1 Yahweh neeamba na Musa, akamba, 2 "Wambie wantu wa Waisraeli, 'mntu yoyose gatigati ya wantu Israeli, au Mgeni yoyose mwekaa miongoni mwa Waisraeli endaeamuavye mwanawe yoyose kwa Moleki, hakika andaakomwe. Ni lazima wantu wa sii wamhonde kwa maiwe. 3 Pia nndanikaze cheni changu dhidi ya mntu uyo na kumsenga hae kuawa gatigati mwa wantu wakwe kwa via kamuavya mwanawe kwa Moleki, ili kuhagea nuhusi hantu hangu hatakatifu na kunajisi zina dangu takatifu. 4 Na kama wantu wa sii wandawafumbue meso yao kwa mntu uyo endahoamuavye yumwe wa wanawe kwa Moleki, kama nkawanawamkome mntu uyo, neaho mimi mwenye nndanikaze cheni changu dhidi ya mntu uyo na ukoo wakwe, 5 Nami nndanimdumue hae hamwe na yoyose mwefenya ukianga ili kugosoa ukianga na Moleki. 6 Mntu yuda mumhitukia watamwiao na watakufa, au na wada wamtamwiao na roho ili kugosoa ukianga nao, Nndanikaze cheni changu dhidi ya mntu uyo; Nami nndanimdumue hae aawe gatigati ya wantu wakwe. 7 Kwa iyo jitakaseni wenye na mue watakatifu kwa via mimi ne Yahweh Mungu yenu. 8 Nndamzitunze amari zangu na kuzifuta. Mimi ne Yahweh amitengae nyinyi muwe watakatifu. 9 Yeyose mumlani tati yakwe au mami yakwe hakika mntu andaakomwe. Kamlani tati yakwe au mami yakwe, kwa iyo ana hatia na astahili kufa. 10 Mgosi yoyose agosoae ukianga na mvye wa mgosi mtuhu, yani, yeyose mgosoa ukianga na mvyee ya jirani yakwe -- yuda mgosi mkianga na mvyee mkianga ni lazima wose waidi wakomwe. 11 Mgosi yoyose mgona na mvyee ya tati yakwe ili kudugana nae kimwii kamfedhehesha tati yakwe mwenye. Wose waidi; mwana uyo na mvyee uyo wa tati yakwe kwa hakika wanda wakomwe. Wanahatia na wastahili kufa. 12 Kama mgosi endaagone na mvyee wa wanawe, wose waidi; mgosi uyo na mvyee uyo na wanawe hakika wanawakomwe. Wagosoa uhitu. Wana hatia na wastahili kufa. 13 Kama mgosi agona na mgosi mtuhu kama agonavyo na mvyee, wose waidi wandawawe wagosoa jambo ido ovu. Hakika nndawakomwe wana hatia na wastahili kufa. 14 Ikiwa mgosi andaamtegue mvyee na pia akamtegua mmaa wa mvyee uyo, unu ni uovu. Ni lazima waokwe kwa moto, wose waidi, mgosi uyo na mvyee uyo, ili kwamba nnkahanahawe na uovu miongoni mwenu. 15 Ikiwa mgosi agona na mnyama, hakika andaakomwe, ni lazima akomwe mnyama uyo pia. 16 Ikiwa mvyee amsogeea mnyama ili agone nae, ni lazima mumkome mvyee uyo hamwe na mnyama. Kwa hakika lazima wakomwe. Wana hatia na wastahili kufa. 17 Ikiwa mgosi agona na umbude, ama ni mndee ya tati yakwe au mndee ya mami yakwe--ikiwa wagona hamwe, iyo ni mbui ya soni. Ni lazima wakomwe waawe mwe meso ya wantu ao, kwa sababu kagona na umbude. Ni lazima enue hatia yakwe. 18 Kama mgosi kagona na mvyee mwe kipindi cha hedhi yakwe, na kadugana nae kimwii, andaawe kagubua mtiririko wa mmpome yakwe, chanzo cha mmpome yakwe. Ni lazima wose waidi wadumulwe kuawa gatigati ya wantu wao. 19 Usekugona na mndee ya mami yako, au mndee ya tati yako, kwa sababu nekudaha kumwaibisha mwezio wa hehi. Ni lazima undaudoe hatia yako mwenye. 20 Ikiwa mgosi agona na mamiyakwe gazi, andaawe kamfedhehesha mtumbawe. Wendahawafe nndaniweke adhabu wose waidi, na wendahowafe nndaniuse ulisi wa wana wao ambao neewaupata kuawa kwa wavyazi wao. 21 Ikiwa mgosi amtegua mvyee wa kakiwe ambapo kakiwe bado yu hai, ido ni jambo de soni. Kamfedhehesha kakiwe, na nndaniuse mai yoyose ambayo wanawe neewakalisi kuawa na wavyazi wao. 22 Ikiwa iyo iwapasa kuzitoza amri na sheia zangu zose; ni lazima mzitii ili kwamba ida sii ambayo niwaeteayo kwekaa isekuwatahisa nyinyi. 23 Msekwenda kwe destui za mataifa ambayo nndaniyaguuse mbele yenu, ni kwavia wagosoa mambo aya yose, nami nkiwachukia wao. 24 Nami nndaniwambia nyinyi, "Nndamuimiliki sii yao, nndaniaavye kwenu ili mmiliki, sii yetikaya mee na asai. Mimi ne Yahweh Mungu yenu, mwekuwatenga nyinyi kuawa kwe wantu wengi. 25 Ni lazima msague kati ya wanajisi na wada watana na kati ya wadege walionajisi na watana. Msekwechafua wenye kwa wanyama au wadege au kiumbe chendachoasi uwanga ya sii chenacho unajisi, ambacho nkitenga kuwa najisi. 26 Mndamuwe watakatifu, kwa via mimi, Yahweh, ni mtakatifu, nami nkiwatenga nyinyi kuawa kwa wantu wengi, kwa via nyie ni wangu. 27 Mgosi au mvyee mtamwiiya na wekufao au mtamwia na roho hakika nndaakomwe. Wantu wandawawahonde kwa maiwe. Wanayo hatia na wastahili kufa.