Genesis 1

Genesis 1:1

Hapo mwanzo, Mungu aliumba mbingu na nchi

"Hii inahusu jinsi gani Mungu aliumba mbingu na nchi hapo mwanzo." Kauli hii inafupisha sura iliyobaki. Lugha zingine huitafsiri kama "Hapo zamani sana Mungu aliziumba mbingu na nchi."

Hapo mwanzo

Hii inalenga kuanza kwa dunia na kila kitu ndani mwake.

mbingu na nchi

"anga, ardhi, na kila kitu ndani yao"

mbingu

Hapa inamaanisha anga

Bila umbo na tupu

Mungu alikuwa hajaweka dunia katika mpangilio.

vilindi

"maji" au "maji ya kina kirefu" au "maji mengi"

maji

"maji" au "uso wa maji"

Genesis 1:3

Na kuwe na nuru

Hii ni amri. Kwa kuamuru kuwepo na nuru, Mungu alifanya iwepo.

Mungu akaona nuru, kuwa ni njema

"Mungu aliifikiria nuru na kufurahishwa nayo." Hapa "Njema" inamaanisha "kufurahisha" au "inayofaa."

akaigawa nuru na giza

"alitenganisha nuru na giza" au "alifanya kuwepo na nuru wakati mmoja na giza wakati mwingine." Hii inamaanisha Mungu aliumba wakati wa mchana na usiku.

Ikawa jioni na asubuhi, siku ya kwanza

Mungu alifanya vitu hivi katika siku ya kwanza ambapo ulimwengu ulianza kuwepo.

jioni na asubuhi

Hii inamaanisha siku nzima. Mwandishi anazungumzia siku nzima kana kwamba ni sehemu mbili. Kwa tamaduni za Kiyahudi, siku moja huanza baada ya jua kuzama.

Genesis 1:6

Na kuwe na anga kati ya maji ...na ligawe

Hizi ni amri. Kwa kuamuru kwamba anga kati ya maji iwepo na igawe maji, Mungu alifanya iwepo na kugawa maji na maji.

anga

"anga tupu na wazi". Watu wa Kiyahudi walichukulia uwazi huu kuwa na umbo kama la kuba au bakuli lililofunikwa.

kati ya maji

"ndani ya maji"

Mungu alifanya anga na kugawanya maji

"kwa namna hii, Mungu alifanya anga na kugawa maji." Mungu alipozungumza, ilitokea. Sentensi hii inaeleza kitu gani Mungu alifanya alipokuwa akizungumza.

ikawa hivyo

"ilitokea kama hivyo" au "Hivyo ndivyo ilivyotokea". Mungu alichoamuru kilitokea kama alivyotamka kitokee. Msemo huu hujitokeza katika sura nzima na una maana ile ile kila unapojitokeza.

jioni na asubuhi

Hii inamaanisha siku nzima. Mwandishi anazungumzia siku nzima kana kwamba ni sehemu mbili. Kwa tamaduni za Kiyahudi, siku moja huanza baada ya jua kuzama.

siku ya pili

Hii inamaanisha siku ya pili ambapo ulimwengu ulipoanza kuwepo.

Genesis 1:9

Maji yaliyo chini ..yakusanyike

Hii inaweza kutafsiriwa kama kitenzi endelevu. Hii ni amri. Kwa kuamuru maji yakusanyike, Mungu aliyafanya yakusanyike pamoja.

na ardhi kavu ionekane

Maji yalikuwa yamefunika ardhi. Basi maji yalisogea pembeni na baadhi ya ardhi kubaki wazi. Hii ni amri. Kwa kuamuru kwamba ardhi kavu ionekane, Mungu alifanya ionekane. "na ardhi kavu ionekane" au "na ardhi kavu iwe wazi" au "na ardhi ifunuliwe"

ardhi kavu

Hii inamaanisha ardhi ambayo haijafunikwa kwa maji. Haimaanishi ardhi ambayo ni kavu sana kwa ajili ya kilimo.

ikawa hivyo

"ilitokea kama hivyo" au "Hivyo ndivyo ilivyotokea". Mungu alichoamuru kilitokea kama alivyotamka kitokee. Msemo huu hujitokeza katika sura nzima na una maana ile ile kila unapojitokeza.

nchi

"ardhi" au "chini"

Akaona kuwa ni vyema

Hapa "ni" inamaanisha nchi na bahari.

Genesis 1:11

Na nchi ichipushe mimea

Hii ni amri. Kwa kuamuru ya kwamba mimea ichipuke juu ya ardhi, Mungu alifanya ichipuke. "Mimea na ichipuke juu ya ardhi" au "Mimea na iote juu ya ardhi"

mimea: miche inayotoa mbegu na miti ya matunda izaayo matunda

"mimea, kila mche unaozaa mbegu na kila mti unaozaa matunda" au "mmea. Kuwe na mimea itoayo mbegu na matunda ya miti yazaayo matunda". Mimea hutumika hapa kama msemo wa jumla inaojumlsiha mimea na miti yote.

miche

Hii ni aina ya mimea ambayo ina mashina laini, na sio kama ya mbao

miti ya matunda izaayo matunda ambayo mbegu yake imo ndani yake

miti izaayo matunda yenye mbegu ndani yake

kila kitu kwa namna yake

Mbegu zingezaa mimea na miti ambayo ingekuwa kama zile zilipotokea. Kwa namna hii, mimea na miti zingejizalisha zenyewe.

ikawa hivyo

"ilitokea kama hivyo" au "Hivyo ndivyo ilivyotokea". Mungu alichoamuru kilitokea kama alivyotamka kitokee. Msemo huu hujitokeza katika sura nzima na una maana ile ile kila unapojitokeza.

Mungu akaona kuwa ni vyema

Hapa "ni" inamaanisha mimea, mazao na miti.

jioni na asubuhi

Hii inamaanisha siku nzima. Mwandishi anazungumzia siku nzima kana kwamba ni sehemu mbili. Kwa tamaduni za Kiyahudi, siku moja huanza baada ya jua kuzama.

siku ya tatu

Hii inamaanisha siku ya tatu ambapo ulimwengu ulianza kuwepo.

Genesis 1:14

Kuwe na mianga katika anga

Hii ni amri. Kwa kuamuru ya kwamba mianga iwepo, Mungu alifanya iwepo

mianga katika anga

"vitu ving'aavyo katika anga" au"vitu vitoavyo mwanga katika anga". Hii inaamanisha jua, mwezi na nyota

katika anga

"katika uwazi wa anga" au "katika uwazi mkubwa wa anga"

kutenganisha mchana na usiku

"kutenganisha mchana na usiku." Hii inamaanisha "kutusaidia kutambua tofauti kati ya mchana na usiku." Jua inamaanisha ni mchana, na mwezi na nyota humaanisha ni usiku.

na ziwe kama ishara

Hii ni amri. Kwa kuamuru ya kwamba ziwe kama ishara, Mungu alizifanya zitumike kama ishara. "Na zitumike kama ishara" au "na zioneshe"

ishara

Hapa inamaanisha kitu kinachofunua au kinacholenga jambo

majira

"Majira" inamaanisha nyakati zitakazotengwa kwa sikukuu na mambo mengine ambayo watu hufanya.

kwa majira, kwa siku na miaka

Jua, mwezi, na nyota huonyesha muendelezo wa muda. Hii inatusaidia kutambua ni wakati gani tukio hutokea kila wiki, mwezi au mwaka.

ziwe mianga katika anga ili kutoa mwanga juu ya nchi

Hii ni amri. Kwa kuamuru ziwe mianga juu ya nchi, Mungu alifanya zimulike juu ya nchi

kutoa mwanga juu ya nchi

"kutoa mwanga juu ya nchi" au "kuangazia nchi". Nchi haitoi mwanga yenyewe bali hupata mwanga na kurudisha mwanga.

ikawa hivyo

"ilitokea kama hivyo" au "Hivyo ndivyo ilivyotokea". Mungu alichoamuru kilitokea kama alivyotamka kitokee. Msemo huu hujitokeza katika sura nzima na una maana ile ile kila unapojitokeza.

Genesis 1:16

Mungu akafanya mianga mikuu miwili

"Kwa njia hii Mungu akafanya mianga miwili mikuu" Sentensi hii inaelezea Mungu alichofanya alipozungumza.

mianga miwili mikuu

"mianga miwili mikuu" au "mianga miwili ing'aaro". Mianga miwili mikuu ni jua na mwezi.

kutawala mchana

"kuongoza mchana kama mtawala angozapo kundi la watu" au "kuweka alama katika siku"

siku

Hii inamaanisha masaa ya mchana pekee

mwanga mdogo

"mwanga mdogo" au "mwanga hafifu"

katika anga

"katika mbingu" au "katika uwazi wa angani"

kutenganisha mwanga na giza

"kutenganisha mwanga na giza" au "kutoa mwanga kwa kipindi kimoja na giza kwa kingine.

Mungu akaona kuwa ni vyema

Hapa "ni" inamaanisha jua, mwezi na nyota.

jioni na asubuhi

Hii inamaanisha siku nzima. Mwandishi anazungumzia siku nzima kana kwamba ni sehemu mbili. Kwa tamaduni za Kiyahudi, siku moja huanza baada ya jua kuzama.

siku ya nne

Hii inamaanisha siku ya nne ambapo ulimwengu ulianza kuwepo.

Genesis 1:20

Na maji yajae idadi kubwa ya viumbe hai

Hii ni amri. Kwa kuamuru viumbe hai wajaze maji, Mungu alifanya viwepo. Baadhi ya lugha huweza kuwa na neno moja linalomaanisha aina wote wa samaki na viumbe wa baharini. "Maji yajae viumbe wote" au "viumbe wengi wanao ogelea waishi baharini".

na ndege waruke

Hii ni amri. Kwa kuamuru ya kwamba ndege waruke, Mungu alifanya waruke.

ndege

"wanyama warukao" au "vitu vinavyoruka"

anga tupu ya angani

"nafasi iliyo wazi ya angani" au "anga"

Mungu aliumba

"kwa njia hii Mungu aliumba"

viumbe wa majini wakubwa

"wanyama wakubwa wanaishi ndani ya bahari"

kwa aina yake

Vitu hai vya "aina" moja ni sawa na kule vilivyotokea.

kila ndege mwenye mabawa

"kila kitu kipaacho chenye mabawa." Iwapo neno kwa ajili ya ndege linatumika, linaweza kuwa kawaida kwa baadhi ya lugha kusema "kila ndege" kwa maana kila ndege ana mabawa.

Mungu akaona kuwa ni vyema

Hapa "ni" inamaanisha ndege na samaki.

Genesis 1:22

akavibariki

"alibariki wanyama aliowaumba"

zaeni na muongezeke

Hii ni baraka ya Mungu. Aliwaambia wanyama wa baharini kuzalisha wanyama wengine wa baharini kama wao wenyewe, ili kwamba wawe wengi baharini. Neno "ongezeka" linafafanua jinsi gani wanapaswa "kuongezeka"

ongezeka

"ongezeka kwa idadi kubwa" au "kuwa wengi"

Ndege waongezeke

Hii ni amri. Kwa kuamuru ya kwamba ndege waongezeke, Mungu aliwafanya ndege waongezeke.

ndege

"wanyama warukao" au "vitu virukavyo"

jioni na asubuhi

Hii inamaanisha siku nzima. Mwandishi anazungumzia siku nzima kana kwamba ni sehemu mbili. Kwa tamaduni za Kiyahudi, siku moja huanza baada ya jua kuzama.

siku ya tano

Hii inamaanisha siku ya nne ambapo ulimwengu ulianza kuwepo.

Genesis 1:24

nchi na itoe viumbe hai

"Nchi na itoe vitu hai" au "na viumbe hai vingi viishi juu ya nchi". Hii ni amri. Kwa kuamuru ya kwamba nchi itoe viumbe hai, Mungu alifanya nchi itoe viumbe hai.

kila kiumbe kwa aina yake

"ili kwamba kila aina ya mnyama izae aina yake zaidi"

mnyama wa kufugwa, vitu vitambaavyo, na wanyama wa nchi

Hii inaonyesha ya kwamba Mungu aliumba kila aina ya wanyama. Iwapo lugha yako inayo namna nyingine ya kuunganisha wanyama wote katika kundi, basi waweza tumia hilo neno, au tumia kundi hili.

mnyama wa kufugwa

"wanyama wanaotunzwa na binadamu"

vitu vitambaavyo

"wanyama wadogo"

wanyama wa nchi

"wanyama mwitu" au "wanyama hatari"

ikawa hivyo

"ilitokea kama hivyo" au "Hivyo ndivyo ilivyotokea". Mungu alichoamuru kilitokea kama alivyotamka kitokee. Msemo huu hujitokeza katika sura nzima na una maana ile ile kila unapojitokeza.

Mungu akafanya wanyama wa nchi

"Kwa njia hii Mungu aliwafanya wanyama wa nchi"

Akaona kuwa ni vyema

Hapa "ni" inamaanisha viumbe hai wa nchi.

Genesis 1:26

na tufanye

Hapa neno "tumfanye" lina maana ya Mungu. Mungu alisema alichokusudia kukifanya. Kiwakilishi nomino "tu" ni wingi. Uwezekano wa sababu za wingi ni 1) wingi huu unaweza maanisha Mungu anajadili jambo na malaika ambao hukamilisha baraza lake la mbinguni au 2) wingi huu unaonyesha dalili baadae katika Agano Jipya kuhusisha ya kwamba Mungu yupo katika Utatu Mtakatifu. Baadhi hutafsiri kama "Na nifanye" au "Nitafanya". Kama utafanya hivi, basi zingatia kuweka maandishi mafupi kusema kuwa neno lina wingi.

mtu

"binadamu" au "watu". Neno hili hapa halimaanishi jinsia ya kiume pekee.

katika mfano wetu, wa kufanana na sisi

Misemo hii miwili ina maana moja na inasisitiza kuwa Mungu alifanya binadamu awe kama yeye. Mstari huu hausemi ni kwa njia zipi Mungu alifanya watu wawe kama yeye. Mungu hana mwili, kwa hiyo haimanishi watu watafanana na Mungu. "na kufanana na sisi".

wawe na mamlaka juu ya

"kutawala" au "kuwa na mamlaka juu"

Mungu akamuumba mtu ...alimuumba

Sentensi hizi mbili zina maana moja na zinasisitiza ya kwamba Mungu aliumba watu katika mfano wake.

Mungu akamuumba mtu

Namna Mungu alivyoumba binadamu ni tofauti na jinsi alivyoumba vitu vingine vyote. Usieleze bayana ya kwamba aliumba binadamu kwa kuongea, kama mistari ya nyuma inavyoonyesha.

Genesis 1:28

Mungu akawabariki

Neno "akawabariki" lina maana ya mwanamume na mwanamke aliowaumba Mungu.

zaeni na kuongezeka

Mungu alimwambia mwanamume na mwanamke kuzalisha watu zaidi kama wao wenyewe ili kwamba wawe wengi kama wao. neno "kuongezeka" linaelezea namna wanavyotakiwa "kuzaa".

Jazeni nchi

jazeni nchi na watu.

Genesis 1:30

Taarifa ya jumla:

Mungu anaendelea kuzungumza

kila ndege wa angani

"ndege wote wanaopaa angani"

chenye pumzi ya uhai

"kinachopumua". Msemo huu unasisitiza ya kwamba wanyama hawa walikuwa na uhai tofauti na mimea. Mimea haiwezi kupumua, na ilipaswa kutumika kama chakula cha wanyama. Hapa "uhai" una maana ya uhai wa mwili.

ikawa hivyo

"ilitokea kama hivyo" au "Hivyo ndivyo ilivyotokea". Mungu alichoamuru kilitokea kama alivyotamka kitokee. Msemo huu hujitokeza katika sura nzima na una maana ile ile kila unapojitokeza.

Tazama

"hasa". Hapa neno "tazama" linaongeza msisitizo kwa kile kinachofuata.

kikawa chema sana

Mungu alipotazama kila kitu alichokiumba, "kikawa chema sana".

jioni na asubuhi

Hii inamaanisha siku nzima. Mwandishi anazungumzia siku nzima kana kwamba ni sehemu mbili. Kwa tamaduni za Kiyahudi, siku moja huanza baada ya jua kuzama.

siku ya sita

Hii inamaanisha siku ya sita ambapo ulimwengu ulianza kuwepo.