Sura 6

1 Mpenzi wako ameenda wapi, uliye mzuri miongoni mwa wanawake? Kwa uelekeo gani mpenzi wako ameenda, ilitumtafute nawe? Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe 2 Mpenzi wangu ameenda katika bustani yake, kwenye vitanda vya manukato, kwenda kula katika bustani na kukusanya nyinyoro. 3 Mimi ni wa mpenzi wangu, na mpenzi wangu ni wangu; hula miongoni mwa nyinyoro kwa raha. Mpenzi wa mwanamke akizungumza naye 4 Wewe ni mzuri kama Tirza, mpenzi wangu, wapendeza kama Yerusalemu, waamasisha kwa utusho kama jeshi lenye bendera mbele. 5 Geuza macho yako mbali na mimi, kwa kuwa yananizidi ukali. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi likishuka chini kutoka miteremko ya Mlima Gileadi. 6 Meno yako ni kama kundi la kondoo likishuka kutoka sehemu ya kuoshwa. Kila mmoja anapacha, na hamna ata mmoja kati yao aliyefiwa. 7 Mashavu yako ni kama majani ya komamanga nyuma ya kilemba chako cha uso. Mpenzi wa mwanamke akizungumza peke yake 8 Kuna malikia sitini, masuria themanini, na wanawake wachanga bila idadi. 9 Hua wangu, wangu asiye na dosari, ni yeye pekee; ni binti pekee wa mama yake; ndiye kipenzi cha mwanamke aliye mzaa. Mabinti wa wenzengu wamemuona na kumuita mbarikiwa; wanawake-malikia na masuria walimuona pia, na wakamsifia: Kile walicho sema wanawake-malikia na masuria 10 "Ni nani huyo anaye jitokeza kama kukicha, mzuri kama mwezi, anayeng'aa kama jua, uamasisha-kwa utisho kama bendera ya jeshi?" Mpenzi wa mwanamke akizungumza mwenyewe 11 Nilienda kwenye kichaka cha miti ya milozi kuona mimea midogo ikikua bondeni, kuona kama mizabibu ilikuwa imechipua, na kama mikomamanga imestawi. 12 Sikujua ni lini nafsi yangu ilinikalisha juu ya gari la farasi wa mfalme wangu waungwana. Mpenzi wa mwanamke akizungumza naye. 13 Geuka nyuma, geuka nyuma, wewe mwanamke mshunami; geuka nyuma, geuka nyuma ili niweze kukutizama kwa mshangao! Mwanamke mdogo akizungumza na mpenzi wake Kwanini wanishangaa, mwanamke mkamilifu, kana kwamba nina cheza katikati ya mistari miwili ya wachezaji?