Mungu alimwambia Nuhu na wanawe kuzaana, kuongezeka na kujaza nchi.
Mungu alimpatia Nuhu na wanawe wote mimea ya kijani na kila kitu chenye uhai kama chakula.
Mungu aliamuru ya kwamba nyama isiliwe na damu ndani mwake.
Mungu alisema ya kwamba kulikuwa na uhai ndani ya damu.
Mungu alitamka ya kwamba yule atakayemwaga damu ya mtu atalazimika kumwaga damu yake.
Mungu alimfanya mwanamume katika mfano wa Mungu.
Mungu aliweka upinde wa mvua katika mawingu kama ishara ya agano alilofanya pamoja na nchi.
Mungu alifanya agano la ahadi ya kwamba kila chenye mwili hatakiangamiza kwa gharika tena.
Majina ya wana watatu wa Nuhu yalikuwa ni Shemu, Hamu, na Yafethi.
Baada ya kupanda mizabibu, Nuhu alikunywa sehemu ya divai na akalewa.
Shemu na Yafethi walitembea kinyumenyume na kanzu, huku wakiwa wametazama upande mwingine, ili kufunika uchi wa baba yao.
Nuhu alimlaani Hamu na kusema, "Alaaniwe Kanaani. Na awe mtumishi kwa watumishi wa ndugu zake"
Nuhu aliwabariki wote Shemu na Yafethi.