1 Yahwe akamtegeeza Sara kwa umakini kana ekuavyo kamwamba, Yahwe akamgosweea Sara kana ekuavyo kamuahidi. 2 Sara akadoa mimba na akamvyaia Abraham mwana kigosi mwe uzee wakwe, mwe muda uda uda ambao Mungu ne kawa kamwamba. 3 Abraham nkamwetanga zina mwanae, ambae kavyaigwa kwakwe, na Sara, Isaka. 4 Abraham akamtahili mwanae Isaka akubuzaho misi mnane, kana via Mungu akuavyo kamuangiiza. 5 Abraham ne kawa na umli wa miaka mia mwenga ukati mwanae Isaka avyaigwa kwakwe. 6 Sara akagombeka, "Mungu katenda niseke; kia mntu mwendaeasikie andaaseke hamwe na mie." 7 Pia akagombeka, "Nndai nekagombeka ka Abraham hambwe Sara andaaee, mwana, na sasa kwei nkimvyaia mwana kigosi mwe uzee wakwe!" 8 Mwana akakua na akaenkeswa kuonka, na Abraham akagosoa sherehe nkuu mwe msi ambao Isaka kaenkeshwa. 9 Sara akamuona mwana wa Hajiri Mmisri, ambae ne kawa kavyaigwa kwa Abraham, akazihaki. 10 Kwa iyo akamwamba Abraham, ''Mguuse uyu mvyee uyu mtumwa hamwe na mwanae: kwa kua mwana uyu wa mvyee mtumwa nkadaha kua mlisi hamwe na mwanangu Isaka." 11 Mbui inu ikamhuzunisha sana Abraham kwa saabu ya mwanae. 12 Akini Mungu akamwamba Abraham, "Usekuhuzunika kwa saabu ya mbwanga uyu, na kwa saabu ya mvyee uyu, mtumwa wako. Tegeeza mbui ambazo Sara juu ya mbui inu, kwa saabu indaiwe kwembokea Isaka hambwe uvyazi wako undawetangwe. 13 N'ndanimgosoe pia mwana wa mjakazi kua taifa, kwa saabu ni uvyazi wako.'' 14 Abraham akenuka keo keo sana, akadoa mkate na kiliba cha mazi, akamwenka Hajiri, akaika uanga ya wega dakwe. Akamuavya mbwanga akamwenka Hajiri na akawausa. Hajiri akahauka akaga mwe jagwa da Beerisheba. 15 Mazi yekusiaho kwe kiliba akamteeza mbwanga mwe kisaka kimwe. 16 Akaawaaho akahauka, na akekaa hae kidogo na yuda mbwanga, uhaekana wa kwasa mshale, kwa via kagombeka, "Na nisekukaua fiie ya mwana." Ekuaho kekaa kumkabili, akaavya mwiiyo wakwe nguvu akaia. 17 Mungu akasikia uizi wa mwana, na malaika wa Mungu akamwetanga Hajiri kuawa mbinguni, akamwamba, "Ni mbwai kikusumbuacho? Usekuogoha, kwa kua Mungu kasikia uizi wa mwana hantu eiho. 18 Enuka mgoose mwana, na umwenke moyo; kwa kua n'ndanimgosoe kua taifa kuu." 19 Akaawaaho Mungu akayakubua meso ya Hajiri, na kaua akaona kisima cha mazi. Akaita akakimemeza kiliba mazi, na kumwenka mbwanga akanywa. 20 Mungu akawa hamwe na mbwanga, na akakua. Akekaa jangwani akawa mkaa. 21 Akekaa mwe jangwa da Parani, na mami yakwe akampatia mvee kuawa Misri. 22 Ikawa hambwe mwe ukati uda Abimeleki na Fikoli kamanda wa jeshi dakwe akamwamba Abraham, akagombeka, "Mungu yu hamwe na weye mwe yose uyagosoayo. 23 Sasa niapize kwa Mungu hambwe nkunaunigosweee baya, waa mwanangu, waa uvyazi wangu. Onesha kwangu na kwe sii ambayo neku ukekaa agano dia dia da uaminifu ambado nkikuoneha weye." 24 Abraham akagombeka, "Naapa." 25 Abraham pia akamlalamikia Abimeleki kuhusu kisima cha mazi ambacho wandima wa Abimeleki wawahoka. 26 Abimeleki akagombeka, "Nkimanya ni ndai mkugosoa mbui iyo. Nkukunambia mapema; na nkizati kudisikia ila ivyeo ivi." 27 Kwa hiyo Abraham akadoa ngoto na ng'ombe makisai akamwenka Abimeleki, na waidi awa wakagosoa agano. 28 Akaawaaho Abraham akawatenga wanangoto wa kivyee mpungati ikedu. 29 Abimeleki akamwamba Abraham, "Ni mbai maana ya awa wanangoto wa kivyee mpungati ambao huwatenga ikedu?" 30 Akaandua, "Awa wanangoto wa kivyee mpungati undauwahokee kuawa mwe mikono yangu, ili hambwe uwe ushahidi kwangu, kua nkifuka kisima iki." 31 Kwa iyo akahetanga hantu hada Beerisheba, kwa saabu hantu hada wose waidi waapa kiapo. 32 Wagosoa agano aho Bersheba, wakaawaaho Abimeleki na Fikoli, amili wa jeshi, wakauya mwe sii ya Wafilisti. 33 Abraham akahanda mti wa mkwaju mwe Beerisheba. Na hada akamvikia Yahwe, Mungu wa milele. 34 Abraham akabakia kua mgeni mwe sii ya Wafilisti kwa misi mingi.