kwa nyota zote za mbinguni. 6 Akaiondoa Ashera kutoka kwenye hekalu la BWANA, nje ya Yerusalemu hata bonde la Kidroni na kuichoma hapo. Akaipiga kwenye mavumbi na kuyatupa yale mavumbi kwenye makaburi ya watu wa kawaida. 7 Akavisafisha vyumba vya makahaba ambao walikuwa kwenye hekalu la BWANA, ambako wanawake waliposhonea nguo kwa ajili ya Ashera. 8 Yosia akawaleta makuhani wote nje ya miji ya Yuda na kupanajisi mahali pa juu ambako makuhani walipokuwa wakichomea ubani, kutoka Geba hata Bersheba. Akapaharibu mahala pa juu kwenye malango ambayo yaliyokuwa ya kuingilia kwenda kwenye lango la Yoshua (liwali wa mji), upande wa kushoto wa lango la mji. 9 Ingawa makuhani wa mahali pa juu hawakuruhusiwa kuhudumu kwenye madhabahu ya BWANA katika Yerusalemu, wakala mikate isiyotiwa chachu miongoni mwa ndugu zao. 10 Yosia akainajisi Tofethi, ambayo ipo kwenye bonde la Ben Hinomu, ili kwamba mtu yeyote asimuweke mtoto wake wa kiume au binti yake kwenye moto kama sadaka kwa Moleki. 11 Akawachukua farasi ambao wafalme wa Yuda waliokuwa wametolewa kwa ajili ya jua. Walikuwa kwenye eneo la lango la kuingilia kwenye hekalu la BWANA, karibu na chumba cha Nathani Meleki, msimamizi mkuu wa nyumba ya mfalme. Yosia akayachoma yale magari ya farasi ya jua. 12 Yosia mfalme akayaharibu madhabahu yaliyokuwa kwenye dari ya juu ya chumba cha Ahazi, ambacho wafalme wa Yuda walikitengeneza, na madhabahu ambayo Manase aliyatengeneza kwenye behewa mbili za nyumba ya BWANA. Yosia akazivunga vipande vipande na kuvitupa kwenye bonde la Kidroni. 13 Mfalme akapaangamiza mahali pa juu magharibi mwa Yerusalemu, kusini mwa mlima wa uharibifu ambapo Sulemani mfalme wa Israeli alipajenga kwa ajili ya Ashtorithi, chukizo la Wamoabu; sanamu za karaha za Wasidoni; kwa Kemoshi, sanamu za karaha wa Moabu; na kwa Moleki, sanamu wa karaha wa watu wa Amoni. 14 Akazivunja nguzo za jiwe kuwa vipande vipande na kuziangusha chini nguzo za Ashera na kuzijaza zile sehemu kwa mifupa ya watu. 15 Yosia pia akaiteketeza kabisa madhabahu iliyokuwa Betheli na mahali pa juu ambako Yeroboamu mwana wa Nebati (ambaye aliwafanya Waisraeli kuasi) aliijenga. Pia aliichoma moto ile madhabahu na mahali pa juu na kupapiga hadi pakawa vumbi. Pia akaichoma moto nguzo ya Ashera. 16 Yosia alipotazama kwenye lile eneo, akagundua kwamba yale makaburi yalikuwa juu ya mlima. Akawatuma watu kuichukua mifupa kutoka kwenye yale makaburi; kisha akaichoma kwenye madhabahu, akainajisi. Hii ilitokana na neno la BWANA ambalo mtu wa Mungu alilonena, yule mtu alikuwa amenena haya mambo kabla. 17 Kisha akasema, "Ni ukumbusho wa nani ule ninao uona?" Mtu wa ule mji akamwambia, "Lile ni kaburi la mtu wa Mungu ambaye alikuja kutoka Yuda na kutabiri kuhusu haya mambo ambayo umeyafanya dhidi ya madhabahu ya Betheli." 18 Hivyo Yosia akasema, "Mwacheni. Mtu asihamishe mifupa yake." Hivyo wakaacha mifupa yake, pamoja na mifupa ya nabii ambaye alikuja kutoka Samaria. 19 Kisha Yosia akahamisha nyumba zote za mahali pa juu ambazo zilikuwa katika mji wa Samaria, ambazo wafalme wa Israeli walizokuwa wamezitengeneza, na ambazo zilizokuwa zimemgadhabisha BWANA . 20 Aliwafanyia kile ambacho kilikuwa kimefanyika katika Betheli. Aliwachinja makuhani wote wa mahali pa juu ya madhabahu na aliichoma mifupa ya watu juu yao. Kisha akarudi Yerusalemu. 21 Kisha mfalme akawaamuru watu wote, akisema, "Itunzeni Pasaka ya BWANA Mungu wenu, kama ilivyoandikwa kwenye hiki kitabu cha agano." 22 Hiyo Pasaka haijawahi kufanyika tangu siku za waamuzi ambao waliiongoza Israeli, wala katika siku zote za wafalme wa Israeli au Yuda. 23 Lakini katika mwaka wa kumi na nane wa Mfalme Yosia Pasaka ya BWANA ilisheherekewa katika Yerusalemu. 24 Yosia pia akawafukuza wale ambao waliokuwa wameongea na wafu au na roho. Pia aliifukuza miungu ya sanamu, na vitu vyote ambavyo ni chukizo vilivyokuwa vinaonekana katika nchi ya Yuda na katika Yerusalemu, hivyo kwa kuthibitisha yale maneno ya sheria ambayo iliyokuwa imeandikwa kwenye kitabu cha Hilkia yule kuhani aliyekuwa amepatikana kwenye nyumba ya BWANA. 25 Kabla ya Yosia, hapakuwa na mfalme kama yeye, aliyekuwa amemwelekea BWANA kwa moyo wake wote, roho yake yote, na nguvu zake zote, ambaye alifuata sheria zote za Musa. Hapakuwa na mfalme kama Yosia aliyeinuka baada ya yeye. 26 Walakini, BWANA hakugeuka kutoka kwenye ukali wa hasira yake, ambayo ilikuwa dhidi ya Yuda kwa waabudu wapagani wote pamoja ambao Manase aliokuwa amemgadhibisha. 27 Hivyo BWANA akasema, "Pia nitaiondoa Yuda usoni kwangu, kama nilivyoiondoa Israeli, na nitautupilia mbali huu mji ambao nilio uchagua, Yerusalemu, na ile nyumba ambayo niliyokuwa nimesema, 'Jina langu litakuwa humo."' 28 Kama kwa mambo mengine yanayo mhusu Yosia, kila kitu alichofanya, je vimeandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda? 29 Katika siku zake, Farao Neko, mfalme wa Misri, alienda kupigana dhidi ya mfalme wa Ashuru huko mto Frati. Mfalme Yosia akaenda kuonana na Neco katika mapigano, na Neko akamuua huko Megido. 30 Watumishi wa Yosia wakambeba kwenye gari la farasi akiwa amekufa kutoka Migido, kumleta Yerusalemu, na kumzika katika kaburi lake mwenyewe. Kisha watu wa nchi wakamchukua Yehoahazi mwana wa Yosia, wakamtia mafuta, na kumfanya kuwa mfalme katika mahali pake. 31 Yehoahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na tatu alipoanza kutawala, na alitawala miezi mitatu katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa akiitwa Hamutali; alikuwa binti wa Yeremia wa Libana. 32 Yehoahazi alifanya yaliyo maovu usoni kwa Yahwe, kama kila kitu ambacho babu zake walichokifanya. 33 Farao Neko akamfunga gerezani huko Ribla katika nchi ya Hamathi, hivyo asiweze kutawala katika Yerusalemu. Kisha Neko akaitoza Yuda talanta mia moja za fedha na talanta moja ya dhahabu. 34 Farao Neko akamfanya Eliakimu mwana wa Yosia mfalme katika mahali pa Yosia baba yake, na kubadilisha jina lake kuwa Yehoyakimu. Lakini akamchukua mfalme Yehoahazi kwenda Misri, na Yehoahazi akafia huko. 35 Yehoyakimu akalipa fedha na dhahabu kwa Farao. Ili akutane na amri ya Farao, Yehoyakimu akaitoza nchi na kulazimisha kila mtu miongoni mwa watu wa nchi wamlipe fedha na dhahabu kulingana na makadirio yao. 36 Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, na alitawala miaka kumi na moja katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa akiitwa Zebida; alikuwa binti wa Pedaia wa Ruma. 37 Yehoyakimu akafanya yale yaliyo maovu usoni kwa BWANA, kama waliyoyafanya babu zake.