1 Lakini Sauli, bado akiendelea kuongea vitisho hata vya kifo kwa wanafunzi wa Bwana, alikwenda kwa kuhani mkuu 2 na kumwomba barua kwa ajili ya masinagogi huko Dameski, ili kwamba akimpata mtu aliye katika Njia ile, awe mwanaume au mwanamke, awafunge na kuwaleta Yerusalemu. 3 Hata alipokuwa akisafiri, ilitokea kwamba alipokaribia Dameski, ghafla mwangaza ikaangaza kotekote nuru kutoka mbinguni,' 4 naye akaanguka chini na akasikia sauti ikimwambia,"Sauli, Sauli, mbona wanitesa mimi?" 5 Sauli akajibu, "U nani wewe Bwana? Bwana akasema, " Mimi ndiye Yesu ambaye unamtesa; 6 Lakini inuka, ingia mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda 7 Wale watu waliosafiri pamoja na Sauli wakasimama kimya, wakisikiliza sauti, wasione mtu. 8 Sauli akainuka kutoka ardhini, na alipofungua macho yake, hakuweza kuona kitu, hivyo wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski. 9 Kwa siku tatu alikuwa haoni, naye hakula, wala kunywa. 10 Basi palikuwapo mwanafunzi Dameski jina lake Anania,Bwana alisema naye katika maono, "Anania!" Naye akajibu akasema,"nipo hapa, Bwana”. 11 "Bwana akamwambia, "Inuka uende zako katika mtaa uitwao Nyoofu, na katika nyumba ya Yuda na ukaulize mtu kutoka Tarso aitwaye Sauli; maana angali anaomba; 12 Ameona katika maono mtu jina lake Anania akiingia na kumwekea mikono juu yake ili apate kuona tena." 13 Lakini Anania akajibu, "Bwana, nimesikia kutoka kwa watu wengi kuhusu mtu huyu, kwa kiasi gani amewafanyia mabaya watu wako watakatifu walioko Yerusalemu; 14 Anayo mamlaka kutoka kwa kuhani mkuu kuweka katika vifungo kila mmoja anayeliitia Jina lako 15 Lakini Bwana akamwambia, "Nenda, kwa maana yeye ni chombo teule kwangu, kulibeba jina langu mbele ya watu wa Mataifa na wafalme na wana wa Israeli 16 kwa maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya jina langu". 17 Hivyo Anania akaondoka, akaingia mle nyumbani; Akaweka mikono yake juu yake, akasema, "Ndugu Sauli, Bwana Yesu, aliyekutokea katika njia ulipokuwa unakuja, amenituma ili upate kuona tena na ujazwe Roho Mtakatifu.." 18 Mara vitu kama magamba vilianguka kutoka kwa macho ya Sauli, naye akapata kuona, akasimama, ;na kubatizwa; 19 akala chakula na kupata nguvu. Akakaa pamoja na wanafunzi huko Dameski kwa siku kadhaa. 20 Wakati huo huo akamtangaza Yesu katika masinagogi, akisema kwamba yeye ni Mwana wa Mungu. 21 Na wote waliosikia walishangaa na kusema, "Siyo mtu huyu aliyewaharibu wote walioita Jina hili huko Yerusalemu? Na hapa amekuja kwa kusudi la kuwafunga na kuwapeleka kwa makuhani." 22 Lakini Sauli aliwezeshwa kuhubiri kwa nguvu zaidi na zaidi,naye alikuwa akisababisha dhiki miongoni mwa Wayahudi waliokaa Dameski, akithibitisha ya kuwa Yesu ndiye Kristo. 23 Baada ya siku nyingi,Wayahudi walipanga shauri pamoja ili wamuue. 24 Lakini mpango wao ukajulikana na Sauli. Wakamvizia mlangoni mchana na usiku wapate kumuua. 25 Lakini wanafunzi wake wakamchukua usiku na kumteremsha kupitia ukutaukutani wakitumia kikapu. 26 Wakati Sauli alipofika Yerusalemu, alijaribu kujiunga na wanafunzi lakini walikuwa wakimuogopa, wasisadiki kuwa yeye ni mwanafunzi. 27 Lakini Barnaba akamchukua na kumpeleka kwa mitume, na akawaeleza jinsi Sauli alivyomuona Bwana njiani na Bwana alivyozungumza naye, na jinsi Sauli alivyohubiri kwa ujasiri kwa jina la Yesu huko Dameski. 28 Alikuwa pamoja nao walipoingia na kutoka Yerusalemu. Akanena kwa ujasiri kwa jina la Bwana Yesu, 29 huku akijadiliana na Wayahudi wa Kiyunani lakini walizidi kujaribu mara kwa mara kumuua. 30 Wakati ndugu walipojua jambo hilo, wakamleta Kaisaria, na kumpeleka Tarso. 31 Basi kanisa lote katika Uyahudi, Galilaya na Samaria, lilikuwa na amani, na likajengwa, na likatembea katika hofu ya Bwana na faraja ya Roho Mtakatifu, kanisa likakua kwa kuongezeka idadi. 32 Kisha ilitokea Petro alipokuwa akizungukazunguka pande zote za mkoa, alishuka pia kwa watu watakatifu wa Mungu waishio katika mji wa Lida. 33 Akamuona huko mtu mmoja jina lake Ainea, aliyekuwa kitandani kwa miaka minane; maana alikuwa amepooza. 34 Petro akamwambia, "Ainea, Yesu Kristo akuponye, Inuka na utandike kitanda chako," .Mara akainuka 35 na watu wote waliokaa Lida na Sharoni wakamwona mtu huyo, wakamgeukia Bwana. 36 Sasa palikuwa na mwanafunzi Yafa aitwaye Tabitha,( ikitafsiriwa"Dorcas”) Huyu mwanamke alijaa kazi njema na matendo ya huruma aliyowatendea maskini. 37 Ilitokea katika siku hizo aliugua na akafa; walipomsafisha, walimpandisha chumba cha juu na kumlaza, 38 Kwa vile Lida ilikuwa karibu na Yafa, na wanafunzi walisikia kwamba Petro alikuwa huko, waliwatuma watu wawili kwake, wakimsihi, "Njoo kwetu bila kuchelewa". 39 Petro akaamka na akaondoka pamoja nao. Alipofika, walimleta katika chumba cha juu. Na wajane wote walisimama karibu naye wakilia, wakimwonyesha kanzu na nguo ambazo Dorcas aliwashonea wakati alikuwa pamoja nao. 40 Petro akawatoa wote nje ya chumba, akapiga magoti akaomba, kisha akaugekia mwili, akasema, "Tabitha, inuka". Hapo akafungua macho yake na alipomwona Petro aakakaa chini. 41 Kisha Petro akampa mkono wake akamwinua, na alipowaita watu watakatifu wa Mungu na wajane, akawakabidhi kwao akiwa hai. 42 Jambo hili likajulikana Yafa yote,na watu wengi wakamwamini Bwana. 43 Ilitokea Petro akakaa siku nyingi huko Yafa na mtu mmoja jina lake Simoni, mtengeneza ngozi.