Genesis 3

Genesis 3:1

Sasa

Mwandishi anaanza sehemu mpya ya simulizi.

mwerevu kuliko

"mjanja zaidi" au "mwenye akili ya kupata kile atakacho kwa kusema uongo"

Je ni kweli Mungu amesema, 'Msile ... bustanini?

Nyoka anajifanya kushangazwa ya kwamba Mungu alitoa sheria hii. Swali hili la balagha laweza kutafsiriwa kama kauli. "Nashangaa ya kwamba Mungu, "Msile ... bustanini."

Msile

Neno "msile" ni wingi na linamaasha mwanamume na mwanamke

Twaweza kula ... Mungu amesema, 'msile'

Hawa alimwambia nyoka ambacho Mungu aliwaruhusu kufanya kwanza na kisha kile Mungu alichowazuia kufanya. Baadhi ya lugha zingesema kile walichozuiwa kufanya kwanza na kisha kusema kile walichoruhusiwa kufanya.

Twaweza kula

"Tunaruhusiwa kula" au "Tunayo ruhusa ya kula"

Msile ... wala ... mtakufa

Neno "msile" ni wingi na linamaasha mwanamume na mwanamke

Msile

"Hampaswi kula" au "Msile"

msiuguse

"na hampaswi kuigusa" au "na msiuguse"

Genesis 3:4

Wewe ... yenu ... hamtakufa

Maneno haya yanamaanisha mwanamume na mwanamke na kwa hiyo yako katika matumizi mawili au wingi.

macho yenu yatafumbuliwa

"macho yenu yatafumbuliwa." Lugha hii ina maana "utakuwa na utambuzi wa mambo." Maana hii yaweza kutajwa wazi. "Itakuwa kana kwamba macho yenu yamefumbuliwa"

mkijua mema na mabaya

Hapa "mema na mabaya" ni msemo ambao unalenga maana zote mbili kabisa na kila kitu katikati. "kujua kila kitu, ikiwemo mema na mabaya"

na kuwa unapendeza macho

"mti ulipendeza kutazama" au"ulikuwa mzuri kuangalia" au "au ulikuwa mzuri sana"

na kwamba mti ulitamanika kwa kumfanya mtu awe mwerevu

"naye alitaka matunda ya mti kwa sababu ingeweza kumfanya mtu awe mwerevu" au "naye alitaka matunda yake kwa sababu yangemfanya kuelewa kipi kizuri na kibaya kama vile Mungu afanyavyo.

Genesis 3:7

Macho ya wote wawili yalifumbuliwa

"Kisha macho yao yakafumbuliwa" au "Wakapata ufahamu" au "Wakaelewa"

Wakashona

"wakakaza" au"wakaunganisha"

majani ya miti

Iwapo watu hawajui majani ya miti yakoje, hii yaweza kutafsiriwa kama "majani makubwa ya mti" au kwa wepesi "majani makubwa"

na wakatengeneza vya kujifunika kwa ajili wao wenyewe

Walifanya hivi kwa sababu walikuwa na aibu. Taarifa hii inayojitokea yaweza kufanywa dhahiri kama itahitajika. "na wakajivika navyo kwa sababu walikuwa na aibu"

majira ya kupoa kwa jua

"katika kipindi hicho cha siku ambapo hewa tulivu huvuma"

kutoka kwa uwepo wa Yahwe Mungu

"kuepuka uwepo wa Yahwe Mungu" au "ili kwamba Yahwe Mungu asiweze kuwaona" au "kutoka kwa Yahwe Mungu"

Genesis 3:9

uko wapi?

"Kwa nini unajaribu kujificha kwangu?" Mungu alijua mwanamume alikuwa wapi. Mwanamume alipojibu, hakusema yupo wapi bali alisema kwa nini amejificha.

"uko"

Katika mstari wa 9 na 11, Mungu alikuwa akizungumza na mwanamume.

nilikusikia

"Nilisikia sauti uliyokuwa unaifanya"

Ni nani alikwambia

Mungu alijua jibu la swali hili. Aliuliza ili kumlazimisha Adamu akiri kuwa hakumtii Mungu.

Je umekula ... kutoka?

Kwa mara nyingine, Mungu alijua kuwa hiki kimetokea. Tafsiri hili swali katika namna ambayo inaonyesha Mungu anamlaumu Adamu kwa kutokutii kwake. Sentensi yaweza kutafsiriwa kwa kauli hii. "Umekula ..kutoka."

Genesis 3:12

Nini hiki ulichofanya?

Mungu alikwishajua ni nini mwanamke alichofanya. Alipouliza swali hili, alikuwa akimpatia nafasi ajieleze kuhusu lile jambo, na alikuwa akionyesha kusikitishwa kwake kwa kile alichokifanya.Lugha nyingi hutumia maswali ya balagha kwa ajili ya kukemea na kukaripia. "Umefanya jambo baya"

Genesis 3:14

umelaaniwa wewe mwenyewe

"wewe peke yako umelaaniwa." Neno "laana" lipo kwanza kwa Kiebrania ili kuweka msisitizo ya tofauti kati ya baraka ya Mungu kwa wanyama na laana juu ya nyoka. Hii ni laana, au namna ambavyo laana zilitamkwa. Kwa kutamka laana hii, Mungu alifanya itokee.

wanyama wote wa kufugwa na wanyama wote wa mwituni

"wanyama wote wa kufugwa na wanyama wote wa mwitu"

Itakuwa kwa tumbo lako utakwenda

"Utasogea kwenye ardhi kwa kutumiatumbo lako". Maneno "itakuwa kwa tumbo lako" huja kwanza kuweka msisitizo ya tofauti kati ya njia ya wanyama wengine wanavyosogea kwa kutumia miguu yao na njia ya nyoka atakavyotelezateleza kwa tumbo lake. Hii pia ni sehemu ya laana.

mavumbi utakula

"utakula mavumbi". Maneno "ni mavumbi" huja kwanza kuweka msisitizo ya tofauti kati ya mimea juu ya ardhi ambayo wanyama wengine hula na chakula kichafu cha ardhi ambacho nyoka angekula. Hii ni sehemu ya laana.

uadui kati yako na mwanamke

Hii inamaana ya kwamba nyoka na mwanamke wangekuja kuwa maadui.

uzao

"mtoto" au "kizazi". Neno "uzao" linamaanisha nini mwanamume huweka ndani ya nwanamke kusababisha mtoto kukua ndani ya mwanamke. Kama neno la "mtoto" linaweza kumaanisha zaidi ya mtu mmoja, kama neno "vizazi".

Atakujeruhi ... kisigino chake

Maneno "wako" na "wake" yanamaanisha uzao wa mwanamke. Iwapo "uzao" ulitafsiriwa kwa wingi, hii yaweza tafsiriwa kama "watajeruhi .. visigino vyao"; kwa hali hii, "wao" na "yao" hutumika kutafsiri kiwakilishi kimoja.

Atakujeruhi

"ponda" au "kujeruhi" au "shambulia"

Genesis 3:16

nitaongeza uchungu wako sana

"Nitafanya maumivu yako kuongezeka sana" au "Nitafanya maumivu yako kuwa makali sana"

wakati wa kuzaa watoto

"katika kuzaa watoto" au "utakapozaa watoto"

Tamaa yako itakua kwa mume wako

"Utakuwa na tamaa kubwa kwa mume wako." Maana yake yaweza kuwa 1) "Utataka kuwa na mume wako sana" au 2) "Utataka kumuongoza mume wako"

atakutawala

"atakuwa bwana wako" au "atakuongoza"

Genesis 3:17

Adamu

Jina Adamu ni sawa na jina la Kiebrania kwa ajili ya neno "mwanamume". Baadhi ya tafsiri husema "Adamu" na baadhi husema "mwanamume". Unaweza kusema yoyote kati yao maana hulenga mtu mmoja.

umesikiliza sauti ya mke wako

Hii ni lahaja. "umetii kile mkeo kakuambia"

umekula kutoka katika mti

Unaweza kusema ni nini kile walichokula. "wamekula tunda la mti" au "wamekula sehemu ya matunda ya mti"

usile matunda yake

"Hutakiwi kula kutoka kwake" au "Usile matunda yake"

ardhi imelaaniwa

Neno "laana" hujitokeza kwenye sentensi kuweka msisitizo ya kwamba ardhi, ambayo ilikuwa "nzuri" imekuwa chini ya laana ya Mungu sasa. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Ninalaani ardhi"

kupitia kazi yenye maumivu

"kwa kufanya kazi ngumu"

utakula

Neno "utakula" linamaanisha ardhi ambayo ni ufafanuzi wa sehemu ya mimea, ambayo huota ardhini na watu hula. "utakula kile kiotacho kutoka kwake"

mimea ya shambani

Maana yaweza kuwa 1) "mimea unayoitunza shambani mwako" au 2) "mimea ya mwitu inayoota katika mashamba yako"

Kwa jasho la uso wako

"Kwa kufanya kazi ngumu na kufanya uso kutoka jasho"

utakula mkate

Hapa neno "mkate" ni kiwakilishi kwa chakula kwa ujumla. "utakula chakula"

mpaka utakapo irudia ardhi

"hadi utakapokufa na mwili wako unawekwa ndani ya ardhi." Kwa baadhi ya tamaduni, waliweka miili ya watu waliokufa kwenye shimo ardhini. Kazi ya mwanamume haikamiliki hadi kipindi cha kifo na kuzikwa kwake.

kwa kuwa wewe ni mavumbi na kwenye mavumbi utarudi

Nimekufanya kutoka kwenye udongo, kwa hiyo mwili wako utakuwa udongo tena".

Genesis 3:20

Mwanamume

Baadhi ya tafsiri husema "Adamu".

akaita mke wake jina Hawa

"alimpa mke wake jina la Hawa" au "alimuita mkewe Hawa"

Hawa

Neno Hawa linafanana na neno la Kihebrania lenye maana ya "wenye uhai".

wote wenye uhai

Neno hapa "wenye uhai" linamaanisha watu. "watu wote"

mavazi ya ngozi

"mavazi yanayotengenezwa kwa ngozi ya wanyama"

Genesis 3:22

Mwanamume

Maana yaweza kuwa 1) Mungu alimaanisha binadamu mmoja, mwanamume au 2) Mungu alikuwa akimaanisha binadamu kwa ujumla, kwa hiyo ilimaanisha mwanamume na mke wake. Hata kama Mungu alikuwa akizungumza kuhusu mtu mmoja, alichosema kiliwahusu wote wawili.

kama mmoja wetu

"kama sisi". Kiwakilishi "sisi" ni wingi.

ajuaye mema na mabaya

Hapa "mema na mabaya" ni msemo ambao unamaana ya tofauti zote mbili na kila kitu katikati. "kujua kila kitu, ikiwemo mema na mabaya"

hataruhusiwa

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Sitamruhusu"

mti wa uzima

"mti unaowapa watu uzima"

ardhi ambayo kwahiyo alikuwa ametwaliwa

"ardhi kwa maana alichukuliwa kutoka ardhini". Hii haimaanishi sehemu moja husika katika nchi ambayo Mungu alimchukua.

Kwa hiyo Mungu akamfukuza mtu huyu nje ya bustani

"Mungu alimlazimisha mwanamume aondoke bustanini." Hii inamaanisha tukio la 3:22, ambapo inasema "Yahwe Mungu alimfukuza kwenye bustani ya Edeni". Mungu hakumfukuza mwanamume mara ya pili.

kulima

Hii ina maana kinachohitajika ili mimea iweze kuota vizuri.

ili kulinda njia ya kwenda kwenye mti wa uzima.

"ili kuzuia watu wasiende kwenye mti wa uzima"

upanga wa moto

Maana yaweza kuwa 1) upanga ambao unatoa moto au 2) moto ulikuwa na umbo kama upanga.