Sura 5

1 Nimekuja katika bustani yangu, dada yangu, bibi arusi wangu; Nimekusanya udi wangu na manukato yangu. Nimekula sega langu la asali na asali yangu; Nimekunywa mvinyo wangu pamoja na maziwa yangu. Marafiki wanazungumza na wapenzi Kuleni, marafiki; kunyweni na mlewe na mapenzi. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe 2 Nilikuwa nimelala, lakini moyo wangu ulikuwa macho katika ndoto. Sauti ya mpenzi wangu yabisha na kusema, "Nifungulie, dada yangu, mpenzi wangu, hua wangu, usiye na dosari, kwa kuwa kichwa changu kimelowa na matone, nywele zangu kwa unyevu wa usiku." 3 "Nimevua joho langu; je, azima nilivae tena? Nimeosha miguu yangu; je, lazima niichafue tena?" 4 Mpenzi wangu kwa mkono wake kupitia kwenye kitasa cha mlango akanigusa, na moyo wangu ukawa umewaka kwa ajili yake. 5 Nimeamka kumfungulia mlango mpenzi wangu; mikono yangu ikawa yamiminika na manemane, vidole vyangu na unyevu wa manemane, katika komeo la mlango. 6 Nimemfungulia mlango mpenzi wangu, lakini mpenzi wangu alikuwa aligeuka na kuondoka. Moyo wangu ukadidimia aliponena; nikakosa tumaini. Nikamtafuta, lakini sikumpata; nikamuita, lakini hakunijibu. 7 Walinzi waliokuwa wakizunguka mjini walinipata mimi; walinipiga chini na kunijeruhi; askari katika ukuta walichukua nguo yangu ya juu. Mwanamke mdogo akizungumza na wanawake wa mji 8 Ninawataka muape, mabinti wa Yerusalemu, kwamba mkimuona mpenzi wangu, ni kitu gani mtamjulisha? mwambie nimenyong'onyea sababu ya upendo wangu kwake. Wanawake wa mji wakizungumza na mwanamke mdogo 9 Mpenzi wako ana ubora gani kuliko mwanaume mwengine, wewe uliye mzuri miongoni mwa wanawake? Kwanini mpenzi wako bora kuliko mpenzi mwengine, hadi utuulize tuweke nadhiri kama hii? Mwanamke mdogo akizungumza na wanawake wa mji 10 Mpenzi wangu amenawiri na ana ng'aa, kati ya wanaume elfu kumi. 11 Kichwa chake ni dhahabu safi; nywele zake ni laini na nyeusi kama kunguru. 12 Macho yake ni kama ya hua pembezoni mwa vijito vya maji, yameoshwa na maziwa, yameundwa kama mikufu. 13 Mashavu yake ni kama vitanda vya manukato, vinavyotoa arufu ya marashi. Midomo yake ni nyinyoro, inayotiririka manemane. 14 Mikono yake ni ya mianzi ya dhahabu iliyo zungushiwa mikufu; tumbo lake ni pembe lililofunikwa yakuti samawi. 15 Miguu yake ni nguzo za marimari, iliyowekwa juu ya dhahabu safi; muonekano wake ni kama Lebanoni, mizuri kama mierezi. 16 Mdomo wake ni mtamu kuliko; ni mzuri sana wa kupendeza. Huyu ni mpenzi wangu, na huyu ni rafiki yangu, mabinti wa Yerusalemu.