Sura 7

1 Kuhani mkuu akasema,"mambo haya ni ya kweli"? 2 Stephano akasema, "Ndugu na mababa zangu,nisikilizeni mimi: Mungu wa utukufu alimtokea baba yetu Abrahamu wakati alipokuwa Mesopotamia, kabla hajaishi Harani,' 3 akamwambia,' Ondoka katika nchi yako na jamaa zako na uende katika nchi nitakayokuonyesha'. 4 Kisha akaondoka katika nchi ya Ukaldayo akaishi Harani, kutoka hapo, baada ya baba yake kufa, Mungu akamleta kwenye nchi hii, mnayoishi sasa. 5 Hakumpa chochote kama urithi wake, hapakuwa na sehemu hata ya kuweka mguu. Lakini Abrahamu aliahidiwa hata kabla hajapata mtoto kuwa atapewa nchi kama miliki yake na uzao wake. 6 Mungu alinena naye hivi,ya kwamba uzao wake wangeishi kwa muda katika nchi ya ugeni, na kwamba wenyeji wa huko watawafanya kuwa watumwa wao  na kuwanyanyasa kwa muda wa miaka mia nne. 7 Na Mungu akasema, nitalihukumu taifa ambalo litawafanya mateka, nawatumwa, na baada ya hapo watatoka na kuniabudu katika sehemu hii mahali hapa.' 8 Badaaye Mungu akampa Abrahamu agano la tohara, hivyo,Abrahamu akawa baba wa Isaka akamtahiri siku ya nane; Isaka akawa baba wa Yakobo, na Yakobo akawa baba wa mababa zetu kumi na wawili. 9 Kwa sababu mababa zetu walimwonea wivu Yusufu walimuuza katika nchi ya Misri, lakini Mungu alikuwa pamoja naye, 10 na akamwokoa kutoka dhiki yake yote, na akampa fadhili na hekima mbele ya Farao mfalme wa Misri. Farao akamfanya awe mtawala juu ya Misri na juu ya nyumba yake yote. 11 Basi kukawa na njaa kuu na dhiki kuu katika nchi ya Misri na Kanani, na baba zetu hawakupata chakula. 12 Lakini Yakobo aliposikia kwamba kuna nafaka Misri, aliwatuma baba zetu kwa safari yao ya kwanza. 13 Katika safari yao ya pili Yusufu akajionyesha kwa ndugu zake, na familia ya Yusufu ikajulikana kwa Farao. 14 Yusufu akawatuma ndugu zake kwenda kumwambia Yakobo baba yao aje Misri, pamoja na jamaa yake yote, jumla ya watu wote ni sabini watano. 15 Hivyo Yakobo akashuka Misri; kisha akafa yeye pamoja na baba zetu. 16 Wakachukuliwa hata Shekemu wakazikwa katika kaburi ambalo Abrahamu alilinunua kwa vipande vya fedha kutoka kwa wana wa Hamori huko Shekemu. 17 Wakati wa ile ahadi ambayo Mungu alimwahidi Abrahamu ulipokaribia, watu wakaongezeka huko Misri, 18 wakati huo aliinuka mfalme mwingine juu ya Misri, mfalme ambaye hakujua kuhusu Yusufu. 19 Huyo mfalme mwingine akawahandaa watu wetu na kuwatenda mabaya baba zetu, na kuwatupa watoto wao wachanga .wasiishi. 20 Katika kipindi kile Musa alizaliwa; alikuwa mzuri mbele za Mungu, akalelewa na kwa miezi mitatu akilelewa kwenye nyumba ya baba yake. 21 Wakati alipotupwa, binti wa  Farao alimchukua akamlea kama.mwanawe.                    . 22 Musa alifundishwa katika hekima yote ya kimisri, alikuwa Mwenye nguvu katika maneno na matendo yake. 23 Lakini baada yakutimiza miaka arobaini, ikamjia katika moyo wake kuwatembelea ndugu zake, wana wa Israeli. 24 Alipomwona Mwisraeli akitendewa mabaya, Musa alimtetea na kulipiza kisasi aliyekuwa akimwonea kwa kumpiga Mmisiri: 25 akifikiri kuwa ndugu zake watafahamu kwamba Mungu anawaokoa kwa mkono wake lakini hawakuelewa. 26 Siku iliyofuata akaenda kwa baadhi ya Waisraeli waliokuwa wanagombana akajaribu kuwapatanisha;akisema ",mabwana nyinyi ni ndugu; mbona mnakoseana ninyi kwa ninyi,?" 27 Lakini aliyekuwa amemkosea jirani yake akamsukumia mbali, na kusema, 'Nani kakufanya mtawala na muhukumu wetu?' 28 "Wewe unataka kuniua, kama ulivyomuua Mmisri jana?" 29 Musa akakimbia baada ya kusikia hivyo; akawa mgeni katika nchi ya Midiani, ambapo alipata kuwa baba wa wana wawili wa kiume. 30 Baada ya miaka arobaini kupita, malaika akamtokea katika jangwa la mlima Sinai, katika mwali wa moto ndani ya kichaka. 31 Wakati Musa alipoona moto,alishangaa na kustaajabia kile alichokiona, na alipojaribu kukisogelea ili kukitazama, sauti ya Bwana ikamjia Ikisema, 32 'Mimi ni Mungu wa baba zako,Mungu wa Abrahamu, na wa Isaka, na wa Yakobo'. Musa alitetemeka na hakuthubutu kuangalia. 33 Bwana akamwambia, 'Vua viatu vyako, maana sehemu unakosimama ni mahali patakatifu. 34 Kwa hakika nimeona mateso ya watu wangu waliopo Misri; Nimesikia kuugua kwao, nami nimeshuka ili niwaokoe; sasa njoo,nitakutuma wewe Misri.' 35 Huyu Musa ambaye walimkataa wakati waliposema, 'nani kakufanya kuwa mtawala na mwamuzi wetu?'_- alikuwa ndiye ambaye Mungu alimtuma awe mtawala na mkombozi.Mungu alimtuma kwa mkono wa malaika ambaye alimtokea Musa kichakani. 36 Musa aliwaongoza kutoka Misri baada ya kufanya miujiza na ishara katika Misri na katika bahari ya Shamu, na katika jangwa kwa kipindi cha miaka arobaini. 37 Ni huyu huyu Musa aliyewaambia wana wa Isiraeli kuwa, 'Mungu atawainulieni nabii kutoka miongoni mwa ndugu zenu, nabii kama mimi'. 38 Huyu ni mtu ambaye alikuwa katika makutano jangwani na malaika ambaye aliongea naye katika mlima Sinai. Huyu ndiye mtu ambaye alikuwa na mababa zetu,na ambaye alipokea neno lililo hai na kutupatia sisi. 39 Lakini mababa zetu walikataa kumtii; walimsukumia mbali nao, na katika mioyo yao waligeuka kurudi Misri. 40 Katika kipindi hicho walimwambia Haruni.'tutengenezee miungu itakayotuongoza.Kwakua huyu Musa, aliyekuwa akituongoza kutoka katika nchi ya Misri, hatujui kilichompata.' 41 Hivyo wakatengeneza ndama siku hizo na wakatoa sadaka kwa hiyo sanamu na wakafurahi kwa sababu ya kazi ya mikono yao. 42 Lakini Mungu aliwageuka na kuwapa waabudu nyota wa angani, kama ilivyoandikwa kwenye kitabu cha manabii, 'Je Mmenitolea mimi sadaka za wanyama mliowachinja jangwani kwa muda wa miaka arobaini, nyumba ya Israeli? 43 Mmekubali hema ya kukutania ya Moleki na nyota ya mungu refani, na sanamu mlizozitengeneza kuziabudu: na nitawapeleka mbali zaidi ya Babeli.' 44 Baba zetu walikuwa na hema ya kukutania ya ushuhuda jangwani, kama Mungu alivyoamuru alipoongea na Musa,kwamba angeitengeneza kwa ilimpasa aitengeneze  mfano wa muundo ule aliouona. 45 Baadaye mababa zetu chini ya Yoshua walipokea hli hema ambayo,waliibeba pamoja nao walipoitwaa nchi.Mungu aliitwaa nchi kutoka kwa mataifa alipowafukuza mbele ya uso wa mababa zetu.Hema ile ilikaa katika nchi mpaka wakati wa Daudi, 46 ambaye alipata kibali machoni pa Mungu,' na akaomba kutafuta makao ya Mungu wa Yakobo. 47 Lakini ni Selemani alimjengea Suleimani aliyejenga nyumba ya Mungu. 48 Hata hivyo Aliye Juu sana haishi kwenye nyumba zilizojengwa kwa mikono; hii ni kama nabii alivyosema 49 Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni sehemu ya kuwekea miguu yangu. Nyumba ya aina gani mtanijengea?, asema Bwana: au ni wapi sehemu yangu ya kupumzikia? 50 Siyo mkono wangu uliofanya hivi vitu vyote?' 51 Enyi watu wenye shingo ngumu msiotahiriwa mioyo na masikio, kila mara mnampinga Roho Mtakatifu,' mnatenda kama baba zenu walivyotenda. 52 Ni nabii yupi katika manabii ambaye baba zenu hawakumtesa?. Waliwaua manabii wote waliotokea kabla ya ujio wa Mmoja mwenye Haki,'na sasa mmekuwa wasaliti na wauaji wake pia, 53 enyi watu mliopokea sheria ile iliyoagizwa na malaika lakini hamkuishika." 54 Kisha wajumbe wa baraza waliposikia mambo haya,walighadhabika sana mioyoni mwao, na wakamsagia meno Stefano. 55 Lakini yeye, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, alitazama mbinguni kwa makini na akauona utukufu wa Mungu,' na kumwona Yesu amesimama mkono wa kuume wa Mungu. 56 Stefano akasema,"Angalia nimeona, ninaona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adam amesimama mkono wa kuume wa Mungu." 57 Lakini kwa hili wajumbe wa baraza waliziba masikio yao na kupiga kelele kwa sauti za juu, wakaziba masikio yao, wakamkimbilia na kumvamia kwa pamoja,na kusudi moja. 58 kwa nguvu wakamtupa nje ya mji na wakampiga mawe: na mashahidi wakavua nguo zao za nje na kuweka chini karibu na miguu ya  kijana aliyeitwa Sauli. 59 Walipokuwa wakimpiga mawe Stefano, aliendelea kumwita Bwana na kusema, "Bwana Yesu, pokea roho yangu,". 60 Akapiga magoti na kulia kwa sauti kubwa"Bwana, usiwahesabie dhambi hii’ Aliposema haya,akakata roho.