Wakolosai 3

1 Ikwa basi mungu amewafufua pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo ya juu juu ambako Kristo anakaa mkono wa kuume wa Mungu. 2 Fikirini kuhusu mambo ya juu,sio kuhusu mambo ya duniani. 3 kwa maana mlikufa na maisha yenu yamefichwa pamoja na kristo ndani ya mungu. 4 Wakati kristo atakapoonekana,ambaye ni maisha yenu,ndipo nanyi pia mtakapoonekana, naye katika utukufu. 5 Kwa hiyo yafisheni mambo yaliyo katika nchi yaani, uasherati, uchafu, shauku mbaya, tamaa mbaya, na tamaa, ambayo ni ibada ya sanamu. 6 Ni kwa ajili ya mambo haya ghadhabu ya Mungu inakuja juu ya wana wasio tii. 7 Ni kwa ajili ya mambo haya ninyi pia mlitembea kwayo mlipoishi kati yao. 8 Lakini sasa ni lazima myaondoe mambo haya yote. Yaani, ghadhabu, hasira, nia mbaya, matusi, na maneno machafu yatokayo vinywani mwenu. 9 Msidanganyane ninyi kwa ninyi, kwa kuwa mmeuvua utu wenu wa kale na matendo yake. 10 Mmevaa utu upya, unaofanywa upya katika maarifa sawasawa na mfano wa yule aliyeuumba. 11 Ambapo hakuna mgiriki wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, mgeni,mskithi,mtumwa, mtu huru , bali Kristo ni yote katika yote. 12 Kama wateule wa Mungu, watakatifu na wapendwao, jivikeni utu wema, ukarimu, unyenyekevu, upole na uvumilivu. 13 Chukulianeni ninyi kwa ninyi. Hurumianeni kila mtu na mwenzake. Kama mtu analalamiko dhidi ya mwingine, amsamehe kwa jinsi ileile ambayo Bwana alivyo wasamehe ninyi. 14 Zaidi ya mambo haya yote, muwe na upendo, ambao ndio kifungo cha ukamilifu. 15 Amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu. Ilikuwa ni kwa ajili ya amani hii mliitiwa katika mwili mmoja. Na muwe na shukrani. 16 Na Neno la Kristo likae kwa wingi ndani yenu,Kwa hekima yote, fundishaneni na kushauriana ninyi kwa ninyi katika hekima yote,mkimwimbia saburi, na nyimbo,na tenzi za rohoni. kwa kushukuru mioyo mwenu kwa Mungu. 17 Na lolote mfanyalo,kwa neno au katika matendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu. Mpeni shukrani Mungu baba kupitia Yeye. 18 Wake, wanyenyekeeni waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana. 19 Nanyi waume, wapendeni wake zenu, na msiwe wakali dhidi yao. 20 Watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote, maana ndivyo impendezavyo Bwana. 21 Akina baba msiwachokoze watoto wenu, ili kwamba wasije wakakata tamaa. 22 Watumwa, watiini mabwana zenu katika mwili kwa mambo yote, sio kwa huduma ya macho kama wapendezao watu tu, bali kwa moyo wa kweli.Mcheni Mungu. 23 Chochote mfanyacho, fanyeni kutoka nafsini mwenu kama kwa Bwana na si kama kwa wanadamu. 24 Mnajua ya kwamba mtapokea ujira wa urithi kutoka kwa Bwana. Ni Kristo Bwana mnayemtumikia. 25 Kwa sababu yeyote atendaye yasiyo haki atapokea hukumu kwa matendo yasiyo haki aliyoyafanya, na hakuna upendeleo.