Sura 3

1 Kwacho, ndugu vatakatifu, vashiriki va udhahao wa mbinguni, mumfikiri yesu, mdume na kuhani mduve wa ukiri wedu. 2 Eveekeri mwaminifu kwa Ruva adhemdua, sha Musa eekeri mwaminifu pia katika mba yoose ya Ruva. 3 Kwa kfa yesu aletadhua ina na heshima nduve kuliko yoeveekeri nayo Musa, kwa sababu ula mba etadhua iva na heshima nduve kuliko mbayo iiveni. 4 Kwa kfa kidha mba yejengwa na mndu fudhani, dhakini ula ejenga kidha kndo ni Ruva. 5 Hakika Musa eveekeri mwaminifu sha mtumishi katika mba yoose ya Ruva, akafuna ushuhuda ihusu mambo yoyeambwa wakati uusha. 6 Dhakini kristu ni mwana katika usimamisi wa mba ya Ruva. Sohoso ni mba yakwe sha duuriilia haraka katika ijiamini na fahari yajiamini. 7 Kwa hiyo, ni sha mo mtakatifu shaaliweamba, ''Dhuni, kolia weishwa sauti yaakwe. 8 Utafanye mo waafo iva mhumu sha Waisraeli vaafanye katika uasi, wakati wejaribiwa nyikani. 9 Shu uveekeri wakati ambao papa venu valeng'asi kwa ing'jaribu, na wakati, kwa miaka arobaini, veledholia matendo yaakwa. 10 Kwa hiyo ngilefurahishwaku na ksasicho. Ngileamba, ''veecheka kidha mara katika mo saavo, na veishi shia sakwaku. 11 Ni sha vidhe ngitheapa katika hasira yakwa: veiingia raha yaakwaku.'' 12 Mve vaangalifu, ndugu, ili kwamba mtasheevafo mo mwofu uteamini kwa umu wenu, mo ambao weenda kwasha na Ruva ekeri hai. 13 Badadha yakwe, muhamasishane kidha siku kidha umu na mwensie, ili kidha iidhahawafo dhuni mutamani, ili kwamba umu kati yenu atafanye iva mhumu kwa idhembwa na sambi. 14 Kwa kfa deleva vashiriki va kristu ikava dweshikamana na usabiti weedu kwa ngufu katika ve ifuma mwanso hadi mwisho. 15 Ihusu ili lidhena eiambwa. ''Dhuni kolia mweihuchania sauti yaakwe,mtafanye mo seenu iva nhumu, sha Waisraeli shaali velefanya wakati wa uasi.'' 16 Ni vovakivo valemwishwa Ruva na ihasi? Veveekeri vala voosaku ambavo Musa eveekeri alevaongosa iuka Misri? 17 Na vovaki vo Ruva alevasua kwa miaka arobaini? Niivo pamoja na vala waletenda sambiku, ambavo miili yavo iledhaa jangwani? 18 Ni vovaki Ruva alevaapia kwamba veingia katika raha yaakwe, kama sio vale ambao vetelemtii ve? 19 Duoni kwamba veledimai iingia katika raha yaakwe kwa sababu yaicheamini.