Sura ya 1

1 Aho bosi Mungu kaumba mbingu na sii. 2 Nayo sii nkaikua na umbo na iwa bue. Kiza kiwa uanga ya cheni cha viindi vya mazi. Roho ywa Mungu kawa akaelea uanga ya cheni cha mazi. 3 Mungu akagombeka, "na kue na nuru," na kue na nuru. 4 Mugnu akaona kua nuru ni yedi. Akaipanga nuru na kiza. 5 Mungu akayetanga nuru "musi" na kiza akachetanga "Kio." Ikawa guoni na keo, msi wa bosi. 6 Mungu akagombeka, "na kue na anga gati ya mazi, na dipange mazi na mazi." 7 Mungu akagosoa anga na kuyapanga mazi yekuayo asi ya anga na mazi ambayo yawa uanga ya anga. Ikawa ivyo. 8 Mungu akayetanga anga "mbingu." Ikawa guoni na keo msi wa kaidi. 9 Mungu akagombeka, "mazi ye asi ya mbingu yekubehamwe hantu hamwe, na alizi nkavu ionekane." Ikawa ivyo. 10 Mungu akayetanga alizi nkavu "sii," na mazi ye kwekubayo akayetanga "bahai." Akaona kua ni vyedi. 11 Mungu akagombeka, sii ihote mimea: miche iavyayo mbeyu na miti ya matunda iavyayo matunda ambayo mbeyu zakwe ziumo ndani ya tunda, kia kintu kwa namna yakwe." Ikawa ivyo. 12 Sii ikaavya mimea, miche iavyayo mbeyu za aina yakwe, na miti iavyayo tunda ambado mbeyu yakwe iumo ndani yakwe, kwa aina yakwe. Mungu akaona kua ni vyedi. 13 Ikawa guoni na keo, msi wa ntatu. 14 Mungu akagombeka, "kue na mianga mwe anga kutenganisha msi na kio. Na ziwe kana ishala, kwa majila, kwa msi na miaka. 15 Ziwe mianga mwe anga ili kuavya mwanga uanga ya sii." Ikawa ivyo. 16 Mungu akagosoa mianga mikuu miidi, mwanga mkuu zaidi kutawala musi, na mwanga mdodo kutawala kio. Akagosoa nyota pia. 17 Mungu akazisawanya mwe anga kuavya mwanga uanga ya sii, 18 Kutawala musi na kio, na kusawanya mwanga kuawa kwe kiza. Mungu akaona kua ni vyedi. 19 Ikawa guoni na keo, msi wa nne. 20 Mungu akagombeka, "mazi yameme idadi nkuu ya viumbe wagima, na wadege waluke uanga ya sii mwe anga da mbingu," 21 Mungu akaumba viumbe vikuu vya bahalini, hamwe na kia kiumbe kigima cha aina yakwe, viumbe wendao na wamemao kia hantu mwe mazi, na kia mdege mwenye mabawa kwa aina yakwe. Mungu akaona kua ni vyedi. 22 Mungu akavibaiki, akamba, "Vyaeni na muongezeke, na mmeme mwe mazi bahalini. Wadege waongezeke uanga sii." 23 Ikawa guoni na keo, msi wa shano. 24 Mungu akagombeka, "sii na iavye viumbe wagima, na kia kiumbe kwa aina yakwe, mnyama wa kufugwa, vintu vitambaavyo, na wanyama wa sii, kia kintu kwa jinsi yakwe." Ikawa ivyo. 25 Mungu akagosoa wanyama wa sii kwa aina yakwe, wanyama wa kufugwa kwa aina yakwe, na kia kitambaacho uanga ya alizi kwa aina yakwe. Akaona kua ni vyedi. 26 Mungu akagombeka, "na timgosoe mntu mwe mfano wetu, wa kusimama na swiswi. Wawe na mamlaka uanga ya samaki wa bahali, uanga ya wadege wa angani, uanga ya wanyama wa kufuga, uanga ya sii yose, na uanga ya kia kintu kitambaacho ambacho tambaa uanga ya sii." 27 Mungu akaumba mntu kwa mfano wakwe. Mwe mfano wakwe akawaumba mgosi na mvyee akawaumba. 28 Mungu akawabaiki na akawamba, "Vyaeni na kuongezeka. Memezani sii, na muitawale. Mue na mamlaka uanga ya samaki wa bahalini, uanga ya wadege wa angani na uanga ya kia kiumbe kigima chendacho uanga ya sii." 29 Mungu akagombeka, "Kaua nkiwenka kia aina ya mmea uvyaao mbeyu ambao u uanga ya sii, na kia mti wenye tunda ambado dina mbeyu ndani yakwe. N'ndaviwe ni nkande kwenu. 30 Kwa kia mnyama wa sii, kwa kia mdege wa angani, na kia kitambaacho uanga ya sii, na kia kiumbe ambacho kina muye wa ugima nkiavya kia mmea kwa ajii ya nkande." Ikawa ivyo. 31 Mungu akaona kia kintu akukiumbacho kana, kikawa chedi sana. Ikawa guoni na keo msi wa mtandatu.