1 Nee aho Yusufu nkekudaha kwezuiya mwenye mbee ya watandima wagookao nkandani yakwe. Akagombeka kwa ukemo, "Kiya mntu ahauke." Ivyo nkakuna mtandima mwekugoka nkandani yakwe ukati Yusufu ekwetambulishaho kwa waumbuze. 2 Akaiya kwa nkoo, Wamisri wakasikia, na nyumba ya Farao wakasikia kuhusu ido. 3 Yusufu akamwaambia waumbuze, "Mie ni Yusufu. Je tate bado ni mgima? Waumbuze nkaokudaha kujibu, kwani watiswa na kuwaaho kwakwe. 4 Naho Yusufu akawaamba waumbuze, "Sooni, tafazai." Nao wamsogeeya. Akagombeka, "Mie ni Yusufu ndugu yenu, mwekumtagae Misri. 5 Akini sasa mwesekuhuzunika au kununa miongoni mwenu kwamba mnitaga uku, inga Mungu kanituma mbee yenu ili kutuza ugima. 6 Maana ni miaka miidi saa imwe sii, na bado kuna miaka mishano ambayo nkakuna kuima wala kubonda. 7 Mungu kanituma mbee yenu kuwahifazi kana sigavu duniani, na kuwaika wagima kwa kuoholwa kukuu. 8 Ivyo nkio nywinywi mwekunegao uku iya ni Mungu, na kanigosoa tate kwa Farao, bwana wa nyumba yakwe yose, na mtawaa wa sii yose ya Misri. 9 Gosoani bidii mwiite kwa tate na mmwambie, 'Ivi ne agombekavyo Yusufu mwanao, "Mugnu kanigosoa bwana mwe Wamisri wose. Seeya kwangu, usekukawia. 10 Wonda wekae mwe sii ya Gosheni, nawe wonda uwe hehi nami, wee na wanao na wana wa wanao, na ngoto wako na mbuzi wako, na vyose wenavyo. 11 Nami nonda nikuhudumie hada, kwa ajii bado kuna miyaka mishano ya saa, ivyo usekweza ukengia mwe uwondezaji, wewe, nyumba yako na vyose wenavyo." 12 Kauwa, meso yenu yakauwa, na meso ya Benjamini nduguyo, kwamba ni kanwa changu kitamwiyacho nanyi. 13 Mwondamwambie tati yetu uwanga ya hishima yangu yose uku Misri na yose myaonayo. Mwonda mgosoe halaka na kumueta tate uku." 14 Akakumbatia singo ya Benjamini ndugu ye na kuiya, na Benjamini akaiya mwe singo yakwe. 15 Akawabusu nduguze wose na kiya kwa ajii yao. Baada ya ayo nduguze wakatamwiya naye. 16 Habai ya mbui inu ikatamwiwa mwe nyumba ya Farao: "Wanduguze Yusufu weza." Ikampendeza sana Farao na watandima wakwe. 17 Farao akamwambia Yusufu, "Waambie nduguzo, 'Gosoani ivi: wapakieni wanyama wenu na mwiite mwe sii ya Kanaani. 18 Mdoeni tati yenu na nyumba zenu mnezee, Nami nonda niwenke matana ya sii ya Misri, nanyi mwonda mda unono wa sii.' 19 Iya mwambigwa gosoani ivi,, doani matololi kuawa Misri kwa ajii ya wana wenu na kwa ajii ya wavyee wenu. Mdoeni tati yenu na kweza nae. 20 Mwese kujai maii zenu, kwani matana yose ya sii ya Misri ni yenu." 21 Wana wa Israeli waagosoa ivyo. Yusufu akawenka mikokoteni, kwa kadii ya maagiiyo ya Farao, na akawenka mahitaji ya ntambo. 22 Akawenka wose nguo za kubadiisha, akini akamwenka benjamini vipande mia ntatu vya feza na nguo shano za kubadii. 23 Akamwegaiya tati yakwe: npunda kumi wekwenuao matana ya Misri, npunda wavyee kumi wekwenuao nafaka, mikate na mahitaji matuhu kwa tati yakwe kwa ajii ya ntambo. 24 Ivyo akawaluhusu nduguze nao wakahauka. Akawamba, "Kauwani msekwezamkagombana siyani." 25 Wakakweya kuawa Misri na kweza mwe sii ya Kanaani, kwa Yakobo tati yao. 26 Wakamwambia "Yusufu yuke meso, na nee mtawaa uwanga ya sii yose ya Misri." Na moyo wakwe utozwa ni kudunduwaa, inga nkekutiamini. 27 Wakamwambia mbui zose za Yusufu ekuwayo kawaambia. Yakobo ekuonaho mikokoteni Yusufu ekuwayo kamwegaiya kuwenuwa, roho ya Yakobo tati yae iyawa mwe ufu. 28 Israeli akagombeka, "Yatosha. Yusufu mwanangu ni mgima. Nondaniite nikamkauwe kabla nkizati kufa."