Sura ya 47

1 Ikabinda Yusufu akengia kwa Farao na kumwamba, "Tate na ndugu zangu, ng'oto wao na mbuzi zao, na yose wenayo, wabua kulawa mwe si ya Kanaani. Kauwa, waaho mwe si ya Gosheni." 2 Akawadoa washano mwe nduguze na kuwatambulisha kwa Farao. 3 Farao akawamba nduguze, "Ndima yenu ni mbwai?" Wakamwamba Farao, "Wandima wako ti wafugaji, enga mababa zetu." 4 Ikabinda wakamwamba Farao, "Teza kwekaa kwa muda mwe si. Malisho nkhakuna kwa jii ya makundi ya wandima wako, kwa ajii ya saa ni nkai sana mwesi ya Kanaani, kwa iyo, tafazai waeke wandima wako wekae mwe si ya Gosheni." 5 Ikabinda Farao akamwamba Yusufu, akamba, "Tati yako na nduguzo weza kwako. 6 Sii ya Misri imbele yako. Umwekaze tati yako na nduguzo ntendeo ntana, si ya Gosheni. Ikiwa wamanya wantu wenao udahi miongoni mwao, uwaike kuwatunduia wanyama wangu." 7 Ikabinda Yusufu akamwengiza Yakobo tati yakwe na kumuika mbele ya Farao. Yakobo akambaliki Farao. 8 Farao akamwamba Yakobo, "Kuishi kwa muda wani?" 9 Yakobo akamwamba Farao, "Myaka ya ntambo zangu ni mia mwenga na saasini. Myaka ya maisha yangu iwa mijihi na ya maumivu. Nkiyo kama myaka ya tati zangu." 10 Ikabinda Yakobo akambaiki Farao na kuhauka mbele yakwe. 11 Ikabinda Yusufu akamuika tati yakwe na nduguze. Akawenkha ntendeo mwe si ya Misri, mphaamo yedi sana ya si, mwe ntendeo ya Ramesesi, enga Farao emwagiizavyo. 12 Yusufu amhudumia tati yakwe kwa nkhande, nduguze, na nyumba yose ya tati yakwe, kuigana na hisabu ya wahitaji wao. 13 Basi nkakwekua na nkhande mwe si yose, kwani saa iwa nkhai muno, si ya Misri na si ya Kanaani ikabanika kwa sibabu ya saa. 14 Yusufu akakusanya hea yose yekuwayo mwe si ya Misri na si ya Kanaani, kwa kuwatagia wekazi wakwe nkhande ikabinda Yusufu akaeta he zia mwe nyumba ya Farao. 15 Hea yose ya si ya Misri na Kanaani ikusiaho, Wamisri wose wakeza kwa Yusufu wakagombeka, "Utenke nkande! Kwaji yani tife mbele yako kwa mana hea yetu isiya?" 16 Yusufu akagombeka, "Atiho hea yenu isiya, eteni wanyama wenu nami nendaniwenke nkhande badii ya wao." 17 Kwa iyo wakaeta wanyama wao kwa Yusufu, Yusufu akawenka nkande kwa kubadiishana na faasi, ng'oto, mbuzi na nphunda. Akawaisa kwa mikate kwa kubaduushana na wanyama wao mwaka uda. 18 Mwaka uda ukusiaho, wakeza kwakwe mwaka ukutongeaa na kumwamba nkatinatifise zumbe yangu kwamba hea yetu yose isia, na wanyama ni wa zumbe wangu. Nkakuna kikusigaacho mbele ya zumbe wangu, ikesekuwa ni miietu na si yetu. 19 Kwani tife mbele ya meso yakwe, swie na si yetu? Utigue swiswi na si yetu badala ya nkhande, na swiswi na si yetu tendatiwe wandima wa Farao. Utenke mbeyu ili kuwa tiishi tiswkufa, na si siekuwa bueu bila wantu. 20 Ivyo Yusufu akamgwiia Farao si yose y Misri. Kwa ajii kia Mmisri akautaga munda wakwe, kwa sibabu saa iwa mkai muno. Kwa sia inu, si ikawa mai ya Farao. 21 Na wantu, awagosoa kuwa watumwa kulawa mhaka umwe wa Misri hadi mhaka mtuhu. 22 Ni si ya makuhani ikedu iwa nkaikugulwa ni Yusufu kwa sibabu makuhani ne wekenkwa posho wadiya, mwe sehemu wekwenkwaye ni Farao, kwa iyo nkawe kitaga si yao. 23 Ikabinda Yusufu akawamba wantu, "Kauwa, nkiwagua nywinywi na si yenu ivyeo kwajii ya Farao. Basi mbeyu inu hanu kwa ajii yenu, nanyi mkahanda mwe si. 24 Ukati wa kuozoa, mmwenke Farao sehemu ya shano na sehemu nne zendaziwe ni zenu, kwa mbeyu za munda na kwa nkande ya nyumba zenu na wana wenu.'' 25 Wakagombeka, "Kuhonya maisha yetu. Na tipate kibali he meso yake. Tenda tiwe wandima wa Farao." 26 Ivyo Yusufu akaigosoa kuwa shaia igosoayo ndima hata ivyeo mwe si ya Misri, kuwa mwenga ya shano ni ya Farao. Eneo da makuhani ikedu nkande kugosolwa kuwa da Farao. 27 Ivyo Israeli akaishi mwe si ya Misri, mwe ntendeo ya Gosheni. Wantu wakwe wakapata umiliki, wakawa wenao uvyazi na kugenyea sana. 28 Yakobo akekaa mwe si ya Misri myaka kumi na saba, kwa iyo myaka ya maisha ya Yakobo iwa myaka mia mwenga alubaini na saba. 29 Ukati wa kufa kwake Yakobo ukabuaho hehi, akamwetanga Yusufu mwanawe na kumwamba, ''Kama nkipata kibali mbele yako, ika mkono wako si ya paja dangu, na unigoswee kwa uaminifu na kwei. Tafazai usekunizika Misri. 30 Nendaho nigone na watate wangu, wenda uniavye Misri na kunizika mwe eneo da kigii cha watate wangu." Yusufu akamba, "Nendanigosoe enga ukugembekavyo." 31 Israeli akagombeka, "Niapia," na Yusufu akamwapia. Ikabinda Israeli akenamasi mbele ya usazi wakwe.