1
Sasa katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya kumi na tatu ambayo ni siku ya Adari, siku ambayo adui wa Wayahudi walitarajia kutekeleza sheria ya mfalme, na kupata nguvu dhidi ya Wayahudi. Badala yake Wayahudi wakapata nguvu dhidi ya adui zao.
2
Wayahudi wote wakakusanyika katika miji yao katika majimbo yote ya Mfalme Ahusiero, kutia mikono juu ya wale waliokusudia ubaya. Hakuna aliye kuwa tayari kusimama kinyume chao, kwa sababu hofu yao ilikuwa imewaangukia watu wote.
3
Wakuu wote wa majimbo, maakida na magavana, na watawala wa mfalme, waliwasaidia Wayahudi kwa kuwa hofu ya Modekai ilikuwa imewaangukia.
4
Kwa kuwa Modekai alikuwa mkuu katika nyumba ya mfalme, na umaarufu wake, ukasambaa katika majimbo yote, kwa kuwa Modekai alikuwa akifanyika mkuu.
5
Wayahudi wakawavamia maadi zao kwa upanga, wakiwatenda vibaya kama walivyokuwa wamekusudiwa mabaya dhidi yao Wakawatenda kama walivyo ona vyema machoni pao.
6
Katika ngome ya mji wa Shushani pekee jumla ya maadui waliouawa na kuharibiwa na Wayahudi ni wanaume mia tano.
7
Miongoni mwa waliouawa ni pamoja na Parishandatha, Dalphoni, Aspatha,
8
Poratha, Adalia, Aridatha,
9
Parimashita, Arisai, Aridai, Vaizatha,
10
na wana kumi wa Hamani, mwana wa Hammedatha, adui wa Wayahudi. Lakini hawakuchua mateka yoyote.
11
Idadi ya wale waliouawa siku hiyo katika mji wa Shushani, ilifikishwa kwa Mfalme Ahusiero.
12
Mfalme akamwambia Malkia Esta, "Wayahudi wameua wanaume mia tano katika mji wa Shushani, wakiwemo wana kumi wa Hamani adui wa Wayahudi. Je wamefanya nini katika majimbo mengine? Na sasa haja yako ni nini? Utapewa. Ombi lako ni nini?"
13
Esta akamjibu, "Mfalme kama ikikupendeza, ruhusu Wayuadi walio katika mji wa Shushani wapige mbiu hii na kesho, na miili ya watoto wa Hamani itundikwe juu ya miti."
14
Mfalme akaamuru ombi la Esta litekelezwe. Mbiu ilipigwa katika mji wa Shushani, na wana kumi wa Hamani wakatundikwa juu ya miti.
15
Wayahudi katika mji wa Shushani walisanyika pamoja siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari, na kuwaua maadui zao mia tatu katika mji wa Shushani, lakini hawakugusa nyara zao.
16
Na Wayahudi katika majimbo mengine wakakusanyika ili kujilinda na wakapata faraja kutoka kwa maadui,na wakawaua maadui zao elfu sabini na tano, lakini hawakugusa mikono yao kwa vitu vya thamani wale waliouwawa.
17
Katika siku ya kumi na tatu ya mwezi wa Adari, Wayahudi wakapumzika katika siku ya kumi na nne, wakapumzika siku hiyo ya karamu na furaha.
18
Lakini Wayahudi walioishi katika mji wa Shushani wakaja pamoja siku ya kumi na tatu na ya kumi na nne. Na siku ya kumi na tano,wakapumzika na wakafanya karamu na kufurahia.
19
Hii ndiyo sababu Wayahudi wa vijijini, wanaishi maeneo ya vijijini, huadhimisha siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari kama siku ya furaha na karamu na siku ambayo hutumiana zawadi kwa kila mmoja.
20
Modekai akaweka mambo haya na akatuma nyaraka kwa Wayahudi wote waliokuwa katika utawala wa Mfalme Ahusiero,
21
akiwataka kuadimisha siku ya kumi na nne na kumi na tano ya mwezi wa Adari kila mwaka.
22
Hizi zilikuwa ndizo siku ambazo Wayahudi walipata faraja kutoka kwa maadui zao, na wakati huu ndio wakati ambao huzuni ya Wayahudi iligeuzwa kuwa furaha, na kutoka kwa maombolezo hadi kwenye pumziko. Walipaswa kuzifanya siku za karamu na furaha, na kutumiana zawadi ya chakula, na zawadi kwa masikini.
23
Wayahudi wakaendelea na maadhimisho wakifanya kile ambacho Modekai alikuwa amewaandikia.
24
Na wakati huo Hamani mwana wa Hammedatha mwagagi, adui wa Wayahudi aliyekuwa amepanga njama ya kuwaangamiza Wayahudi, na kwa kupiga Puri (yaani akapiga kura) ili kuwaangamiza kabisa.
25
Lakini Mfalme Ahusiero alipopata taarifa ya mpango mbaya huu alioupanga Modekai dhidi ya Wayahudi, aliagiza kwa nyaraka afanyiwe Modekai mwenyewe, na kwamba yeye na wana wake wanyongwe juu ya miti.
26
Hivyo Wayahudi wakaziita siku hizi Purimu, kutokana na jina Puri. Kwa sababu ya mambo yote yaliyo kuwa yameandika katika barua, na mambo yote ambayo walikuwa wameyaona kwa macho yao, na yale yalikuwa yamewapata,
27
Wayahudi wakapokea jukumu na desturi mpya. Desturi hii iwe kwa ajili yao, watoto wao, na kila ambaye aliyeungana nao. Na itakuwa kwamba maadhimisho haya watayafanya kwa kila mwaka. Wataadhimisha kwa namna fulani na nyakati hizo hizo kila mwaka.
28
Siku hizi zilipaswa kuadhimishwa katika kila kizazi, kila familia, kila jimbo na kwa kila mji. Wayahudi hawa na watoto wao hawakuacha kuadhimisha siku hizi za Purimu, ili kwamba wasizisahau.
29
Malkia Esta na Modekai wakaandika kwa mamlaka yote na kuthibitisha barua hii ya pili kuhusu Purimu.
30
Barua zilipelekwa katika majimbo 127 ya mfalme Ahusiero, zikiwatakia Wayahudi wote amani na kweli.
31
Na kuthibitisha siku za Purimu sawa sawa na maelekezo ya Modekai na Esta yaliyowataka Wayahudi waadhimishe. Wayahudi wakatii maagizo kwa ajili yao na uzao wao, kama walivyotii siku za kufunga na kuomboleza.
32
Agizo la Esta likahakikisha sheria hizi kuhusu Purimu, na ikaandikwa katika kitabu.