1 Akaawaaho Eliashibu, kuhani mkuu, akagooka hamwe na nduguze makuhani, wakazenga lango da ngoto. Wanding'aza na kuika nyuvi zakwe. Waika wakfu mpaka mnaa wa Hamea na mpaka mnaa wa Hananeli. 2 Wakaawaaho wantuwa Yeliko wakazenga, na kuawaaho Zakuli mwanawe da Imli akazenga. 3 Wana wa Senaa wakasenza lango da samaki.Waika mihimii yakwe na kuika nyuvi zakwe na vyuma vyakwe na mihindo yakwe. 4 Melemosi kaandaa ntendeo itongeayo. Yeye ni mwana ulia mwana Hakosi. Na akaawaho Meshulamu akagosoa. Ye ni mwana Belekia mwana Mashezabeli. Hehi nao Sadoki akagosoa.Ye ni mwana Baama. 5 Wakaawaaho Watekoi wakagosoa, mia viongozi wao waemea kugosoa ndima yekuagiiwayo ni wakuu wao. 6 Yoyada mwana Pasea, na Meshulamu mwana Besodeya, wahosoa lango da kae. Waika mihimi,na kuika nyuvi zakwe na vyuma vyakwe na mihindo yakwe. 7 Nao, Melatia Mgibeoni, na Yadoni Melonosi, wantu wa Gibeoni na Misipa, wagosoea ugosozi uanga ya hantu ambaho mkuu ya mkoa ng'ambu ya mto kekaa. 8 Na akaawaaho Uzieli mwana Halilaya, yumwe mwe wasana zahabu, akagosoa; akaawaaho hanania, mgosozi ya manukato. Wakazenga vituhu Yelusalemu mpaka ukanto mzangaamu. 9 Na akaawaaho Lefanya mwana Huli akazenga. Nee ni mtawala ya nusu ya wilaya ya Yelusalemu. 10 Na akaawaaho Yedaya mwana Halumafu akazenga hehi na nyumba yakwe . Na kuawaaho Hatushi mwana Hashabineya akazenga. 11 Malik mwana Halimu na Hashubu mwana Pahati Moabu, wazenga hantu hantu hamwe ne mnaa wa tanuu. 12 Akaawaho Shalumu mwana Haloheshi, mkuu ya nusu ya wilaya Yelusalemu, akazenga, hamwe na wanawe wakivyee. 13 Hanuni na wenyezi wa Zanoa wa zenga lango da koongoi. Wazenga vituhu na kuika nyuvi zakwe na vyuma vyakwe na kihindo yakwe. Wazenga zilaa elufu mpaka lango da kifusi. 14 Malikiya mwana Lekabu mkuu ya wilaya ya Bes-Hakelemu, akazenga lango da kifusi. Akazenga na kuika nyuvi zakwe, na vyuma vyakwe na mihindo yakwe. 15 Shalumu mwana Kalihoze, mkuu ya wilaya ya Misipa, akazenga lango da ngodi. Kazenga, na kuika ngubiko wanga yakwe na kuika nyuvi zakwe na vyuma vyakwe na mihindo yakwe. Kazenga uhya ukanto wa npwani wa Siloamu kwa bustani ya mfaume, mpaka vidanto vya kuongoza kwe mzi wa Daudi. 16 Nehemia mwana azibuki, mtawala ya nusu ya wilaya ya Bee-Suli akazenga hantu aho, kuawa makabui ya Daudi, mpaka biika dekuzengwado ni wantu na nyumba ya wantu wenye nguvu. 17 Wakaawaaho Walawi wazenga, hamwe na Lehumi mwana Bani na ikaawaaho, Hashabia, mtawala ya nusu ya wilaya ya Keila, kwa wilaya yakwe. 18 Wakaawaaho wantu wasii zao wazenga, ikawa ni hamwi na Binui mwana Henadadi, mkuu ya nusu ya wilaya ya Keila. 19 Akaawaaho akazenga Ezeli, mwana Yohua, mtawala ya Misipa, kazenga hantu hantu kuelekea gala da silaha kwe kona ya ukando. 20 Akaawaaho Baluki, mwana Zakai akazenga kwa hiali hantu hantuhu, kuawa kona ya ukanto mpaka uvi wa nyumba ya Eliashibu, kuhani mkuu. 21 Akaawaaho Melemosi mwana Ulia, mwana Hakosi, akazenga hantu hantuhu, kuawa uvi wa nyumba ya Eliashibu mpaka kiheo cha nyumba ya Eliashibu. 22 Waakawaaho makuhani, wantu wa ntendeo izo hehi na Yelusalemu, wakazenga. Akaawaaho Benyamini na Hashubu wakazenga kuelekes nyumba yao. 23 Akaawaaho Benyamini na Hashulubu wakazenga kuelekea nyumba yao. akawaaho Azalia mwana Maaseya mwana Anania, kazenga hehi na nyumba yakwe. 24 Akaawaaho Binui mwana Henadadi akazenga hantu hatuhu, kuawa nyumba ya Azalia hadi kona ya ukanto. 25 26 Palali mwana Uzai akazenga uanga ya kona ya ukanto na mnaa utangaao uanga kuawa nyumba ya uanga ya mfaume mwe uwanda wa walinzi. Akaawaaho Pedaya mwana Paloshi akazenga. Sasa wandima ntendeo za Hifazi ya Mazi ntendeo za mashaiki ya mnaa weaviizao. 27 Wakaawaaho Watekai wazenga hantu hatuhu, kuelekea mnaa mkuu wa chongoi, mpaka ukanto wa Ofeli. 28 Makuhani wakazenga uanga ya lango da falasi, kia yumwe kuelekea nyumba yakwe. 30 Akaawaaho Sadoki, mwana Imeli, kazenga ntendeo iyo kuelekea nyumba yakwe. Naakaawaho Shemaya mwana Shekania, mlinzi ya lango da Mashaiki akazenga. 29 Akaawaaho Hanania, mwana Selemia na Hanuni mwana ya mtandatu ya Salafu, wakazenga hantu hantuhu. Meshulamu mwana Belekia akazenga kuelekea kwe vyumba vyakwe. 31 Akaawaaho Malikiya, yumwe ya wasana zahabu, akazenga mpaka nyumba ya wandima wa hekalu na wagosoa biashaa wekuao wakaelekea lango da geeza na mpaka chumba cha uanga cha nkandai. 32 Wagosoa biashaa ya zahabu na wagosoa biashaa wazenga gatigati ya chumba cha uanga cha kona na lango da ngoto.