1 Yahweh akamwamba Musa, 2 "Tamwiia na wantu wa Israeli, uwambe, 'Kana ikatenda mvyee enda awe naifu na kusuzamia mwana kigosi, naye enda awe nagisi mda wa misi mfungate, ni kana tu via eivyo nagisi mwe misi ya kipindi chakwe kwa mwezi. 3 Mwe msi wa mnane nyama ya zobe da mwana kigosi denda digwise. 4 Ikabinda un'gazi wa mmaa wa kuawa npome yakwe wenda usongwekwa mda wa misi mitatu. Nkakunda kudonta kintu chochose ambacho ni kitakatifu au kusogea eneo da hema kiamuo yendaho isie misi ya kung'azwa kwakwe. 5 Akini kana enda asuzamie mwana kivyee, nae enda awe nagisi kwa mda wa majuma maidi, kana eivyo ukati wa kipindi chakwe, ikabinda ung'azi wa mmaa wenda uendee kwa misi sitini mtandatu. 6 Misi ya ung'azi wakwe ndiho isiie, kwa ajii ya ya mwana au mndee enda alazike kueta kwa kuhani mwana-ngoto ywa mwaka umwe kuwa sadaka ya kuokwa na kinda da ngiwa au huwa kuwa sadaka ya zambi, mbee ya engiiyo da hema da kudugania, 7 Ikabinda enda awaavye mbele za Yahweh na kugosoa sadaka ya kwevana kwa ajii yakwe, naye enda ang'azwe kuawana na uawaji wa npome yakwe. Ini nee sheia kuhusu mvyee msuzamia ama mwana kigosi au kivyee. 8 Na kana nkana uwezo wa kuavya mwana-ngoto, naye enda aete makinda maidi ya ngiwa au huo, yumwe kwa ajii ya sadaka ya kokwa na mtuhu kuwa sadaka ya zambi, nae kuhani enda agosoe wevano kwa ajii yakwe; naye enda awe mtanda."