1
Usijisifu kwa ajili ya kesho, maana hujui siku italeta nini.
2
Mtu mwingine akusifu na wala si kinywa chako mwenyewe, mgeni na wala si midomo yako mwenyewe.
3
Fikiria uzito wa jiwe na uzito wa mchanga uchokozi wa mpumbavu ni mzito zaidi kuliko hivyo vyote.
4
Kuna ukatili wenye ghadhabu kali na mafuriko ya hasira, lakini ni nani anayeweza kusimama mbele ya wivu?
5
Ni bora karipio la wazi kuliko upendo uliofichwa.
6
Mwaminifu ni jeraha zilizosababishwa na rafiki, lakini adui anaweza kukubusu kwa kuomba radhi mno.
7
Mtu aliyekula na kushiba hulikataa hata sega la asali, bali kwa mtu mwenye njaa, kila kitu kichungu ni kitamu.
8
Ndege anayezurura kutoka kwenye kiota chake ni kama mtu anayepotea sehemu ambayo anaishi.
9
Marham na manukato huufanya moyo ufurahi, lakini utamu wa rafiki ni bora kuliko ushauri wake.
10
Usimwache rafiki yako na rafiki wa baba yako, na usiende kwenye nyumba ya ndugu yako katika siku ya msiba wako. Ni bora rafiki ambaye yupo karibu kuliko ndugu ambaye yupo mbali.
11
Mwanangu, uwe na busara, moyo wangu ufurahi; kisha nitamjibu yule anayenidhihaki.
12
Mtu mwenye busara huiona taabu na kujificha mwenyewe, lakini mjinga huendelea mbele na kuteseka kwa ajili ya taabu.
13
vazi kama mwenyewe anaweka pesa kama dhamana kwa deni la mgeni; lichukue kama anaweka dhamana kwa malaya.
14
Anayempa jirani yake baraka kwa sauti ya juu mapema asubuhi, baraka hiyo itafikiriwa kuwa laana!
15
Mke mgomvi ni kama siku ya manyunyu ya mvua ya daima;
16
kumzuia ni kama kuuzuia upepo, au kujaribu kushika mafuta kwa mkono wako wa kulia.
17
Chuma hunoa chuma; kwa njia ile ile; mtu humnoa rafiki yake.
18
Yule anayeutunza mtini atakula matunda yake, na yule mwenye kumlinda bwana wake ataheshimiwa.
19
Kama maji yanavyoakisi taswira ya sura ya mtu, ndivyo hivyo moyo wa mtu humwaksi mtu.
20
Kama kuzimu na Uharibifu havitosheki, ndivyo yalivyo macho ya mtu hayawezi kutosheka.
21
Kalibu ni kwa fedha na tanuru ni kwa dhahabu; na mtu hujaribiwa anaposifiwa.
22
Hata kama utamponda mpumbavu kwa mchi pamoja na nafaka bado upumbavu wake hautatoka.
23
Hakikisha unajua hali ya makundi yako na ujishughulishe juu ya makundi yako,
24
maana utajiri haudumu daima. Je taji hudumu kwa vizazi vyote?
25
Majani huondoka na ukuaji mpya huonekana na milima ya chakula cha mifugo hukusanywa ndani.
26
Wanakondoo watakupatia mavazi yako na mbuzi watakupatia gharama ya shamba.
27
Kutakuwa na maziwa ya mbuzi kwa chakula chako chakula kwa kaya yako na chakula kwa watumishi wako wasichana.