Sura 2

1 Mwe mwezi wa Nisani, mwe mwaka wa ishiini wa mfaume Aitashasta, nee kasagua divai, na nikaidoa na kumwenka mfaume Sasa nchekuwahi kusikitika mbele ye mfaume. 2 Akini mfaume akanamba, "Kwambwai cheni chako kina usoyoyo? nkuonekana kuwa mtumwa, Inu ni lazima iwe usoyoyo wa moyo," Ikabinda nikaogoha sana. 3 Nikamwamba mfaume. "Mfaume ekae kae na kae! Kwa mbwai cheni changu chesekuwa na usoyoyo? ikiwa mzi, hantu he makabui yatate,, uko mwe mahagae na malango yakwe yabanangwa ni moto." 4 "Nee mfaume anamba, "Waondeza mbwai nigosoe? "Kwa iyo nikamuombeza Zumbe Muungu ywa mbinguni. 5 Nikamwamba mfaume, "Mfaume ukaona vyaagiza, na kana mndima ywako kagosoa vitana h meso yako, wadaha kuhituma Yuda mzi a kabui za tate, ili nipate kuuzenga vituhu. 6 "Mfaume akanitambaisa (na malikia pia nae ekao hehi nae) "wenda wekae kwa mda wani mpaka uuye? Mfaume akaona ni vitana kunengaa nami nikamwenka mda. 7 Nee na mwambia mfaume, "Kana vyendavikutamie mfaume, nenka baua kwa ajii ya wakuu seja ya mto, ili wapate kuniluhusu nemboke mwe maeneo yao siai kuita Yuda. 8 Pia kuwe na baua kwa Asafu, mlinzi ywa mzitu wa mfaume ili anenke miti ya kugosoa mihili ya miango ya ngome hehi na hekalu, na kwa ukanto wa mzi na kwa numba ndima neke, "Kwa iyo kwakuwa mkono mtana wa mfaume nee ujuu yangu, mfaume nee anenka hitaji dangu. 9 Nkibua kwa wakuu seja ya mto na kuwenka baua za mfaume. Basi mfaume nee kegaa maofisa wa jeshi na wakwea faasi hamwe na mimu. 10 Sanbalati Mhoroni na Tobbia mndima ywa amoni wekusikiaho mbui inu, watamiwa sana kwa kuwa muntu nee keza ambae nee akageeza kuwambiza wantu wa Islael. 11 Basi nikauya Yelusalemu na nee niuko siku ntatu. 12 Nee nchenuka nakio mimi na wantu eacheche. Nchee' kumwambia muntu yoyose kia Muungu ywangu ekuikacho mwe moyo wangu kugosoa Yelusalem. Nkakwekuwa na mnyama hamwe na mimi, iya yuda nekuwae nkimkwea. 13 Nkihauka nakio kwa sia ya lango da kwe koongo kuelekea kisima cha joka na kwenako uvi wa kifusi, na kuagua kanto za Yelusalemu ambazo zihazamulwa, na nyuvi za mbao zibanangwa ni moto. 14 Ikabinda nikaita kwelango na ngodi ya mfaume. Nafasi nee ni sisi sana kwa mnyama kwa mnyama nekukweae kwemboka. 15 Kwaa iyo nikaita ichoicho nkandai ya koongo na kuchunguza ukanta, nikauya nyuma na kwengia kwa lango da kwe koongo na ivya nikauya. 16 Watawala nkawekumanya nekuitaho au kia nekugosoacho na nche kuwambia Wayahudi waa makuhani waa wakuu waa watawala waa wantuhu wekugosoao ndima iyo. 17 Nikawamba," waona sungu tenayo, namna Yelusalem mwe mahagae na nyuvi zokwe zibanangwa ni moto. Soni tezenge uhya ukanto wa Yelusalam ili tesekuwa nu soni vituhu. 18 Nee nkiwamba mkono mtana wa Muungu ywangu nee ujuu yangu na pia kuhusu mbui mbui ya mfaume ambayo nee kanambia. Wakamba, " Hebu tihauke na kuzenga, "Kwa iyo wakaimarisha mikono yao kwaajii ndima ntana. 19 Akini sanbalati Mhoroni na Tobia mndima ywakwe Mwamani, na Geshemu, Mwarabu wekusikiaho mbui iyo wakatiseka na kutikana wakamba, "Wagosoani? Je wagombana na mfaume? 20 Nee nawatambaisa,, "Muungu ywa mbinguni enda atenke mafanikio, swiswi ti wandima wakwe na tenda tihauke na kuzenga. Akini nkuna sehemu nkaku na dai da kihisitolia uko Yelusalemu.