1
Kisha Ayubu akajibu na kusema,
2
"Hata hivi leo malalamiko yangu ni machungu; maumivu yangu ni mazito kuliko manung'uniko yangu.
3
Ee, ningejua niwezapokumwona mungu! Ee, kwamba ningeweza kwenda alipo!
4
Ningeweka shitaka langu mbele yake na kukijaza kinywa changu hoja.
5
Ningejua ambavyo angenijibu na kufahamu ambavyo angesema juu yangu.
6
Je angehojiana nami katika ukuu wa nguvu zake? Hapana, angenisikiliza.
7
Pale mwenye haki angehojiana nami. Kwa njia hii ningeonekana bila hatia kwa mwamzi wangu.
8
Tazama, naelekea mashariki, lakini hayupo pale, na upande wa magharibi, lakini siwezi kumwona.
9
Kaskazini, anapofanya kazi, lakini siwezi kumwona, na kusini, anapojificha hata nisimwone.
10
Lakini anaijua njia ninayoichukua; atakapokuwa amenipima, nitatoka kama dhahabu.
11
Mguu wangu umeunganishwa na hatua zake; nimezitunza njia zake na sijageuka.
12
Sijaiacha amri ya midomo yake; nimeyatii maneno ya kinywa chake.
13
Lakini yeye ni wa pekee, naniawezaye kumgeuza? Analolitaka, hulitenda.
14
Kwa maana hulitimiza agizo lake kinyume changu; anamipango mingi kwa ajili yangu; ipo mingi kama hiyo.
15
Kwa hiyo, nimetishwa mbele zake; ninapofikiri kumhusu, ninamwogopa.
16
Kwani Mungu ameudhoofisha moyo wangu; Mwenyezi amenitisha.
17
Si kwa sababu nimeondolewa na giza, wala siyo kwamba giza nene limeufunika uso wangu.