Sura 1

1 Tamko kuhusu Ninawi. Kitabu cha maono ya Nahumu, Mwelkoshi. 2 Yehova ni Mungu mwenye wivu na mlipiza kisasi; Yehova hulipiza kisasi na amejaa ghadhabu; Yehova ni Mungu hulipiza kisasi kwa adui zake, na huiendeleza hasira yake kwa adui zake. 3 Yehova si mwepesi wa hasira na ni mwenye nguvu; hatawahesabia haki watu waovu. Yehova hufanya njia yake kwenye upepo wa kisulisuli na dhoruba, na mawingu ni mavumbi ya miguu yake. 4 Huikemea bahari na kuifanya ikauke; hukausha mito yote. Bashani ni dhaifu, na Karmeli pia; maua ya Lebanoni imekuwa dhaifu. 5 Milima hutetemeka uweponi mwake, na vilima huyeyuka; nchi huanguka mbele zake, kweli, dunia na watu wote wanaoishi ndani yake. 6 6Nani anaweza simama mbele ya ghadhabu yake?Nani anaweza zuia ukali wa hasira yake?Ghadhabu yake imemwagwa kama moto,na miamba ameipasua. 7 Yehova ni mwema, boma katika siku ya taabu; na yeye huwatambua wale wanaomkimbilia. 8 Lakini atafanya mwisho wa adui zake kwa mafuriko ya kutisha; atawawinda kwenye giza. 9 Watu wanapanga nini dhidi ya Yehova? Yeye atakomesha; taabu haitainuka mara ya pili. 10 Kama michongoma na kama mvinyo wa walewao ,wataharibiwa kama mabua makavu. 11 Kutoka kwako, Ninawi, amejitokeza mmoja ambaye alipanga uovu dhidi ya Yehova ,mshauri muovu. 12 Hivi ndivyo anavyosema Yehova, "Hata kama wana nguvu zao timilifu na idadi timilifu, hata hivyo wataondolewa; watu wao hawatakuwepo tena. Lakini wewe, Yuda: Ingawa nimekutesa, sitakutesa tena. 13 Sasa nitaivunja ile nira ya watu kutoka kwako; nitaikata minyororo yako". 14 Yehova ametoa amri juu yako, Ninawi: " Hakutakuwa na uzao tena utakaoendeleza jina lako. Nitaharibu sanamu zilizochongwa na kuziondoa sanamu za chuma kutoka kwenye nyumba za miungu yenu. Nitaandaa kaburi lako,kwa kuwa umedharauliwa." 15 Tazama, juu ya milima kuna miguu ya mtu aletaye habari njema, anayetangaza amani! Sherehekeeni sikukuu zenu, Yuda, na timizeni nadhiri zenu, kwa maana yule mwovu hatawavamia tena; ameondolewa kabisa.