1
Yosia alikuwa na umri wa miaka minane wakati alipoanza kutawala; alitawala kwa mda wa miaka thelathini na moja katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Yedida (Alikuwa binti wa Adaye wa Bozkathi).
2
Alifanya yale yaliyo mema usoni mwa BWANA. Alitembea kwenye njia zote za Daudi baba yake, na hakugeuka wala upande wa kulia au kushoto.
3
Ikawa kwamba katika mwaka wa kumi na nane mfalme Yosia, akamtuma Shafani mwana wa Azalia mwana wa Meshulamu, mwandishi, kwenye nyumba ya BWANA, akisema,
4
"Panda juu kwa Hilkia yule kuhani mkuu na mwambie ahesabu pesa ambazo zilizokuwa zimeletwa kwenye nyumba ya BWANA, ambazo walinzi wa hekalu wamezikusanya kutoka kwa watu.
5
Zigawanywe kwenye mikono ya wafanyakazi ambao ni wasimamizi wa nyumba ya BWANA, na waache wawapatie wafanya kazi ambao wako kwenye nyumba ya BWANA, ili waweze kutengeneza pale palipoharibika.
6
Wapewe pesa maseremala, wajenzi, na waashi, na pia kununua mbao na kukata jiwe kukarabati nyumba ya BWANA."
7
Lakini zile pesa hazikutakiwa kuhesabiwa wakati walipokuwa wanapewa, kwa sababu waliimudu ile kazi kwa uaminifu.
8
Hilkia kuhani mkuu akamwambia Shafani yule mwandishi, "Nimekipata kitabu cha sheria katika nyumba ya BWANA." Basi Hilkia akampatia kile kitabu Shafani, na kukisoma.
9
Shafani akaenda na kuchukua kile kitabu kwa mfalme, na pia kumjulisha, akisema, "Watumishi wako wamezitumia zile pesa ambazo zilizokuwa zimepatikana kwenye hekalu na zimegawiwa kwenye mikono ya wafanya kazi ambao husimamia kuangalia nyumba ya BWANA."
10
Kisha Shafani yule mwandishi akamwambia mfalme, "Hilkia yule kuhani amenipatia kitabu." Kisha Shafani akakisoma mbele ya mfalme.
11
Ikawa kwamba wakati mfalme aliposikia maneno ya sheria, alichana nguo zake.
12
Kisha mfalme akamwamuru Hilkia yule kuhani, Ahikamu mwana wa Shafani, Akbori mwana wa Mikaya, Shafani mwandishi, na Asaya, mtumishi wake mwenyewe, akisema,
13
Nenda na ukaongee pamoja na BWANA kwa ajili yangu, na kwa ajili ya watu na kwa Yuda yote, kwa sababu ya maneno ya hiki kitabu ambacho kilichopatikana. Kwa hasira kubwa ya BWANA ambayo ametukasirikia dhidi yetu kwa sababu baba zetu hawakusikiliza maneno ya hiki kitabu hivyo kama kutii yote ambayo yalikuwa yameandikwa kuhusiana na sisi.
14
Basi Hilkia yule kuhani, Ahikamu, Akbori, Shafani, na Asaya wakaenda kwa Hulda nabii wa kike, mke wa Shalumu mwana wa Tikva mwana wa Harhasi, mtunza kabati la nguo (aliishi katika Yerusalemu katika mtaa wa pili), na wakaongea pamoja naye.
15
Akawaambia, "Hivi ndivyo BWANA, Mungu wa Israeli, asemavyo: 'Mwambie huyu mtu aliyekutuma kwangu,
16
hivi ndivyo BWANA asemavyo: 'Tazama, nitaleta janga kwenye hii sehemu na juu ya wakaao hapa, kulingana na kila kitu kilichoandikwa kwenye kitabu ambacho mfalme wa Yuda alichokisoma.
17
Kwa sababu wamenitelekeza na kufukiza ubani kwa miungu mingine, hivyo basi wanaweza kunichochea hasira pamoja na matendo yote waliyoyafanya, kwa hiyo hasira yangu ilikuwa inawaka dhidi ya hii sehemu, na haitazimika."'
18
Lakini kwa mfalme wa Yuda, aliye watuma kuuliza mapenzi ya BWANA, hivi ndivyo mtakavyo mwambia: "BWANA, Mungu wa Israeli asema hivi: Kuhusu yale maneno uliyoyasikia,
19
kwa sababu moyo wako ulikuwa mlaini, na kwa sababu umejinyenyekesha mwenyewe mbele za BWANA, wakati uliposikia nilichokisema dhidi ya hii sehemu na wenyeji wake, kwamba wanaweza kuwa wakiwa na laana, na kwa sababu ulizozirarua nguo zako na kulia mbele yangu, Nami pia nimekusikia hivi ndivyo BWANA asemavyo.
20
Tazama, nitakukusanya na baba zako, nawe utawekwa kaburini kwako kwa amani. Macho yako hayataona maafa yote ambayo nitayaleta kwenye hii sehemu.'" Hivyo watu wakachukua ujumbe huu kuurudisha kwa mfalme.