1
Katika siku za Yehoyakimu, Nebukadreza mfalme wa Babeli akaiteka Yuda; Yehoyakimu akawa mtumishi kwa muda wa miaka mitatu. Kisha Yehoyakimu akarudi na kuasi dhidi ya Nebukadreza.
2
BWANA akatuma vikosi vya Wakaldayo dhidi ya Yehoyakimu, Washami, Wamoabu, na Waamoni; akawatuma dhidi ya Yuda kuiharibu. Hii ilikuwa ni kuthibitisha pamoja na neno la BWANA ambalo aliloliongea kupitia watumishi wake manabii.
3
Ilikuwa baada ya muda mfupi kwenye kinywa cha BWANA kwamba hili likaja juu ya Yuda, kuwaondoa usoni mwa uso wake, kwa sababu ya dhambi za Manase, yote aliyoyafanya,
4
na pia kwa sababu ya damu isiyokuwa na hatia aliyoimwaga, kwa kuijaza Yerusalemu kwa damu isiyokuwa na hatia. BWANA hakuwa tayari kusamehe hilo.
5
Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Yehoyakimu, na yote aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
6
Yehoyakimu akalala pamoja na wazee wake, na Yekonia mtoto wake akawa mfalme katika sehemu yake.
7
Mfalme wa Misri hakushambulia tena nje ya nchi yake, kwa sababu mfalme wa Babeli alikuwa amezishinda nchi zote ambazo zilikuwa zikitawaliwa na mfalme wa Misri, kutoka kwenye kijito cha Misri mpaka Mto wa Frati.
8
Yekonia alikuwa na umri wa miaka kumi na nane alipoanza kutawala; alitawala Yerusalemu miezi mitatu. Mama yake alikuwa anaitwa Nehushta; alikuwa binti wa Elnathani wa Yerusalemu.
9
Alifanya yaliyo maovu usoni mwa BWANA; alifanya yale yote ambayo baba yake aliyafanya.
10
Katika kipindi hicho jeshi la Nebukadreza mfalme wa Babeli liliishambulia Yerusalemu na kuuzunguka mji.
11
Nebukadreza mfalme wa Babeli akaja kwenye mji wakati maaskari wake walipokuwa wameuzunguka,
12
na Yekonia mfalme wa Yuda akatoka nje kwenda kwa mfalme wa Babeli, yeye, mama yake, watumishi wake, watoto wake, na maafisa wake. Mfalme wa Babeli akamteka katika mwaka wa nane wa utawala wake.
13
Nebukadreza akachukua kutoka pale vitu vyote vya thamani katika nyumba ya BWANA, na walio katika nyumba ya kifalme. Akavikata vipande vipande vitu vyote vya dhahabu ambavyo Sulemani mfalme wa Israeli alivitengeneza katika hekalu la BWANA, kama alivyokuwa amesema ingetokea.
14
Akawachukua wote utumwani Yerusalemu, viongozi wote, na wapiganaji wote, mateka elfu kumi, na mafundi wote, na wafua vyuma. hakuna aliyekuwa amesalia isipokuwa watu masikini katika nchi.
15
Nebukadreza akamchukua Yekonia utumwani Babeli, pia na mama yake na mfalme, wake, maafisa, na wakuu wa nchi. Akawachukua kwenda utumwani kutoka Yerusalemu mpaka Babeli.
16
Wapiganaji wote,7,000 kwa hesabu, na mafundi 1,000 na wafua vyuma, wote wanaostahili kumpiga mfalme wa Babeli aliwaleta hawa watu kwenye utumwa Babeli.
17
Mfalme wa Babeli akamfanya Matania, kaka yake na baba yake na Yehokimu, mfalme katika sehemu yake, na kubadilisha jina lake kuwa Sedekia.
18
Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na moja wakati alipoanza kutawala; alitawala miaka kumi na moja katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Hamutali; alikuwa binti wa Yeremia kutoka Libna.
19
Alifanya yaliyo maovu machoni mwa BWANA; aliyafanya yale yote ambayo Yehokimu aliyoyafanya.
20
Kupitia hasira ya BWANA, haya matukio yote yalitokea Yerusalemu na Yuda, hadi alipowaondoa kwenye uso wake. Kisha Sedekia akaasi dhidi ya mfalme wa Babeli.