1 Yahweh akatamwiia na Musa akamba, 2 'Waete Aroni hamwe na wanawe, nguo na mavuta ya upako, fahali kwa ajii ya kafaa ya zambi, ngoto ngosi waidi ba ngahu ya mkate wesao hamila. 3 Etanga kusanyiko dose kwe engiiyo da hema da kudugania." 4 Kwa iyo Musa akagosoa kana Yahweh ekumwamuluvyo nado kusanyiko nee deza hamwe mbele ya engiiyo da hema da kudugania. Ikabinda Musa akadambia kusanyiko, 5 "Ivi nee ekutiamuluvyo Yahweh tigosoe." 6 Musa akamweeta Aroni na wanawe na kuwasunta kwa mazi. 7 Akamhamba Aroni kanzu ya ndani yenayo mikono milefu wa kubua mwe mavindi na kumtaha ukumbuu mwe kigudi chakwe, akamhamba joho da chongoi denado mikono milefu na kumhamba kia kisibao chenacho vipande viidi mwe ifu na mgongo na kukitaha kuzunguka mwe kigudi chakwe na mkuuzo wekusokotwao kwa usitadi na na kukazwa mwe mwii wakwe. 8 Ikabinda Musa akaika kafuko mwe kifua cha Aroni, na mwe kafuko ako akaika Urimu na Thumimu. 9 Na akaawa aho akamfunga kilemba mwe mtwi na uwanga ya kilemba kwa mbele akaika bamba da zahabu; diwe taji takatifu, kana Yahweh ekumwamuluvyo yeye. 10 Musa akayadoa aye mavuta ya upako, akadihaka dia hema da kudugania na kia kintu chekwachoumo ndani yakwe na kuvipagua kwa ajii ya Yahweh. 11 Akamyaga ayo mavuta uwanga ya mazabahu maa mfungate, akabinda akaihaka mavuta iyo mazabahu na via vyakwe vyose na chano cha kwehakia na kitako chakwe ili kuvipagua kwa ajii ya Yahweh. 12 Akagida sehemu ya mavuta ya upako uwanga ya mutwi wa Aroni na akaawa aho akamhaka mavuta ili kumpagua. 13 Musa akawaeta wana wa Aroni na kuwahamba kia yumwe kazu ya ndani yenayo ulefu wa kubua kwa mavindi. Kia yumwe ywao akamtaha ukumbuu mwe kigudi chakwe na kuwafunga vitambaa vya kitani mwe mitwi yao kana via Yahweh ekumwamuluvyo Musa. 14 Musa akamweeta uyo fahali kwa ajii ya kafaa ya zambi, nae Aroni na wanawe wakaika mikono yao uwanga wa mutwi wa fahali ambae wamweeta kwa ajii ya da zambi. 15 Musa akamchinja na akabinda akadoa sehemu ya mphome yakwa kwa chaa chakwe na kuiika uwanga ya mphembe za mazabahu, akaing'aza iya mazabahu, na kuipagua kwa Mungu, ambaho kwa kugosoa ivyo kaisibabisha mazabahu kuwa hantu ya kafaa kwa kugosweea wevano. 16 Akadoa mavuta yose yekuwaho hantu ha ndani, kia kiwambo cha ini, zia figo mbii hamwe na mavuta yakwe, Musa akayoka iyo nyama uwanga ya mazabahu. 17 Akini yuda fahali, babu dakwe, nyama yakwe na mavi yakwe akavyoka chongoi ya nkambi, kama via Yahweh ekuwavyokaamulu yeye. 18 Musa akamweeta yuda ngoto mgosi kwa ajii ya kudagamizwa, nae Aroni na wanawe wakaika mikono yao uwanga ya mutwi wa uyo ngoto. 19 Musa akamchinja ngoto na kumyaga mphome yakwe kia upande wa mazabahu. 20 Nae akamsengasenga ngoto ntiintii akauteketeza mutwi wakwe hamwe na zia ntii za mavuta. 21 Akazisunta kwa mazi zia mphaamo za ndani hamwe na miundi na akamdamiza ngoto ngima uwanga ya mazabahu. Nee ni zabihu ya kudagamizwa na iavya mhenpe mtana, kafaa dekusolwado kwa Yahweh kwa moto kana via Yahweh ekumwamuluvyo Musa. 22 Ikaawa aho Musa akamweeta yuda ngoto mgosi mtuhu, ngoto ywa kuikwa wakfu, nae Aroni na wanawe wakaika mikono yao uwanga ya mutwi wa ngoto. 23 Aroni akamchinja, nae Musa akadoa sehemu ya mphome na kuiika kwe mphembo ya gutwi da Aroni da kuume, uwanga ya chaa kikuu cha mkono wakwe wa kuume na kwe chaa kikuu cha muundi wakwe wa kuume. 24 Akawaeta wana wa Aroni, nae akaika sehemu ya mphome ya ngoto yuda mwe mphembo ya gutwi dao da kuume mwe chaa kikuu chao cha mkono wa kuume na mwe chaa chao kikuu cha muundi wa kuume. Ikabinda Musa akamyaga mphome ya uyo kia mphaamo ya mazabahu. 25 Nae akayadoa yada mavuta, mavuta yakwe mkia, mavuta yekuwayo mphaamo za ndani na mavuta yagubikayo ini, zia figo mbii hamwe na mavuta yakwe na nyonga ya kuume. 26 Akadoa mkate umwe kuawa mwe ngahu ya mikate ye sayokuwa na hamila ambayo nee imbele za Yahweh, akadoa mkate umwe wesao na hamila, na mkate umwe wekwaandaiwao kwa mavuta, na mkate msisii wa kaki na akaiika uwanga ya mavuta na uwanga ya nyonga ya ya la ngoto. 27 Akaiika yose mwe mikono ya Aroni na mwe mikono ya wanawe na kuisingisa mbele za Yahweh kuwa kafaa da kusingiswa. 28 Ikaawa aho Musa akaidoa mikate iyo kuwa mwe mikono yao na kuidagamiza uwanga ya mazabahu kwa ajii ya kafaa da kudagamizwa. Nee ni kafaa da kuikwa wakfu na iavya mhemphe mtana. Nee ni kafaa dekusolwado kwa Yahweh kwa moto. 29 Musa akakidoa kidali na kukisingisa kuwa kafaa ya kusingiswa kwa kwa Yahweh. Nee ni mgao wa Musa wa ngoto wa kuikiwa mikono kwa makuhani, kama via Yahweh ekuwavyo kamwaamulu yeye. 30 Musa akadoa sehemu ya mavuta ya upako na mphome yekuwayo uwanga ya mazabahu, nae akayamyaga aya uwanga ya nguo za Aroni, uwanga ya nguo zakwe mwenye na uwanga ya nguo za wana wa Aroni wekuwao hamwe nae. Kwa sia inu kampagua Aroni na nguo zakwe na wanawe na nguo zao kwa ajii ya Yahweh. 31 Kwa iyo Musa akawambia Aruni na wanawe, "Yembikeni nyama mbele ya engiiyo da hema da kuduganiana, na aho mwenda mwiide hamwe na mkate we mwe ngahu ya kuikwa wakfu, kana ekuamliwavyo, kwamba, "Aroni na wanawe wenda waide.' 32 Masigazo yoyose ya nyama na mikate wenda uyadagamize kwa moto. 33 Na nkamna mhauke kwe engiio da hema da kudaganiana kwa muda wa misi mfungate, hata ndiho zitimie misi ya kuikwa mikono kwenu. Kwa kuwa mda wa misi mfungate, Yahweh enda amiike wakfu. 34 Chekugosokacho msi unu-- Yahweh nee kakiamulu kigosoke ili kugosoa wevano kwa ajii yenu. 35 Mwenda mwekae kwe engiio da hema da kuduganiana musi na kio misi mfungate, nanywi itozeni amli ya Yahweh ili mwesekweza kufa, kwa ajii ivi nee vyekuamliwavyo. 36 Kwa iyo Aroni na wanawe wakagosoa mbui yose ambayo Yahweh nee kawaamulu kwa kanwa cha Musa.