1 Mgosi akagona na Hawa mkaziwe. Akenua ifu na akamvyaa Kaini. Akagombeka, "Nkivyaa mwanakigosi nchambizwa ni Yahwe." 2 Akabinda akamvyaa nduguye Habili. Habili akatenda muisi, mia Kaini akatenda muimi. 3 Ikatenda baada ya muda Kaini akaeta sehemu ekupatayo inga kafaa kwa Yahwe. 4 Habili nae akaeta sehemu ya uvyazi wakwe wa bosi wa wanyama wakwe na sehemu zekunonazo. Yahwe akamkubali Habili hamwe na kafaa yakwe, 5 akini Kaini hamwe na kafaa yakwe Mungu nkekuikubali. Nee Kaini akimwa visiavyo, na cheni chakwe kikakunjana. 6 Yahwe akamwamba Kaini, "kwa mbwai kukimwa na kwani cheni chako kukikunja? 7 Kana ukagosoa vyedi, je nkuna upate kibali? akini kana nkunautende dedi, zambi iuko yakutabii he muango naho yatamani kukutawala, iyakini wondigwa uivote. 8 Kaini akamwamba nduguye Habili. Hata ukati wekuaho tanga, Kaini kenuka zidi ya Habili nduguye akamkoma. (mwetafasii za kae zagombeka, Kaini kamwamba nduguye Habili, "tite tanga" wekuaho tanga Kaini akamwenukia nduguye Habili akamkoma). 9 Akabinda Yahwe akamuuza Kaini, "Nduguyo Habili yukuhi? Akamba, "nkimanya. Je mie ni mlinzi ywa ndugu yangu?" 10 Yahwe akagombeka, "Kutendani? Mphome ya nduguyo yanetanga mimi kuawiia si hesanga. 11 Na ivi nigombekaho kuigitwa wewe kuawa kwe sanga ambayo igubua kanwa chakwe kuhokea mphome ya nduguyo kuawa mwemikono yako. 12 Kuvokea ivisasa na kuendeea ndiho uime sanga nkaina ikuvyaie wewe nguvu yakwe. Ondautende mkimbizi na muntu mwese na chekao mwe inu dunia." 13 Kaini akamtambaisa Yahwe, "Azabu yangu ni nkuu komboka udahiso wangu wa kuzizimiza. 14 Kwa kwei ivieo kuniguusa kuawa mwesanga inu naho nkinanioneke hecheni chako. Ndantende mkimbizi na mwese chekao mwe inu dunia na yoyose mondaanione andaanikome." 15 Yahwe akagombeka, "Ati mntu yoyose ondaamkome Kaini, nkuu yondaimgwiie maa mfungate." Akabinda Yahwe akaika utangio mwe Kaini, ili mondaawe yoyose akamuona, muntu uyo esekumgwa unkondo. 16 Nee yatenda Kaini akahaawa hemeso ya Yhwe akenda kwekaa mwesi ya Nodi, mashaliki mwe Edeni. 17 Kaini akammanya mkaziwe akenua ifu. Akamvyaa Henoko. Akazenga mzi akawetanga kwa zina da mwanawe Henoko. 18 Kwa Henoko akavyaigwa Iradi. Iradi akamvyaa Mehuyaeli. Mehuyaeli amvyaa Methushaeli. Methushaeli akamvyaa Lameki. 19 Lameki akedoea wavyee waidi: zina dimwe nee ni Ada, na zina da yuda mtuhu nee ni Sila. 20 Ada akamvyaa Yabali. Uyu nee mwekua tati yao da wada wekwekaao mwehema wada wafugao wanyama. 21 Nduguye nee aketangwa Yubali. Uyu neekawa tati yao da wada watoao kinubi na fiimbi. 22 Sila nae akamvyaa Tubal Kaini, msani ywa via vya shaba na chuma. Dada da Tubal Kaini nee ni Naama. 23 Lameki akagombeka na wakaziwe, Ada na Sila, tegeezani sauti yangu; nywie wavyee wa Lameki, ntegeezani n'ngombekacho. Kwa ajii nkikoma muntu kwa kuniumiza mbwanga kwa kunizubua. 24 Ati Kaini ondaaihizwe nkuu maa mfungate nee ndiho Lameki onda aihizwe nkuu maa sabini na mfungate." 25 Adam akammanya mkaziwe vituhu, nee amvyaa mwanakigosi. Akamwetanga zina dakwe Sethi na akagombeka, "Mungu kunenka vituhu mwanakigosi kwa nafasi ya Habili, kwa ajii Kaini kamkoma." 26 Mwana kigosi akavyaigwa kwa Sethi na akamwetanga zina dakwe Enoshi. Ukati uo wantu nee wavoka kudetanga zina da Yahwe.