1
Tazama, siku inakuja, inawaka kama tanuru, ambayo wote wenye kiburi na waharifu watakuwa mabua. siku inakuja itawachoma," asema Bwana wa Majeshi, "siku hiyo itaondoa mzizi au shina.
2
Lakini kwenu mnaoliogopa jina langu, jua la haki litawaangazia na uponyaji katika mbawa zake. Mtarukaruka kama ndama zizini.
3
Na waovu wote mtawakanyaga chini, watakuwa majivu chini ya nyazo za miguu yenu siku hiyo nitatenda," asema Bwana wa Majeshi.
4
Kumbukeni kutii sheria za mtumishi wangu Musa, mmri na sheria nilizomwamuru huko Horebu, kwa Israel wote.
5
Tazama, nitamtuma Eliya nabii mbele yenu kabla ya siku kuu na yenye kutisha ya kuja kwa Bwana.
6
Atarudisha moyo wa baba kwa watoto, na mioyo ya watoto kwa baba zao; ili kwamba nisije nikaiangamiza nchi kwa uharibifu wote."