Sura 1

1 Paulo, mtumishi wa Mungu na mtume wa Yesu Kristo, kwa ajili ya imani ya wateule wa Mungu na maarifa ya kweli unaopatana na utauwa, 2 na tumaini la uzima wa milele ambao Mungu, asiyesema uongo, aliuahidi kabla ya enzi zote za wakati. 3 Kwa wakati ufaao alilifunua neno lake kwa mahubiri ambayo mimi nimekabidhiwa sawasawa na agizo la Mungu mwokozi wetu. 4 Kwa Tito, mwana wa kweli katika imani tunayoshiriki sote. Neema na amani kutoka kwa Mungu Baba na Yesu Kristo mwokozi wetu. 5 Kwa sababu hii nalikuacha Krete, ili upate kupanga mambo ambayo bado hayajakamilika na kuweka wakfu wazee wa kanisa kwa kila mji kama nilivyokuagiza. 6 Mzee wa kanisa lazima asiwe na lawama, mme wa mke mmoja, aliye na watoto waaminifu wasiotuhumiwa mabaya au wasiotii. 7 Ni muhimu kwa mwangalizi, kama meneja wa nyumba ya Mungu, asiwe na lawama. Asiwe mtu mwenye kiburi, hakasiriki kirahisi, si mraibu wa mvinyo, si mgomvi na asiwe mwenye tamaa. 8 Badala yake: awe mtu mkarimu, apendaye wema, mwenye busara, mnyoofui, mtakatifu na anayejidhibiti. 9 Awezaye kushika sana ujumbe wa kuaminika uliofundishwa, ili aweze kuwatia moyo wengine kwa mafundisho ya ukweli na kuwarekebisha wale wanaompinga. 10 Kwa maana wako waasi wengi, wanenao matupu na wandanganyao, hasa wale wa tohara. 11 Ni muhimu kuwazuia. Wanasumbua familia nzima kwa kufundisha kwa faida isiyofaa yale wasiyopaswa kufundisha. 12 Mmoja wa manabii wa amesema "Wakrete daima ni waongo, wanyama wabaya, walafi wavivu." 13 Ushuhuda huu ni kweli. Kwa hiyo warekebishe kwa ukali, ili wapate kuwa wakweli katika imani, 14 bila kuzingatia hekaya za kiyahudi au amri za watu wanaoiacha kweli. 14 Wewe usijihusishe na hadithi zisizo za kweli za Kiyahudi au amri za watu, ambao hurudisha nyuma ukweli. 15 Kwa wote walio safi, vitu vyote ni visafi. Bali kwa walioharibika na wasioamini, hakuna kilicho kisafi, lakini akili zao na dhamiri zao zimeharibika. 16 Wanakiri kumjua Mungu, lakini kwa matendo yao wanamkana. Wao ni machukizo, wasiotii, na wasiofaa kitu kwa kazi yo yote njema.