Sura 12

1 Hawa walikuwa wanaume walio kuja kwa Daudi huko Zikilagi, wakati akiwa bado amefukuzwa katika uwepo wa Sauli mwana wa Kishi. Walikuwa miongoni mwa wanajeshi, wasaidizi wake katika mapambano. 2 Walikuwa wana upinde na waliweza kutumia mkono wa kuume na wakushoto kurusha mawe na manati na kupiga mishale kutoka kwenye upinde. Walikuwa Wabenjamini, jamaa wa Sauli. 3 Kiongozi alikuwa Ahi Eza, halafu Yoashi, Wana wote wa Shemaa Mgibeathi. Kulikuwa na Yezieli na Peleti, wana wa Azimavethi. Kulikuwa pia na Beraka, Yehu Waanathothi, 4 Ishimaia Mgibeoni, mwanajeshi kati ya wale thelathini ( na kiongozi wa wale thelathini); Yeremia, Yahazieli, Yohanani, Yozabadi Mgederathi 5 Eluzai, Yerimothi, Bealia, Shemaria, Shefatia Mharufi, 6 Wakorahi ni Elkana, Ishia, Azareli, Yoeza, Yashobeamu, na 7 Yoela na Zebadia, wana wa Yeroham wa Gedori. 8 Baadhi ya Wagadi walijiunga na Daudi katika ngome iliyo nyikani. Walikuwa mashujaa hodari, wanaume wa vita, tayari kwa vita, walioweza kumudu ngao na mkuki; ambao nyuso zao zilikuwa kali kama za simba. Walikuwa wepesikama swala juu ya milima. 9 Kulikuwa na Eza kiongozi, Obadia wapili, Eliabu watatu, 10 Mishimana wanne, Yeremia watano, 11 Atai wasita, Elieli wasaba, 12 Yohanani wanane, Elizabadi watisa, 13 Yeremia wakumi, Makibanai wakumi na moja. 14 Wana wa Gadi walikuwa viongozi wa jeshi. Wamwisho aliongoza mia moja, na mkubwa aliongoza elfu moja. 15 Walivuka Yordani mwezi wa kwanza, ilipofurika kingo zake, na kuwafanya wote wanaoishi katika mabonde kukimbia, kuelekea mashariki na kuelekea magharibi. 16 Baadhi ya wanaume wa Benjamini na Yuda walikuja kwenye ngome kwa Daudi. 17 Daudi alienda nje kuwasalimu na kuwahutubia: "kama mmekuja kwa amani kunisaidia, moyo wangu utaungana nanyi Lakini kama mmekuja kunisaliti kwa maadui zangu, Mungu wa mababu zetu awaone na kuwakemea, kwa kuwa sijakosa." 18 Kisha roho ikaja juu ya Amasai, ambaye alikuwa kiongozi wa wale thelathini. Amasai alisema, "Sisi ni wako, Daudi. Sisi tupo upande wako, mwana wa Yesse. na amani iwe juu ya yeyote atakaye kusaidia. Amani na iwe wanaokusaidia, kwa kuwa Mungu wako anakusaidia." Kisha Daudi akawapokea na kuwafanya wakuu wa watu wake. 19 Baadhi kutoka kwa Manase pia wakamwendea Daudi alipokuja na Wafilisti dhidi ya Sauli katika pambano. Lakini hawakuwasaidia Wafilisti kwasababu mabwana wa Wafilisti walishauriana na wakamfukuza Daudi. Walisema, "Atamwendea Bwana wake Sauli na kuhatarisha maisha yetu." 20 Alipokwenda kwa Zikilagi, wanaume wa Manase walioungana nae walikuwa Adina, Yozabadi,Yediaeli, Yozabadi, Elihu, na Zilethai, viongozi wa maelfu wa Manase. 21 Walimsaidia Daudi kupigana na kikundi cha wezi, maana walikuwa wanaume wa mapambano. Baadae walikuwa wakuu katika jeshi. 22 Siku hadi siku, wanaume walikuja kwa Daudi kumsaidia, mpaka wakawa jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu. 23 Hii ni kumbukumbu ya wanajeshi wa vita, walio kuja kwa Daudi Hebroni, kuupindua ufalme wa Sauli kwake, ilikutimiza neno la Yahweh. 24 Waanume wa Yuda walio beba ngao na mkuki ni 6, 800, tayari kwa vita. 25 Kutoka kwa Wasimeoni walikuwa 7, 100 mashujaa hodari waliofunzwa vita. 26 Kutoka kwa Walawi kulikuwa na wanaume wa mapambano 4, 600. 27 Yehoiada alikuwa kiongozi wa uzao wa Aruni, na kwa yeye walikuwa 3, 700. 28 Pamoja na Zadok, kijana mmoja, shujaa wa vita, walikuwa viongozi ishirini na mbili kutoka ukoo wake 29 Kutoka kwa Benjamini, jamaa ya Sauli, walikuwa elfu tatu. Wengi wao walikuwa wameilinda nyumba ya Sauli mpaka wakati huu. 30 Kutoka kwa Waefraimu palikuwa na mashujaa wa vita 20, 800, wanaume maarufu kwenye koo zao. 31 Kutoka kabila nusu la Manase palikuwa na wanaume elfu kumi na nane maarufu walio kuja kufanya Daudi mfalme. 32 Kutoka kwa Isakari, palikuwa na viongozi mia mbili waliokuwa na ufahamu wa nyakati na walijua kile ambacho Israeli walipaswa kufanya. Ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao. 33 Kutoka Zebuloni palikuwa na wanaume elfu hamsini wa mapambano, tayari kwa vita, na silaha zote za vita, na tayari kutoa uwaminifu usiogawanyika. 34 Kutoka kwa Naftali palikuwa na askari elfu moja, na pamoja nao wanaume elfu thelathini na saba wenye ngao na mikuki. 35 Kutoka kwa Wadani palikuwa na wanaume 28, 600 wameandaliwa kwa ajili ya pambano. 36 Kutoka kwa Asheri palikuwa na wanaume elfu arobaini wameandaliwa kwa pambano. 37 Kutoka upande wa pili wa Yordani, kutoka kwa Warubeni, Wagadi, na nusu kabila la Manase, palikuwa na wanaume 120, 000 wameandaliwa na silaha za kila namna kwa ajili ya pambano. 38 Hawa wanajeshi wote, waliandaliwa kwa pambano, walikuja Hebroni na moyo wote ili kumfanya Daudi awe mfalme juu ya Israeli yote. Waisraeli wote waliosalia walikubali kumfanya Daudi mfalme pia. 39 Walikuwa pale na Daudi siku tatu, wakila na kunywa, kwa kuwa jamaa zao waliwapa mahitaji ya kwenda nayo. 40 Kwa kuongezea, wao walio kuwa karibu nao, kwa umbali wa Isakari na Zebuloni na Naftali, walileta mkate kwa punda, ngamia, nyumbu na fahali, na keki za tini, mvinyo, vishada vya zabibu kavu, divai, mafuta, ng'ombe na kondoo, kwa maana kulikwa na furaha katika Israeli