1 Nadabu na Abihu, wana wa Aroni, wakadoa kia muntu kivunkizo chakwe, akaika moto umo, na akagea uvumba. Wekubindaho wakaavya moto uemewai mbele ya Yahweh, moto wekuao nkeekuwaagiia wowo kuuavya. 2 Kwa iyo moto ukaseea sii mbele ya Yahweh na kuwada, nao wakaumbwa mzimu mbele ya Yahweh. 3 Akaawaaho Musa akamwamba Aroni, Ivi nee Yahweh ekuavyo akatamwiia ekugombekaho, 'Nondaniugubue utakatifu kwa wada wezao mbele yangu. Nami n'ndanigimbikwe mbele ya wantu wose." Naye Aroni nkeekugombeka mbui yoyose. 4 Musa akamwetanga Mishaeli na Elzafani, wana wa Uzieli mtumbawe da Aroni, nae akamwamba, "Soo uku na uwaavye nduguzo chongoi ya nkambi waawe mbele ya hema." 5 Ivyo wakezahehi na kuwadoa wakewehamba nkazu zao za kukuhani, nao wakawegaa chongoi ya nkambi, kana Musa ekuavyo kaangiizwa. Kuawaaho Musa akamwamba Aroni na wanawe watuhu aidi, Eliezari na Ithamari," 6 Mwesekubada chazae fii za mitwi yenu, waa mwesekuhaabua nguo zenu, ili kwamba mwesekweza mkaumbwa mzimu, na kua Yahweh esekukimwa ni bunga gima. Akini waekeni jamaa zenu, nyumba yose ya Israeli wadahe kugosoa mviko wa kweyayata kwa ajii ya ao ambao Yahweh kawadagamiza kwa moto. 7 Mwesekuita chongoi kuawa kwe engiio da hema da kukintania, ama nkivyo n'nda muumbe mzimu, kwa kua mavuta ya Yahweh ya kwesisa ya uanga yenu." Kwa iyo wakagosoa sawasawa na maangiizo ya Musa. 8 Mungu akatamwiia na Aroni, akagombeka, 9 "Mwesekunywa mvinyo waa kinywaji kikai, wee au wanao wasigaao hamwe na wewe, ili kwamba ndihomwengie kwe hema da kukintania mwesekweza kuumbwa mzimu. Inu yondaiwe amli ya kwekaisa mwe vivyazi vyose vya wantu wenu. 10 Ili kutofautisha kati ya mbui takatifu na mbui za kawaida, na kati ya najisi na safi, 11 ili kwamba mweze muwahinye wantu wa Israeli amli zose ambazo Yahweh kaziagiia kwa kanwa cha Musa. 12 Musa akatamwiia na Aroni na wanawe waidi wekusigaao; Eliazari na Ithamari, Avyani kafaa ya nafaka isigaayo kuawana na kafaa igosolwayo kwa Yahweh kwa moto nanywi ideni nkandai hemviko kisi hamila, kwa kua ni takatifu sana. 13 Lazima n'ndamuide hantu hatakatifu kwa sibabu uo ni mpangano wako wewe na mpangano wa wanao wa matoleo yekugosolwayo kwa Yahweh kwa moto, kwa kua ivi nee nekuamliwavyo nimyambie. 14 Kia kidali kisingiswacho na ida nyonga ambayo yaavigwa kwa Yahweh, yondigwa muide hantu hasafi hakubalikaho kwa Mungu. We mwenye wanao na wanao wa vivyee we hamwe na wewe mwondamde ntendeo izo, kwa kua ziavigwa kua mpangano wako na mpangano wa wanao kuawana na zabihu ya kafaa ya ushiika wa wantu wa Israeli. 15 Ida nyonga yekuavigwayo na kidali chekusingiswacho, ni lazima zietwe hamwe na kafaa ya mavuta yekugosolwayo kwa moto, ili kukuchwa mbele ya Yahweh. Nazo zondaziwe zako wewe na wanaonkuwa mpangano wenu daima, kana Yahweh ekuamuuvyo. 16 Akaawaaho Musa akauza kuhusu yuda mbuzi ya kafaa ya zambi, nae akamanya kua nee kadagamizwa kwa moto. Kwa iyo akakimwa ni Eliazari na Ithamari, wana wa Aroni wekusigaao; akawamba, 17 "Kwa mbwai nkamzati kuida kafaa ya zambi he ntendeo ya hema, kwa ajii ni takatify sana, na kua Yahweh kaiavyakae kwenu ili kudoa ubanasi wa utifii, ili kugosoa wevano kwa ajii yao mbele zakwe? 18 Kaua, mphome yakwe nkayokuetwa mwe hema, kwa iyo yondigwa kwa hakika kua kaida kae kwe ntendeo za hema, kana nekuagiiavyo? 19 Akaawaaho Aroni akamwandua Musa, "Kaua, ivyeo waavy kafaa yao ya zambi na kafaa ya kudagamiza mbele ya Yahweh, na mbui inu viavia igosoka kwangu ivyeo. Ati nkidakae kafaa ya zambi ivyeo, Je! Nkayokua iagizakae mbele ya Yahweh?" 20 Nae Musa ekusikiaho ivyo, akalizika.