Genesis 40

Genesis 40:1

Kwa nini mfalme aliwaweka mnyweshaji na mwokaji wake gerezani?

Aliwaweka gerezani kwa sababu walimkasirisha.

Genesis 40:4

Nini kilitokea kwa mnyweshaji na mwokaji usiku huo huo?

Mnyweshaji na mwokaji kila mmoja aliota ndoto usiku huo huo.

Genesis 40:6

Kwa nini mnyweshaji na mwokaji wote wawili walikuwa na huzuni asubuhi iliyofuata?

Wote wawili walikuwa na huzuni kwa sababu hakuna aliyeweza kutafsiri ndoto zao.

Yusufu alisema ni nani aliyeweza kutoa tafsiri ya ndoto zile?

Yusufu alisema ya kwamba Mungu angeweza kutoa tafsiri ya ndoto zile.

Genesis 40:12

Yusufu alisema tafsiri ya mnyweshaji ilikuwa ni nini?

Yusufu alisema ya kwamba ndoto ilimaanisha kuwa ndani ya siku tatu Farao atarejesha mnyweshaji katika shughuli yake.

Genesis 40:14

Yusufu alitoa ombi gani kwa mnyweshaji baada ya kutoa tafsiri ya ndoto yake?

Yusufu aliomba ya kwamba mnyweshaji amkumbuke, na kumtaja kwa Farao, na kumtoa nje ya gereza.

Genesis 40:18

Yusufu alisema tafsiri ya mwokaji ilikuwa ni nini?

Yusufu alisema ya kwamba ndoto ilimaanisha katika siku tatu Farao atamtundika mwokaji juu ya mti.

Genesis 40:20

Tukio gani muhimu lilitokea siku tatu baadae?

Siku ya kuzaliwa ya Farao ilikuwa siku tatu baadae.

Farao alifanya nini kwa mnyweshaji na mwokaji katika siku hiyo?

Farao alimrejesha mnyweshaji, lakini alimtundika mwokaji, kama Yusufu alivyotafsiri kwao.

Je mnyweshaji alikumbuka ombi la Yusufu kwake?

Hapana, mnyweshaji hakukumbuka kumsaidia Yusufu, lakini alimsahau.