1
Kulikuwa na njaa kwa miaka mitatu katika siku za utawala wa Daudi, na Daudi akautafuta uso wa Yahwe. "Hivyo Yahwe akasema, "njaa hii ni kwa sababu ya mauaji ya Sauli na familia yake, kwa kuwa aliwauwa Wagibeoni."
2
Basi Wagibeoni hawakuwa uzao wa Israeli; walikuwa ni masalia ya Waamori. Watu wa Israeli walikuwa wameapa kutowauwa, lakini Sauli alitaka kuwaangamiza wote kwa husuda kwa ajili ya watu wa Israeli na Yuda.
3
Ndipo Daudi alipowaita pamoja Wagibeoni na kuwaambia, "Niwafanyie nini kwa ajili ya upatanisho? Ili kwamba mweze kuwabariki watu wa Yahwe wanaorithi wema na ahadi zake?"
4
Wagibeoni wakamjibu, "Hili siyo jambo la fedha wala dhahabu kati yetu na Sauli au familia yake. Na siyo hitaji letu kumuua mtu yeyote katika Israeli." Daudi akasema, "manasema nini ili niwafanyie nyinyi?"
5
Wakamjibu mfalme, "Mtu aliyetaka kutuuwa aliyepanga kinyume chetu, ili kutuangamiza na kukosa eneo katika mipaka ya Israeli -
6
haya na tupewe watu saba kutoka katika uzao wake, nasi tutawatundika mbele ya Yahwe katika Gibea ya Sauli, palipochaguliwa na Yahwe." Mfalme akasema, "Nitawapeni"
7
Lakini mfalme akamuifadhi Mefiboshethi mwana wa Yonathani mwana wa Sauli, kwa ajili ya kiapo cha Yahwe kati ya Daudi na Yonathani mwana wa Sauli.
8
Mfalme akawachukua wana wawili wa Rispa binti Ayia aliomzalia Sauli, hawa wana wawili waliitwa Armoni na Mefiboshethi; na pia Daudi akawachukua wana watano wa Mikali binti Sauli, aliomzalia Adrieli mwana wa Berzilai Mmeholathi.
9
Akawaweka katika mikono ya Wagibeoni. Nao wakawatundika juu ya mlima mbele za Bwana, na wote saba wakafa pamoja. Waliuawa katika kipindi cha mavuno, katika siku ya kwanza mwanzoni mwa mavuno ya shayiri.
10
Kisha Rispa, binti Aiya, akachukua nguo ya gunia na akajitanda mwenyewe juu ya mlima kando ya miili ya waliokufa tangu mwanzo wa mavuno mpaka wakati mvua ilipoanza kunyesha. Hakuruhusu ndege wa angani kutua juu ya miili mchana wala hayawani wa mwituni wakati wa usiku.
11
Daudi akaambiwa alichokifanya Rispa, binti Aiya, suria wa Sauli.
12
Hivyo Daudi akaenda na kuchukua mifupa ya Sauli na mifupa ya Yonathani mwanawe kutoka kwa watu wa Yabeshi Gileadi, waliokuwa wameiiba kutoka katika eneo la jumuiya la Beth Shani, Wafilisti walipokuwa wamewatundika baada ya Wafilisti kumuua Sauli katika Gilboa.
13
Daudi akaiondoa pale mifupa ya Sauli na mifupa ya Yonathani mwanawe, na wakakusanya pia mifupa ya wale watu saba waliotundikwa.
14
Wakaizika mifupa ya Sauli na Yonathani mwanawe huko Zela katika nchi ya Benjamini, katika kaburi la Kishi babaye. Wakafanya kila alichoagiza mfalme. Ndipo Mungu akajibu maombi yao kwa ajili ya nchi.
15
Kisha Wafilisti wakaenda tena katika vita na Israeli. Hivyo Daudi na jeshi lake wakashuka na kupigana na Wafilisti. Akiwa vitani Daudi akachoshwa na vita.
16
Ishbibenobu, wa uzao wa Warefai, ambaye mkuki wake wa shaba ulikuwa na uzito wa shekeli mia tatu na alikuwa na upanga mpya, alitaka kumuua Daudi.
17
Lakini Abishai mwana wa Seruya akamuokoa Daudi, akampiga Mfilisti na kumuua. Ndipo watu wa Daudi wakamuapia, kusema, "Hautakwenda vitani pamoja nasi tena usije ukaizima taa ya Israeli."
18
Ikawa baadaye kuwa na vita tena kati ya Wafilisti huko Gobu, wakati Sibekai Mhushathi alipomuua Safu, aliyekuwa miongoni mwa uzao wa Warefai.
19
Ikawa tena katika vita na Wafilisti huko Gobu, huyo Elhanani mwana wa Jari Mbethlehemu akamuua Goliathi Mgiti, ambaye fumo la mkuki wake lilikuwa kama mti wa mfumaji.
20
Ikawa katika vita nyingine huko Gathi kulikuwa na mtu mrefu sana mwenye vidole sita katika kila mkono na vidole sita katika kila mguu, jumla yake ishirini na vinne. Yeye naye alikuwa wa uzao wa Warefai.
21
Alipowatukana Israeli, Yonathani mwana mwana wa Shama, nduguye Daudi, akamuua.
22
Hawa walikuwa wa uzao wa Warefai wa Gathi, waliuawa kwa mkono wa Daudi na kwa mkono wa askari wake