1
Je hekima haiti? Je ufahamu hapazi sauti yake?
2
Juu ya kilima kando ya barabara, kwenye njia panda, hekima anasimama.
3
Kando ya njia ya kuingilia mjini, karibu na milango ya mji, anaita kwa sauti.
4
Watu, ninawaita ninyi na ninapaza sauti yangu kwa wana wa wanadamu.
5
Ninyi wajinga, jifunzeni hekima, na ninyi mnaochukia maarifa, lazima mjipatieni moyo wa ufahamu.
6
Sikiliza na mimi nitasema mambo mazuri na nifumbuapo midomo yangu nitaongea haki.
7
Maana kinywa changu hunena uaminifu na midomo yangu huchukia uovu.
8
Maneno ya kinywa changu yote ni haki; hakuna kilichogeuzwa wala kupotoshwa.
9
Maneno yangu yote yamenyooka kwa yule mwenye kuelewa; maneno yangu ni haki kwa wale wanaotafuta maarifa.
10
Chagua fundisho langu badala ya fedha na maarifa kuliko dhahabu safi.
11
Maana mimi, hekima ni bora kuliko vito; hakuna unachokitamani kinaweza kulinganishwa na mimi.
12
Mimi, hekima, naishi kwa utaratibu, na ninamiliki maarifa na busara.
13
Hofu ya Mungu ni kuchukia uovu nachukia majivuno na kiburi, njia ya uovu, na kauli iliyopotoka- hivyo ninavichukia.
14
Ninaushauri mzuri na hekima sahihi; mimi ni busara; nguvu zipo kwangu.
15
Kwa njia yangu wafalme hutawala- pia na waungwana, na wote ambao hutawala kwa haki.
16
Kwa njia yangu wafalme hutawala na waungwana na wote wanaotawala kwa haki.
17
Nawapenda wale wanaonipenda, na wale wanaonitafuta kwa bidii, wataniona.
18
Kwangu kunautajiri na heshima, utajiri wa kudumu na haki.
19
Tunda langu ni bora kuliko dhahabu, bora hata kuliko dhahabu safi.
20
Ninazalisha kilicho bora kuliko fedha safi. Natembea katika njia ya haki,
21
katika mapito ambayo huelekea kwenye haki, ili niwape urithi wale wanaonipenda na kuzijaza hazina zao.
22
Yehova aliniumba tokea mwanzo, mwazoni mwa matendo yake ya nyakati za kale.
23
Tokea enzi za kale niliwekwa katika nafasi tokea kwanza, tokea mwanzo wa dunia.
24
Kabla ya bahari, mimi nilizaliwa kabla ya kuwepo chemchemi zenye maji tele.
25
Kabla ya milima na vilima kuwekwa, mimi nilizaliwa.
26
Nilizaliwa kabla ya Yehova hajaiumba dunia wala makonde, hata mavumbi ya kwanza katika dunia.
27
Nilikuwepo alipoziimarisha mbingu, wakati alipochora mstari katika sura ya kilindi.
28
Nilikuwepo alipoimarisha anga la juu na wakati wa kutengeneza kina cha chemchemi.
29
Nilikuwepo alipotengeneza mipaka ya bahari, ili maji yasisambae kuvuka pale alipoyaamuru, na wakati anaamuru misingi ya dunia sehemu ya kukaa.
30
Nilikuwa kando yake, kama fundi stadi mkuu, na mimi nilikuwa furaha yake siku kwa siku, nikifurahi mbele zake daima.
31
Nilikuwa nikifurahi katika dunia yake yote na furaha yangu ilikuwa kwa wana wa wanadamu.
32
Na sasa, wanangu, nisikilizeni, maana wale wazishikao njia zangu watakuwa na furaha.
33
Sikilizeni fundisho langu na mpate hekima; wala msilipuuze.
34
Anisikilizaye atakuwa na furaha kila siku akitazama katika malango yangu, akinisubiri pembeni mwa milango ya masikani yangu.
35
Maana yeyote anionaye mimi, anapata uzima, naye atapata kibali kwa Yehova.
36
Na yeyote asiyeniona mimi, hujiumiza mwenyewe, wote wanaonichukia hupenda mauti.