Sura 8

1 Ninatamani ungekua kama kaka yangu, aliyenyonya ziwa la mama yangu. Ila kila nilipokutana nawe nje ningekubusu pasipo mtu kunidharau. 2 Ningekuongoza na kukuleta kwenye nyumba ya mama yangu, --yeye aliyenifundisha. Ningekupa mvinyo uliochachwa unywe na baadhi ya jwisi ya komamanga. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe 3 Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu na mkono wake wa kulia wanikumbatia. Mwanamke akiongea na wanawake wengine 4 Ninataka muape; mabinti wa wanaume wa Yerusalemu, kuwa hamsha au kuchochea mapenzi yetu hadi yatakapo isha yenyewe. Wanawake wa Yerusalemu wakizungumza. 5 Ni nani huyu ambaye anakuja kutoka nyikani, akimuegemea mpenzi wake? Mwanamke mdogo akizungumza na mpenzi wake nimekuamsha chini ya mti wa mpera; pale mama yako alichukua mimba; pale alikuzaa, alijifungua wewe. 6 Niweke kama muhuri kwenye moyo wako, kama muhuri kwenye mkono wako, kwa kuwa mapenzi yana nguvu kama mauti. Mapenzi mazito hayana kurudi kama kwenda kuzimu; miale yake yalipuka; ni miale ya moto inayo waka, miale yenye joto kuliko moto wowote. 7 Maji yaliyozuka hayawezi kuzimisha upendo, wala mafuriko hayawezi kuuondoa. Mwanaume akitoa mali zake zote kwa ajili ya upendo, ukarimu wake utadharauliwa. Kaka zake mwanamke mdogo wakizungumza wenyewe 8 Tuna dada mdogo, na matiti yake bado hayajakua. Tutamfanyia nini dada yetu siku hatakayoahidiwa kuolewa? 9 Kama yeye ni ukuta, tutamjengea juu yake mnara wa fedha. Kama yeye ni mlango, tutampamba kwa mbao za mierezi. Mwanamke mdogo akizungumza peke yake 10 Nilikuwa ukuta, lakini matiti yangu sasa ni kama nguzo imara; hivyo nimekomaa machoni pake mleta amani. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe 11 Sulemani alikuwa na shamba la mizabibu huko Baali Hamoni. Aliwakodishia wao ambao wangelitunza. Kila mmoja alipaswa kuleta shekeli elfu moja za fedha kwa matunda yake. 12 Shamba langu la mzabibu ni langu hasa, li mbele yangu; shekeli elfu moja ni za kwako, Sulemani mpenzi, na shekeli mia mbili ni za wale wanaotunza matunda yake. Mpenzi wa mwanamke akizungumza naye. 13 Wewe unayeishi katika bustani, marafiki zangu wanasikiliza sauti yako; acha na mimi niwezekuisikia pia. Mwanamke mdogo akiongea na mpenzi wake 14 Harakisha, mpenzi wangu, na uwe kama paa au mtoto wa paa kwenye milima ya manukato.