Genesis 27

Genesis 27:1

Isaka alishindwa kufanya nini tena alipozeeka?

Isaka alipozeeka, hakuweza kuona tena.

Genesis 27:3

Isaka alimwomba Esau kufanya nini na kwa nini?

Isaka alimuomba Esau kwenda kuwinda na kumtengenezea aina ya chakula ambayo anaipenda, ili kwamba aweze kula na kumbariki Esau.

Genesis 27:8

Mpango wa Rebeka wa kuandaa chakula kwa ajili ya Isaka ulikuwa upi, na kwa nini?

Rebeka alimwambia Yakobo kuchukua mbuzi wawili na angetengeneza chakula ambacho Isaka alikipenda, ili kwamba Yakobo ampelekee Isaka na kupokea ile baraka.

Genesis 27:11

Yakobo alijishughulisha na nini katika kuleta chakula kwa Isaka?

Yakobo alijishughulisha ya kwamba Esau alikuwa mtu mwenye nywele na yeye alikuwa mtu laini, na kwamba Isaka angemgusa na kugundua ya kuwa Yakobo alikuwa mdanganyifu na angemlaani.

Genesis 27:15

Rebeka alitatuaje tatizo la Esau kuwa mtu wa nywele nyingi, na Yakobo kuwa mtu laini?

Rebeka alimpatia Yakobo nguo za Esau na kumvisha ngozi ya mbuzi juu ya mikono na shingo yake.

Genesis 27:20

Isaka alipouliza, Yakobo alisemaje ya kwamba amepata windo kwa haraka hivyo?

Yakobo alisema ya kwamba Yahwe, Mungu wa Isaka, alileta windo kwake.

Genesis 27:22

Kwa sababu hakuwa na uhakika, Isaka alijaribuje kuthibitisha ni nani aliyekuwa akimpatia chakula?

Isaka alimgusa Yakobo mkononi na kuhisi manyoya ya ngozi ya mbuzi.

Genesis 27:24

Yakobo alisema nini Isaka aliposema, "Wewe kweli ni mwanangu Esau?"

Yakobo alisema, "Ni mimi"

Genesis 27:26

Jambo gani mwishowe lilimshawishi Isaka ya kwamba mtu anayeleta chakula alikuwa Esau?

Yakobo alipomkaribia Isaka kumbusu, Isaka alinusa nguo za Esau.

Genesis 27:29

Isaka alisema ni nani angeinama chini kwa Yakobo?

Isaka alisema mataifa yangeinama chini kwa Yakobo na kwamba mwana wa mama wa Yakobo atainama chini kwake.

Genesis 27:30

Esau alifanya nini baada ya Yakobo kuondoka katika hema la Isaka?

Esau alirudi kutoka mawindoni, akaandaa chakula, na kukileta kwa Isaka.

Genesis 27:34

Isaka alisema nini Esau alipomuomba Isaka baraka yake?

Isaka alisema ya kwamba Yakobo amechukua baraka ya Esau kwa udanganyifu.

Genesis 27:36

Ni kwa njia gani mbili Esau alisema Yakobo amemdanganya?

Esau alisema ya kwamba Yakobo alimdanganya kwa haki yake ya kuzaliwa na baraka yake.

Genesis 27:39

Ni "baraka" gani ambayo Isaka alimpatia Esau?

Isaka alisema ya kwamba Esau ataishi mbali na utajiri wa nchi, ya kuwa atamtumikia ndugu yake, lakini hatimaye atapambana naye na kuondoa nira ya Yakobo juu yake.

Genesis 27:41

Esau aliamua kufanya nini baada ya kifo cha Isaka?

Esau aliamua kumuua Yakobo baada ya kifo cha Isaka.

Genesis 27:43

Rebeka alifanya nini baada ya kusikia mipango ya Esau?

Rebeka alimtuma Yakobo kwa Labani, kaka yake, Harani.