Sura 19

1 Ilikuja baadaye kwamba Nahashi, mfalme wa watu wa Amoni, akafa, na mwanae akawa mfalme baada yake. 2 Daudi akasema, "Nitaonyesha ukarimu kwa Hanuni mwana wa Nahashi, kwa sababu baba yake alionyesha ukarimu kwangu." Hivyo Daudi akatuma wajumbe kumfariji kuhusu baba yake. Watumishi wa Daudi wakaingia nchi ya Waamoni na wakaenda kwa Hanuni, ilikumfariji. 3 Lakini wakuu wa Waamoni wakamwambia Hanuni, "Unadhani Daudi anamheshimu baba yako sababu ametuma watu kukufaraji? Watumishi wake hawaji kwako ili kuipeleleza na kuichunguza nchi ili waipindue? 4 Hivyo Hanuni akawakamata watumishi wa Daudi, akawanyoa, akakata nguo zao katikati kwenye matako na kuwafukuza. 5 Walipo eleza haya kwa Daudi, alienda kukutana nao, kwa maana watu hao waliona aibu sana. Mfalme akasema, "Bakini Yeriko hadi ndevu zenu ziote tena, kisha mrudi." 6 Wakati Waamoni waliona wamekuwa uvundo kwa Daudi, Hanuni na Waamoni walituma talanta elfu moja za fedha kukodisha magari ya farasi kwa Waaremei na wanaume wa farasi kutoka Naharaimu, Maka, na Zoba. 7 Waliwakodishia magari ya farasi elfu thelathini na mbili pamoja na mfalme wa Maka na jeshi lake, walio kuja na kueka kambi mbele ya Medeba. Kisha Waamoni wakajikusanya pamoja kutoka miji yao, na wakaja kwa vita. 8 Wakati Daudi aliposikia, alimtuma Yoabu na jeshi lake lote la mashujaa. 9 Watu wa Amoni walikuja na kupanga mstari kwa ajili ya pambano katika lango la mji, nao wafalme waliokuja walikuwa peke yao katika shamba. 10 Wakati Yoabu alipoona mistari ya pambano imemzunguka mbele na nyuma, alichagua wapiganaji bora wa Israeli na kuwapanga dhidi ya Waaremi. 11 Na jeshi lingine aliliweka chini ya Abishai kaka yake, akawapanga kwa mstari ya pambano dhidi jeshi la Amoni. 12 Yoabu akasema, "Kama Waaremi wananguvu kunishinda, basi wewe, Abishai, lazima uniokoe. Lakini kama jeshi la Waamoni lina nguvu kukuzidi, basi nitakuja kukuokoa. 13 Kuwa hodari na tujionyeshe kuwa hodari kwa ajili ya watu wetu na kwa ajili ya miji ya Mungu wetu, kwa kuwa Yahweh atafanya lililo jema machoni mwake." 14 Hivyo Yoabu na askari wa jeshi lake wakasogea kwenye pambano dhidi ya Waaremi, walio lazimika kukimbia mbele ya jeshi la Waisraeli. 15 Wakati jeshi la Waamoni lilipoona kuwa Waaremi wamekimbia, nao pia wakamkimbia Abishai, ye Yoabu, na wakakurudi mjini. Kisha Yoabu akarudi kutoka kwa watu wa Amoni na kurudi Yerusalemu. 16 Waaremi walipoona kwamba wameshindwa na Waisraeli, wakatuma wajumbe na kuwarudisha Waaremi kutoka ng'ambo ya Mto Frati, na Shofaki mkuu wajeshi la Hadadezeri. 17 Daudi alipo ambiwa haya, akakusanya Israeli yote, akuvuka Yordani, na kuja juu yao. Alipanga jeshi kwa ajili ya pambano dhidi ya Waaremi, na wakapigana nao. 18 Waaremi waliwakimbia Waisraeli, na Daudi akaua waendesha magari ya farasi ya Waaremi elfu saba na wanajeshi wa miguu elfu arobaini. Pia alimuua Shopaki, mkuu wa jeshi. 19 Wafalme wote walio kuwa watumishi wa Hadadezeri walipoona kuwa wameshindwa na Israeli, walifanya amani na Daudi na kumtumikia. Hivyo watu wa Aramu hawakuwa tayari kuwasaidia Waamoni.