1 Uzao wa Yuda ulikuwa Peresi, Hesroni, Karmi, Huri, na Shobali. 2 Reaya, mwana wa Shobali alikuwa baba waYahathi. Yahathi alikuwa baba wa Ahumai na Lahadi. Hawa walikuwawa koo za Wasorathi. 3 Hawa walikuwa wana wa Etamu: Yezreeli, Ishma, na Idbashi. Dada yao alikuwa Haselelponi. 4 Penueli alikuwa mwanzilish wa Gedori. Ezeri alikuwa mwanzilishi wa Husha. Hawa walikuwa uzao wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrathi, na muanzilishi wa Bethelehemu. 5 Ashuri baba wa Tekoa alikuwa na wake wawili, Hela na Naara. 6 Naara alimzalia Ahuzamu, Heferi, Temeni na Ahashtari. Hawa walikua wana wa Naara. 7 Wana wa Hela walikua Serethi, Sohari, Ethnani, 8 na Kozi, aliyekua baba wa Anubu na Hasobeba, na koo zilizotoka kwa Aharheli mwana wa Harumu. 9 Yabesi aliheshimika zaidi ya kaka zake. Mama yake alimuita Yabesi. Alisema, "Kwa sababu nimemzaa katika uchungu 10 Yabesi akamuita Mungu wa Israeli na kusema, "Laiti ungenibanibariki kweli, upanue eneo langu, na mkono wako ukuwe jpamoja nami. Ukifanya hivi utaniepusha na madhara, ili kwamba niwe huru na huzuni!" Kwa hivyo Mungu akamjalia maombi yake. 11 Kelubu kaka wa Shuha akawa baba wa Mehiri, aliyekuwa baba wa Eshtoni. 12 Eshtoni akawa baba wa Beth-Rafa, Pasea, na Tehina, ambaye alianzisha mji wa Iri Nahashi. Hawa ni wanaume walioishi Reka. 13 Wana wa Kenazi walikua Othinieli na Seraia. Wana wa Othinieli walikuwa Hathathi na Meonothai. 14 Meonothai akawa baba wa Ofara, na Seraia akawa baba wa Yohabu, mwanzilishi wa Ge Harashimu, ambao watu wake walikua wahunzi. 15 Wana wa Kalebu mwana wa Yefune walikua Iru, Ela na Namu. Mwana wa Ela alikua Kenazi. 16 Wana wa Yehaleli walikua Zifi, Zifa, Tiriya, na Azareli. 17 Wana wa Ezra walikua Yetheri, Meredi, Eferi, na Yaloni. 18 Mke wake Meredi wa Kimisri alishika mimba na kuwazaa Miriamu, Shamai, na Ishiba, aliyekua baba wa Eshitemoa. Hawa walikua wana wa Bithia, binti wa Farao, ambaye Meredi alimuoa. Mke wa Kiyahudi wa Meredi alimzaa Yeredi ambaye alikua baba wa Gedore; Heberi, aliyekua baba wa Soko; na Yekuthieli aliyekua baba wa Zanoa. 19 Kati ya wana wawili wa mke wa Hodia, dadake Nahamu, mmoja wao akawa baba wa Keila Mgarimi. Mwingine alikua Eshitemoa Mmakathi 20 Wana wa Shimoni walikua Amnoni, Rina, Beni Hanani, na Tiloni. Uzao wa Ishi walikua Zohethi na Beni-Zohethi. 21 Uzao wa Shela mwana wa Yuda, ulikua ni Eri baba wa Leka, Laada baba wa Maresha na koo za wafanyakazi wa kushona kule Beth Ashbea, 22 Yoakimu, wanaume wa Kozeba, na Yoashi na Sarafi, aliyekuwa na mamlaka huko Moabu na Yashubi Lehemu. Maelezo haya yametoka kwenye nakala za zamani.) 23 hawa walikuwa ni wafinyanzi walioishi Netaimu na Gedera na kufanya kazi kwaMfalme. 24 Uzao wa Simeoni ulikua Nemueli, Yamini, Yaribu, Zera, na Shauli. 25 Shalumu alikua mwana wa Shauli, Mibisamu alikua mwana wa Shalumu, na Mishima alikua mwana wa Mibisamu. 26 Ukoo wa Mishima ulikua Hamueli mwana wake, Zakuri mjukuu wake, na Shimei kitukuu chake. 27 Shimei alikua na wana kumi na sita na mabinti sita. Kaka zake hawakuwa na watoto wengi, Kwa hiyo koo zao hazikuongezeka sana kwa kama watu wa Yuda walivyoongezeka. 28 Waliishi Beasheba, Molada, na Hazari Shuali. 29 Pia waliishi Bilha, Ezemu, Toladi, 30 Bethueli, Horma, Zikilagi, 31 Bethi Markabothi, Hazari Susimi, Bethi Biri, na Shaaraimu. Hii ilikua miji yao mpaka wakati wa utawala wa Daudi. 32 Vijiji vyao vitano vilikua Etamu, Aini, Rimoni, Tokeni na Ashani, 33 pamoja na vijiji vya kando mpaka Balith Haya yalikua makazi yao, na walitunza kumbukumbu za uzao wao. 34 Viongozi wa ukoo walikua Meshobabu, Yamileki, Yoshahi mwana wa Amazia, 35 Yoeli, Yehu mwana wa Yoshibia mwana wa Seraia mwana wa Asieli, 36 Elioenai, Yaakoba, Yeshohaia, Asaia, Adieli, Yesimieli, Benaia, 37 na Ziza mwana wa Shifi mwana wa Aloni mwana wa Yedaia mwana wa Shimiri mwana wa Shemaia. 38 Hawa walio orodheshwa kwa majina walikua viongozi wa koo zao, na koo zao ziliongezeka sana. 39 Walienda karibu na Gedori, upande wa mashariki wa bonde, kutafuta malisho ya mifugo yao. 40 Walipata malisho mengi na mazuri. Nchi ilikua tambarare, tulivu na ya amani. Wahamu waliishi hapo awali. 41 Hao walio orodheshwa hapo kwa majina walikuja katika siku za Hezekia mfalme wa Yuda, na wakashambulia makazi ya Wahamu na Wameuni, ambao pia walikua hapo. Waliwaangamiza kabisa na kuishi hapo sababu walipata malisho kwa ajili ya mifugo yao. 42 Wanaume mia tano wa kabila la Simeoni walienda katika mlima Seiri, pamoja na Pelatia, Nearia, Refaia, na Uzieli, wana wa Ishi, kama kiongozi wao. 43 Waliwashinda wakimbizi wa Waamaleki waliobakia, na wakaishi hapo hadi siku hii.