1
Kisha Elifazi kutoka kabila la temani akajibu na kusema,
2
Kama mtu yeyote akijaribu kuzungumza na wewe, je utakosa ustahimilivu? Lakini ni nani anaweza kujizuia asizungumze?
3
Tazama, wewe umewafunza wengi; wewe imeipa nguvu mikono iliyokuwa dhaifu.
4
Maneno yako yamemsaidia yeye mwanamme aliyekuwa anaanguka; wewe umeyaimarisha magoti dhaifu.
5
Lakini sasa matatizo yamekuja kwako, na wewe umechoka; yanakugusa wewe, na wewe umetatizika.
6
Je si hofu yako imani yako, na ukamilifu wa njia zako tumaini lako?
7
Tafakari juu ya hili, tafadhari: ni nani aliyeangamia akiwa hana kosa? Au ni lini watu wakamilifu walikatiliwa mbali?
8
Kutokana na vile nilivyoona, wale walimao uovu na kupanda taabu huvuna hayo.
9
Kwa pumzi ya Mungu huangamia; kwa mlipuko wa hasira zake huteketea.
10
Kuunguruma kwa simba, sauti ya simba mkali, meno ya simba wadogo - yamevunjika.
11
Simba mzee huangamia kwa kukosa wahanga; watoto wa simba jike wametawanyiko kila mahali.
12
Sasa nililetewa kwangu jambo fulani kisiri, na sikio langu likapokea uvumi kuhusu hilo.
13
Kisha yakaja mawazo kupitia ndoto wakati wa usiku, wakati uwaangukiwapo usingizi mzito watu..
14
Ilikuwa usiku wakati nilipopatwa hofu na kutetemeka, na mifupa yangu yote ikatikisika.
15
Kisha nafsi ikapita mbele ya uso wangu, na nywele zangu za mwili zilisimama.
16
Nafsi ilisimama kimya, lakini sikuweza kupambanua sura yake. Umbo lilikuwa mbele ya macho yangu; kulikuwa kimya, nami nikasikia sauti ikisema,
17
"Je binadamu anaweza kuwa mwenye haki zaidi kuliko Mungu? Je mtu anaweza kuwa msafi zaidi kuliko muumba wake?
18
Tazama, kama Mungu hawaamini watumishi wake; kama hulaumu upumbavu wa malaika zake,
19
je si zaidi sana ukweli huu kwa wale waishio katika nyumba za udongo, ambao misingi yao ipo katika vumbi, wale waliopondwa mbele ya nondo?
20
Kati ya asubuhi na jioni wameangamizwa; wameangamia milele wala bila yeyote kuwatambua.
21
Je kamba za hema yao hazikung'olewa kati yao? Wanakufa; wanakufa bila hekima.