1 Wana wa Rubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli - sasa Rubeni alikuwa mzaliwa wa kwanza wa Israeli, lakini haki yake ya mzaliwa wa kwanza ilipewa kwa wana wa Yusufu mwana wa Israeli kwa sababu Rubeni alinajisi kochi la baba yake. Kwa hivyo hajaandikwa katika nasaba kuwa ana haki ya mzaliwa wa kwanza. 2 Yuda ndiye alikuwa na nguvu kati ya ndugu zake, na kiongozi angetoka kwake. Lakini haki ya mzaliwa wa kwanza ilikuwa ya Yusufu - 3 wana wa Rubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli alikuwa Hanoki, Palu, Hezroni, na Karmi. 4 Uzao wa Yoeli ulikuwa huu: Mwana wa Yoeli alikuwa Shemaia. Mwana wa Shemaia alikuwa Gogi. Mwana wa Gogi alikuwa Shimei. 5 Mwana wa Shimei alikuwa Mika. Mwana wa Mika alikuwa Reaia. Mwana wa Reaia alikuwa Baali. 6 Mwana wa Baali alikuwa Bera, ambaye Tiligathi Pileseri alimpeleka matekani kule Assiria. Bera alikuwa kiongozi katika kabila la Rubeni. 7 Ndugu zake kwa na koo zao, walioandikishwa katika nasaba kwa vizazi vyao: Yeieli kiongozi, Zekaria, 8 na Bela mwana wa Azazi mwana wa Shema mwana wa Yoeli. Waliishi Aroeri, kwa umbali wa Nebo na Baali Meoni, 9 na kuelekea mashariki hadi mwanzo wa jangwa linaloendelea hadi Mto Efarati, kwa sababu mifugo yao ilikuwa imeongezeka katika nchi ya Gileadi. 10 Katika siku za Sauli, kabila la Rubeni lilishambulia Wahagiri na kuwashindaWakaishi ndani ya hema za Wahagiri katika nchi yote mashariki mwa Gileadi. 11 Watu wa kabila la Gadi waliishi karibu nao, katika nchi ya Basha Saleka. 12 Yoeli alikuwa kiongozi wao, Shafamu alikuwa wa pili na Yanai na Shafati walikuwa wa Bashani. 13 Ndugu zao, kwa koo zao, walikuwa Mikaeli, Meshulamu, Sheba, Yorai, Yakani, Sia na Eberi - jumla saba wote. 14 Hawa watu walio tajwa hapo juu ni uzao wa Abihaili, na Abihaili alikuwa mwana wa Huri. Huri alikuwa mwana wa Yaroa. Yaroa alikuwa mwana wa Gileadi. Gileadi alikuwa mwana wa Mikaeli. Mikaeli alikuwa mwana wa Yeshishai. Yeshishai alikuwa mwana wa Yado. Yado alikuwa mwana wa Buzi. 15 Ahi mwana wa Abidieli mwana wa Guni, alikuwa kichwa cha ukoo wao. 16 Waliishi Gileadi, Bashani, katika miji yake, na katika nchi zote za malisho ya Sharoni kwa umbali wa mipaka yake. 17 Hawa wote waliorodheshwa katika nakaka za uzao katika siku za Yothamu mfalme wa Yuda na Yeroboamu mfalme wa Israeli. 18 Warubeni, Wagadi, na nusu ya kabila la Manase walikuwa na wana jeshi 44,760 walio fuzu kwa vita, walio beba ngao na upanga, na waliovuta upinde, ambao wangewezakwenda vitani. 19 Waliwashambulia Wahagiri, Yeturi, Nafishi, na Nodabu. 20 Walipokea msaada wa kiungu dhidi yao. Katika hili Wahagiri na wote walio kuwa nao walishindwa. Hii ni kwa sababu Waisraeli walipaza sauti katika vita, na yeye akawajibu, kwa sababu waliweka tumaini lao kwake. 21 Walikamata wanya wao, pamoja na ngamia elfu hamsini, kondoo 250, 000, punda elfu mbili, na wanaume 100, 000. 22 Kwa sababu Mungu aliwapigania, waliua maadui wengi. Waliishi katika nchi yao mpaka nyakati za kuwekwa utumwani. 23 Wana wa nusu ya kabila la Manase waliishi katika nchi ya Bashani kwa umbali wa Bali Hermoni na Seniri (hiyo ni, Mlima Hermoni). 24 Hawa walikuwa viongozi wa koo zao: Eferi, Ishi, Elieli, Azrieli, Yeremia, Hodavia, na Yahdieli. Walikuwa mashujaa hodari,wanaume mashuhuri, viongozi wa familia zao. 25 Lakini walikuwa sio waaminifu kwa Mungu wa babu zao. Walifanya uzinzi na miungu ya watu wa hiyo nchi, ambao Mungu aliwaangamiza mbele yao. 26 Mungu wa Israeli akamchochea Puli mfalme wa Assiria ( ambaye pia uitwa Tiligathi Pileseri, mfalme wa Assiria). Aliwapeleka matekani Warubeni, Wagadi, na nusu ya kabila la Manase. Aliwaleta kwa Hala, Habori, Hara, na kwenye mto wa Gozani, ambapo wapo hadi leo.