SURA 8

1 Siku hiyo Mfalme Ahusiero akampa Malkia Esta mali yote ya Hamani, adui wa Wayahudi. Na kisha akampandisha cheo Modekai ili atumike mbele zake, kwa sababu Malkia Esta alikuwa amemueleza Mfalme uhusiano wake na Modekai. 2 Kisha Mfalme akampa pete yake aliyokuwa amempa Hamani. Malkia Esta akampandisha Modekai ili awe mkuu katika shamba la Hamani. 3 Kisha Esta akaongea tena na mfalme. Akaanguka chini na kulia mbele za mfalme, akimsihi Mfalme abatilishe njama ya kuwaua Wayahudi wote, iliyokuwa imetangazwa na Hamani Muagagi 4 kisha mfalme akamnyoshea Esta fimbo yake ya dhahabu, akainuka na kusimama mbele ya mfalme. 5 Esta akasema, "Kama ikikupendeza na kama nimepata kibali mbele zako, agiza mbiu ipigwe ili kubatilisha barua zilizoandikwa na Hamani mwana wa Hammedatha muagagi, barua alizoziandika ili kuwaangamiza Wayahudi wote walikuwa katika majimbo yote ya mfalme. 6 Ninawezaje kuona ubaya ukiwapa watu wangu? Ninawezaje kutazama uharibifu wa jamaa zangu?" 7 Mfalme Ahusiero akamwambia Esta na Modekai, Muyahudi, tazama nimempa Esta nyumba yote ya Hamani,na wamemtundika Hamani katika mti kwa sababu,alikuwa amekusudia kuwaangamiza Wayahudi wote. 8 Hivyo andika mbiu nyingine kwa ajili ya Wayahudi kwa jina la mfalme na uipige muhuri kwa pete ya mfalme. Kwa sababu mbiu imekwisha andikwa kwa jina la mfalme na kugongwa muhuri kwa pete ya mfamle, na haiwezi kubatilishwa." 9 Kisha waandishi wa mfalme wakakusanyika kwa wakati huo huo katika mwezi wa tatu, ambao ni mwezi wa Sivani, siku ya ishirini ya mwezi wa tatu. Mbiu iliandikwa yote ambayo Modekai aliyaamuru kwa Wayahudi watendewe na wenyeji wa kila jimbo. Mbiu iliandikwa kwa maakida, magavana na wakuu wa majimbo yote yaliyokuwa ,toka India hadi Ethiopia, majimbo 127 kila jimbo iliandikwa kuwa maandishi yake, na kila watu kwa lugha yao, na kwa Wayahudi kwa maandishi na lugha yao. 10 Modekai akaandika kwa jina la Mfalme Ahusiero na akazipiga muhuri kwa pete ya mfalme. Akapeleka nyaraka kwa matarishi, akawapandisha kwenye farasi waendao kwa haraka waliotumika kwa huduma ya mfalme, waliozaliwa kwa mfalme. 11 Mfalme akawapa Wayahudi wote katika majimbo ya utawala wake kibali cha kukusanyika ,na kujilinda, na ruhusa ya kuangamiza, kuua na kuharibu mtu yeyote aliyekuwa na kusudi la kuwaua Wayahudi wote na kupora mali zao. 12 Jambo hili lilipaswa litekelezwe katika majimbo yote ya Mfalme Ahusiero, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, ambao ni mwezi wa Adari. 13 Nakala ya mbiu ilipaswa kutolewa kama sheria na kutangazwa kwa watu wote. Wayahudi walikuwa tayari kwa siku hiyo kulipa kisasi kwa adui zao. 14 Hivyo matarishi wakaendesha farasi waliokuwa wakitumiwa katika huduma za kifalme. Walienda kwa haraka sana. Mbiu hii pia ilikuwa imetolewa katika mji wa Shushani pia. 15 Kisha Modekai akaondoka mbele za mfalme akiwa amevaa mavazi ya kifalme, nguo buluu na nyeupe, na taji kubwa ya dhahabu,na joho la zambarau. Mji wa Shushani ukafurahia. 16 Wayahudi walikuwa na nuru, na furaha na heshima. Mji wowote ambao mbiu hii ilipigwa, Wayahudi walifurahia na walifanya karamu na pumziko. 17 Watu wengi wakatamani kuwa Wayahudi sababu ya hofu ya Wayahudi iliyokuwa juu yao.