1 Kisha Waisraeli wote walikuja Hebroni kwa Daudi na kusema, "Angalia, sisi ni nyama na mifupa yako. 2 Katika wakati uliopita, Sauli alipoo kuwa mfalme juu yetu, ni wewe uliye ongoza jeshi la Israeli. Yahweh Mungu wako alisema kwako, 'utawachunga watu wangu wa Isaraeli, na utakuwa mtawala wa watu wangu wa Israeli"'. 3 Kwaiyo wazee wote wa Israeli wakamjia mfalme huko Hebroni, na Daudi akafanya agano nao mbele ya Yahweh. Wakampaka mafuta Daudi kuwa mfalme wa Israeli. Kwa namna hii, neno la Yahweh lilo nenwa na Samweli likawa kweli. 4 Daudi na Israeli yote wakaenda Yerusalemu (yani, Yebusi). Sasa Wayebusi, wakazi wa nchi, walikuwa pale. 5 Wakazi wa yebusi wakamwabia Daudi, "Hautakuja humu." Lakini Daudi alichukuwa ngome ya Sayuni, mji wa Daudi. 6 Daudi alikuwa amesema, "Yeyote atakaye washambulia Wayebusi akiwa wa kwanza atakuwa mkuu na komanda wa jeshi." Kwaiyo Yoabu mwana wa Zeruia akashambulia wa kwanza, hivyo akafanywa mkuu wa jeshi. 7 Kisha Daudi akaanza kuishi katika ngome. Kwaiyo wakaiita mji wa Daudi. 8 Akaimarisha mji kutoka Milo na hadi mpaka ukuta unao zunguka. Yoabu akaimairisha mji wote uliyo baki. 9 Daudi akawa mkuu na mkuu kwa sababu Yahweh wa Majeshi alikuwa naye. 10 Hawa walikuwa viongozi Daudi aliyo kuwa nao, waliyo jionyesha imara katika ufalme wake, pamoja na Israeli, kumfanya mfalme, kutii neno la Yahweh kuhusu Israeli. 11 Hii ni orodha ya wanajeshi shupavu wa Daudi. Yashobeami, mwana wa Mhakimoni, alikuwa mkuu wa kikosi cha thelathini. Aliwaua wanaume mia tatu na mkuki wake katika sehemu moja. 12 Baada ya yeye alikuwa Eleazari mwana wa Dodo, Mahohi, aliyekuwa mmoja wa wanaume watatu hodari. 13 Alikuwa na Daudi huko Pasidamimu, na pale Wafilisti wakakusanyika pamoja kwa mapambano, ambapo palikuwa na uwanja wa ngano na jeshi liliwakimbia Wafilisti. 14 Walisimama katikati ya uwanja. Wakautetea na kuwakata Wafilisti na Yahweh akawaokoa na ushindi mkubwa. 15 Kisha watatu wa viongozi thelathini wakashuka chini kwenye mwamba wa Daudi, katika pango la Adulamu. Jeshi la Wafilisti walieka kambi katika bonde la Refaim. 16 Kwa wakati huo Daudi alikuwa katika ngome yake, pangoni, Wafilisti walikita kambi yao Bethilehemu. 17 Daudi alikuwa na kiu ya maji na akasema, "Laiti mtu akanipatia maji ya kunywa kutoka kisima kilicho Bethilehemu, kisima kilicho pembeni mwa lango!" 18 Hawa wanaume hodari watatu wakatoboa kupita jeshi la Wafilisti na kuchota maji kwenye kisima cha Bethilehemu, kisima pembeni mwa lango. Wakachukuwa maji na kumletea Daudi, lakini alikataa kunywa. Badala yake, akamwaga chini kwa Yahweh. 19 Kisha akasema, "Iwe mbali mbele ya Mungu kwamba nifanye hivi Je ninywe damu ya wanaume hawa walio hatarisha maisha yao?" Kwa sababu waliyaweka maisha ya hatarini, Daudi akakataa kuyanywa. Haya ni matendo ya wale mashujaa 20 Abishai kaka wa Yoabu, alikuwa kiongozi wa wale watatu. Aliwahi kutumia mkuki wake dhidi ya watu mia tatu na kuwaua. Ametajwa pamoja na wale watatu. 21 Kati ya wale watatu, yeye alipewa heshima mara mbili na akawa kiongozi wao, ijapo hakuwa mmoja wa miongoni mwao. 22 Benaia mwana wa Yehoiada alikuwa shujaa jasiri kutoka Kabizeli, aliye fanya matendo makuu. Aliua wana wawili wakiume wa Arieli wa Moabu. Pia alishuka chini ya shimo na kumuua simba wakati theluji ilikuwa ikianguka. 23 Hata alimuua Mmisri, mwanaume mwenye mita mbili na theluthi moja. Mmisri alikuwa na mkuki kama gongo la mshonaji, lakini alimfuata chini na fimbo tu.Akakamata mkuki katika mkono wa Mmisri na kumuua na mkuki wake. 24 Benaia mwana wa Yehoiada alifanya haya matukio, na akatajwa miongoni mwa wale wanaume hodari watatu. 25 Alisifika zaidi ya wale wanajeshi thelathini kwa ujumla, lakini hakuwa pewa hadhi ya wale wanajeshi watatu hodari. Lakini Daudi alimweka juu ya walinzi wake. 26 Mashujaa hodari walikuwa Asaheli kaka wa Yoabu, Elhanani mwana wa Dodo wa Bethilehemu, 27 Shamothi Mherori, Helezi Mpeloni, 28 Ira mwana wa Ikeshi Mtekoi, Abieza Manathothi, 29 Sibekai Mhushathite, Ilai Mahohi, 30 Maharai Mnetofathi, Heledi mwana wa Baana Mnetofathite, 31 Itai mwana wa Ribai wa Gibea uzao wa Benjamini, Benaia Mpirathoni, 32 Hurai wa mabonde ya Gaashi, Abieli Marbathi, 33 Azmavethi Mbaharumi, Eliaba Mshaalboni, 34 wana wa Hashemu Mgizoni, Yonathani mwana wa Shagee Mharari, 35 Ahiamu mwana wa Sakari Mharari, Elifali mwana wa Uri, 36 Hefa Mmekarathi, Ahija Mpeloni, 37 Hezro Mkarimeli, Naarai mwana wa Ezibai, 38 Yoeli kaka wa Nathani, Mibhari mwana wa Hagiri, 39 Zeleki Mamoni, Naharai Mberothi ( mbeba ngao ya Yoabu mwana wa Zeruia), 40 Ira Mithire, Garebu Mithire, 41 Uria Mhiti, Zabadi mwana wa Ahlai, 42 Adina mwana wa Shiza Mreubeni ( kiongozi wa Wareubeni) na thelathini pamoja naye, 43 Hanani mwana wa Maaka, na Yoshafati Mmithini, 44 Uzia Mashiterathi, Shama na Yeieli wana wa Hothamu Waaroeri, 45 Jediaeli mwana wa Shimri, Joha ( kaka yake Mtize), 46 Elieli Mmahavi, Yeribai na Yoshavia wana wa Elnaamu, Ithima Mmoabi, 47 Elieli, Obedi, na Yaasieli mmezobai.