1 Israeli akaita na vyose ekuwavyo navyo akeza Beersheba. Hada akalavya sadaka kwa Mungu ywa Isaka tatiakwe. 2 Mungu akamwamba Israeli mwe sozi nakio, akaamba, "Yakobo, Yakobo." 3 Akazumia, "Mi mwehanu." Akagombeka, "Mi ni Mungu, Mungu wa tatizako. Wesekuogoha kuseea Misri, ka kua ndanikugosoe taifa kuu uko. 4 Toondatite hamwe nawe uko Misri, nami nndanikukueze uku vituhu bila wengee. Yusufu nae akayagupika meso yako kwa vifumba vyakwe." 5 Yakobo akenuka kuawa Beersheba. Wana wa Israeli wakamwegaa Yakobo tatiyao, wana wao na avyee wao, kwe mikokoteni yekwegalwayo ni Farao kuwadoa. 6 Wakadoa mifugo yao na mai zao wekuwazowapata kwe si ya Kanaani. Wakeza Misri, Yakobo na uvyazi wakwe wose hamwe. 7 Akeza Misri hamwe na wanawe na wezukuuwe, wana vivyee na uvyazi wao wose. 8 Aya nee mazina ya wanangwa wa Israeli wekwezao Misri, Yakobo na wanawe: Rubeni, mvyaigwa ya bosi ya Yakobo; 9 wanangwa wa Rubeni Hanoki na Palu na Hezroni na Karmi; 10 wana wa Simoni, Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Zohari, na Shauli, wana wa mwanamke Mkanaani; 11 wana wa Lawi Gershoni, Kohathi, na Merari. 12 Wana wa Yuda: Eri, Shela, Peresi, na Zera, (Lakini Eri na Onani walikufa katika nchi ya Kanaani). Na wana wa Peresi walikuwa Hezroni na Hamuli. 13 Wana wa Isakari nee ni Tola, Puva, Lobu, na Shimroni; 14 Wana wa Zabuloni walikuwa Seredi, Eloni, na Yahleeli 15 Awa ne wanangwa wa Lea ekumvyaiao Yakobo uko Padani Aramu, hamwe na Dina mwanawe ya kivyee. Wanawe na wana kivyee nee wabua saasini na ntatu. 16 Wana wa Gadi walikuwa Zifioni, Hagi, Shuni, Ezboni, Eri, Arodi, na Areli. 17 Wana wa Asheri nee ni Imna, Ishva, Ishvi, na Beria; na Sera alikuwa dada yao. Wana wa Beria walikuwa Heberi na Malkieli. 18 Awa wawa wanangwa wa Zilpa, mwekua Labani kamwenka Lea mwanawe ya kivyee. Wana ekumvyaiao Yakobo wose nee ni kumi na mtandatu. 19 Wana wa Raheli mkaziwe da Yakobo wawa Yusufu na Benjamini. 20 Uko Misri Manase na Efraimu wakavyaigwa mwe Yusufu na Asenathi, binti Potifera kuhani wa Oni. 21 Wana wa Benjamini walikuwa Bela, Bekeri, Ashbeli, Gera, Naamani, Ehi, Roshi, Mupimu, Hupimu, na Ardi. 22 Awa wawa wanangwa wa Raheli waliozaliwa kwa Yakobo - jumla yao kumi na wanne. 23 Mwana wa Dani alikuwa Hushimu. 24 Wana wa Naftali walikuwa Yahzeeli, Guni, Yezeri, na Shilemi. 25 Awa nee ni wana wa Bilha wekumvyaiaoYakobo, ambaye Labani kamwenk Raheli mwanawe ya kivyee - wose wamo mpungati. 26 Wose wakaita na Yakobo, wekuwao uvyazi wakwe, bila kutaazia wakaza wanawe da Yakobo ne wamo sitini na sita. 27 Hamwe na wana waidi wa Yusufu wekuvyaigwao kwakwe uko Misri, wantu wa familia yakwe wekuitao Misri nee wamo sabini hamwe wose. 28 Yakobo akamwagiia Yuda kuwaongoea mbele ya Yusufu kuonyesa sia kuita Gosheni, nao wakeza kwe eneo da Gosheni. 29 Yusufu akazenga kumbi dakwe akaita kumgokea tatiakwe uko Gosheni. Akambwiia akamuumbatia singo yakwe, akaia mwe singo yakwe kwa mda. 30 Israeli akamwamba Yusufu, "Ivyo na niumbwe mzimu iviaha kwa kua nkikiona cheni chako kua ukeemgima." 31 Yusufu akawamba nduguze na nyumba ya tatiakwe, "Nondaniite nikamhinye Farao, kua, ''Ndugu zangu na nyumba ya tate mimi wekuwao kwe si ya Kanaani wanezea. 32 Wantu awa ni waisi, kwa ajii wawa waisi weza na mabunga yao ya ngoto, na mbuzi, na vyose wenavyo. 33 Yendaiwe, Farao endahoawetange na kuwauza, 'Ndima yenu ni ihi? 34 Umwambe, wandima wako nee ni waisi wa wanyama yangia mwande kubua ivi, swiswi, na tatizetu.' Gosoani ivyo ili mdahekwekaa mwe sii ya Gosheni, kwa kua kia muisi ana mbifya na Wamisri."