Genesis 34

Genesis 34:1

Shekemu, mwana wa Hamori, alifanya nini alipomuona Dina, binti wa Lea?

Shekemu alimkamata Dina, akamshambulia, na kumbaka.

Genesis 34:4

Yakobo alifanya nini awali aliposikia kuhusu kilichotokea kwa Dina?

Yakobo alijizuia kwanza hadi pale wanawe waliporudi kutoka shambani.

Genesis 34:6

Wana wa Yakobo waliitikiaje waliposikia kile alichofanya Shekemu kwa Dina?

Wana wa Yakobo walipatwa na hasira sana.

Genesis 34:8

Hamori, baba wa Shekemu, alimtaka Yakobo kufanya nini?

Hamori alimtaka Yakobo kumpatia Dina kuwa mke wa Shekemu, na kuruhusu familia ya Yakobo kuoana na familia ya Hamori.

Genesis 34:11

Shekemu alisema yupo tayari kufanya nini ili awe na Dina kama mke wake?

Shekemu alisema angelipa mahari kubwa ambayo Yakobo angetaja.

Ni kwa namna gani wana wa Yakobo walimjibu Shekemu, na kwa nini?

Wana wa Yakobo walimjibu Shekemu kwa udanganyifu, kwa sababu Shekemu alimnajisi Dina.

Genesis 34:14

Wana wa Yakobo walitaja mahitaji gani kwa Hamori kabla ya kukubali kuoana na familia ya Hamori?

Wana wa Yakobo walihitaji ya kwamba wanamume wote wa familia ya Hamori watahiriwe.

Genesis 34:22

Hamori na Shekemu walisema nini kingekuwa chao iwapo wataoana na familia ya Yakobo, walipokuwa wakizungumza na wanamume wa mji wao?

Walisema ya kwamba mifugo, mali, na wanyama wote wa Yakobo vitakuwa vyao iwapo wataoana na familia ya Yakobo.

Genesis 34:24

Wanamume wa mji wa Hamori walijibuje walipoulizwa kama walikuwa tayari kutahiriwa?

Wanamume wa mji wa Hamori walimsikiliza hamori na Shekemu na kila mwanamume alitahiriwa.

Simoni na Lawi walifanya nini katika siku ya tatu baada ya wanamume wa familia ya Hamori kuwa wametahiriwa?

Simoni na Lawi waliwaua wanamume wote katika mji wa Hamori.

Genesis 34:27

Wana wote wa Yakobo walifanya nini?

Wana wote wa Yakobo walipora mji, wakachukua utajiri wote, na kukamata watoto na wake.

Genesis 34:30

Yakobo aliitikiaje alipojua kuhusu kile walichofanya Simoni na Lawi?

Yakobo alisema ya kwamba Simoni na Lawi wameleta shida juu yake kwa sababu wakazi wa nchi ile wanaweza kumuangamiza yeye na nyumba yake.

Kwa nini Simoni na Lawi walisema walifanya vile?

Simoni na Lawi walisema walifanya vile kwa sababu Shekemu alimtendea dada yao Dina kama kahaba.