Sura 2

1 Bali wewe, sema yale yanayopatana na mafundisho ya kweli. 2 Wafundishe wanaume wazee kuwa na kiasi, wenye heshima, wenye busara na timamu katika imani, katika upendo, na katika uvumilivu. 3 Vvyo hivyo, fundisha wanawake wazee kuwa na tabia ya heshima, si wasingiziaji, na wasiwe watumwa wa divai nyingi lakini wawe walimu wa yale yaliyo mema. 4 na kufundisha wanawake wadogo kuwapenda waume zao na watoto wao, 5 kuwa na busara, wasafi, watunzaji wazuri wa nyumba zao, na kuwatii waume zao wenyewe, ili neno la Mungu lisisemwe kuwa baya. 6 Vivyo hivyo, watie moyo vijana wa kiume wawe na busara. 7 Katika njia zote jionyeshe mwenyewe kama mfano wa matendo mema. Katika mfundisho yako onyesha uadilifu, heshima, 8 na ujumbe wa ukweli usioweza kukosolewa, ili kwamba yeyote akupingaye aaibishwe kwa sababu hawana ubaya wa kusema juu yetu. 9 Watumwa na wawatii mabwana zao katika kila kitu, wawafurahisha na sio kubishana nao, 10 wasiwaibie, bali waonyeshe nia njema yote, ili kwa njia zote wailete sifa mafundisho kumhusu Mungu mwokozi wetu. 11 Kwa kuwa neema ya Mungu imeonekana kwa ajili ya wokovu wa watu wote. 12 Inatufundisha kukataa mambo yasiyo ya kimungu na tamaa za kidunia, na kuishi maisha ya kiasi, uadilify, na utauwa katika zama hizi, 13 huku tukitazamia kupokea tumaini letu lenye baraka, kuonekana kwa utukufu wa Mungu wetu mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo. 14 Yesu alijitoa nafsi kwa ajili yetu ili atukomboe na maasi yote na kujitakasia watu maalum walio na hamu ya kufanya matendo mema. 15 Yaseme mambo haya, watie watu moyo kuyatimiza na utoe marekembisho kwa mamlaka yote. Usikubali mtu yeyote akupuuze.